Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-05-22 15:18:11    
Barua 0520

cri

Msikilizaji wetu Paul Mungai Mwangi wa shule ya msingi Mwiteithia , engineer, S.L.B 69 North Kinangop Nchini Kenya ametuletea barua akiwasalimu watangazaji wote wa idhaa ya Kiswahili ya radio china kimataifa, msikilizaji wetu yeye ni mzima akiendelea kuitegea sikio idhaa ya Kiswahili ya radio China Kimataifa.

Katika barua yake hii kwa kwanza anatoa shukrani zake kwa zawadi murua alizotumiwa na kwa hakika aimemfanya apate hamasa zaidi ya kuendelea kuisikiliza radio China Kimataifa.Na hivi karibuni amepokea kalenda ya mwaka 2007, na zawadi zote hizo huzitundika ukutani ambapo wageni na marafiki hupata nafasi ya kuziona, na jambo lilimfurahisha zaidi ni kusikia jina lake kwa mara ya kwanza likisomwa katika kipindi cha salamu.

Jambo la pili Bwana Mungai anasema, akiwa msikilizaji wa dhati wa radio china Kimataifa hujaribu kadiri ya uwezo wake kuwahamasisha marafiki na majirani zake wajiunge na radio china Kimataifa ili waweze kufahamishwa,kuelimishwa na kuburudishwa.Na juhudi zake sasa zimezaa matunda kwani wengi wao sasa wanafurahia kuisikiliza Radio China Kimataifa.

Msikilizaji wetu huyu pia anaendelea kusema kuwa, ni ukweli usiofichika kuwa matangazo ya CRI yanaambatana na hali halisi, ukweli unadhiirika waziwazi katika vipindi vyote.Kwa mfano kipindi cha safari nchini China huyateka mawazo ya wasikilizaji na kujiona kama wanazitembelea sehemu mbalimbali nchini China.Hivyo kwa kuwa China ni nchi moja ya nchi zinazoendelea kwa kasi duniani hivyo CRI ingefaa kuongeza muda wa matangazo yanayohusu China ili kuwaelimisha watu wa Afrika ya mashariki jinsi ya kuinuka kiuchumi.

Anamalizia barua yake kwa kueleza furaha yake baada ya kusikia Mtangazaji mahiri wa CRI Mama Chen ameongezewa muda wa kufanya kazi badala ya kustaafu na hata atakapostaafu mwakani ataendelea kutumia ujuzi wake katika idhaa ya Kiswahili ya radio China Kimataifa

Msikilizaji wetu Joseph Mukaburu Wasire wa Muungano salamu club, S.L.B 1031 Bungoma nchini Kenya anaanza barua yake kwa kuwasalimia watangazaji wote wa idhaa ya Kiswahili ya CRI, vilevile anapenda kuwashukuru na kuwaombea watangazaji wote wa CRI maisha mema na marefu ili muendeleee na kazi nzuri ya kurusha matangazo kuhusu habari za dunia na China, chemsha Bongo, utamduni, kichina na habari za Afrika, ka hayo yote anatoa pongezi nyingi sana.

Bwana Wasire anaiomba idhaa ya Kiswahili ya CRI iongeze muda wa matangazo kwa wasikilizaji na pia CRI ifanye mpango wa kukutana na wasikilizaji angalau mara mbili kwa mwaka.

Mwisho anaishikuru CRI kwa kuwakumbuka wasikilizaji wakati wa kusherekea miaka 65 ya CRI na anashukuru pia kwa kalenda ya mwaka 2007, yeye pamoja na wasikilizaji wengine kama vile Telly Wambwa,Ayub Mtanda,, Richard Wekesa na wengine wengi wanawakaribisha wafanyakazi wa CRI mjini Bungoma.

Msikilizaji wetu Paul N. Sirengo S.L.P 172 Bungoma Kenya natoa salamu nyingi za mwaka mpya kwa wafanyakazi wote wa idhaa ya Kiswahili ya CRI,yeye ni mzima wa buheri wa afya.

Dhumuni la barua yake kwanza ni kutoa shukrani shukrani kwa kazi nzuri inayofanywa na idhaa ya Kiswahili ya CRI, kwa hakika mpangilio wa vipindi ni mzuri na wenye utaratibu na wenye kutia for a.

Pili ana furaha sana kubwa isiyo kifani kwa zawadi ambazo ametumiwa na wanazotumiwa wasikilizaji mara kwa mara, kwa hakika kama mtatembelea kwangu mtakuta mapambo kama vile ninaishi nchini China wakati nipo nchini Kenya, ndivyo anavyosema msikilizaji wetu huyu.Mapambo alinayo ni pamoja na kalenda na picha zinazoonyesha majengo mbalimbali ya Beijing.

Bwana Sirengo anaendelea kusema kuwa kupitia vipindi vya CRI amejifunza mambo mengi kuhusu utamaduni wa China, na kwa kweli ni wenye kutia fora sana, mpaka anatamani kufika nchini China ili ajionee kwa macho.

Mwisho wa barua yake anapenda kuwasihi wasikilizaji wote waendelee kuwsiliana kupitia Radio China Kimataifa na wale ambao wanatamani kujiunga milango iko wazi.

Msikilizaji wetu Andrew Pilla, wa S.L.P. 36 Bunyore nchini Kenya ametuletea barua kwa mtangazaji mpendwa, anasema, salamu nyingi ziwafikie wote watangazaji wa idhaa ya kiswahili ya CRI. Yeye ni mzima na anaendelea na kufurahia mpangilio wa vipindi vya CRI ni wa haki na unaambatana na wakati. Pongezi kwa sherehe ya kudhimisha miaka 65 ya CRI. Pia kwa hiki kituo cha FM kilichoko Nairobi ingawaje hakisikiki kwa upande wetu wa kakamega kwa hali nzuri.

Anawapongeza washindi wa nafasi maalum na CRI kwa kuwaalika wasikilizaji hao kwenda kuhudhulia sherehe za miaka 65 ya CRI.

Pongezi kuwa Barua na Zawadi mnazotoa wasikilizaji ambazo na mimi pia nimezipata.

Nawatakia kila laheri kwa vipindi na matangazo yote ya mwaka 2007, huku nikiendelea na juhudi za kuzikiliza CRI na marafiki zangu na Mungu awabariki wafanyakazi wote wa CRI na Wananchi wote.

Msikilizaji wetu Benson Irungu anayetuziwa barua zake na Njamuya S.L.P. 832 Murancia Kenya kwanza kabisa anachukua fursa hii kumshukuku Rabuka kwa kumuwezesha kuwasiliana na radio china kimataifa kupitia kwenye njia hii ya kalamu na karatasi licha ya hayo ana shukuru sana kwa picha nzuri na zawadi na pia kwa kukubukwa kwenye shindano la chemsha mbongo.

Mwana sayansi Isaac Newton (1643-1727) wa uingereza msomi huyo alisema kila tendo lina kinyume chake, katika msingi huu, mtu akiiba anapambana na mkono wa sheria na kulipia matendo yake maovu. kila tendo lina mwangwi (echo) mwangwi ni sauti inayosika mtu apigapo kelele katika chumba kisichokuwa na kitu, ndani ya pango kubwa au kati ya milima. Kila tuna potenda ni muhimu tuzingatie tendo lenyewe nia yake, mazingira yake na matokeo yake matokeo ya tendo ni sawa na mavuno. Kuna matendo ambayo ni mazuri kwa jinsi yalivyo tu mfano ni kusoma kuzungumza vizuri na watu na kusali. Mazungumzo nayo yana sehemu yake katika kufanya tendo kuwa jema sana au mbaya sana. mahakama zinatumia ushahidi wa kimazingisa kwa mfano mtu anayeonekana mahali fulani kisha kitu kipotee mahali pale huwa mshukiwa wa kwanza kuna vpimo vya matendo mema na vipimo hivyo ni uzuri wa matendo yenyewe mazingira yake matokeo yake na nia au lengo la mtendaji

Msikilizaji wetu Machuki M Philip wa Nyakwale CRI -List Club, S.L.P 646 Kisii nchini Kenya anaanza barua yake kwa kutoa salamu za mwaka mpya wa 2007 kwa wafanyakazi wote wa idhaa ya Kiswahili ya CRI, yeye ni mzima na anamshukuru Mungu kwa kuwapatia mvua nyingi huko Kisii.

Bwana Machuki anapenda kuchukua fursa hii kutoa pongezi zake kwa yale yote ambayo idhaa ya Kiswahili ya CRI imewafanyia wasikilizaji wake kwa kipindi chote cha mwakla 2006. Kwa kweli mwaka 2006 ulikuwa mwaka wa mafanikio kati ya idhaa ya Kiswahili ya CRI na wasikilizaji wake, kwani baadhi ya wasikilizaji walipata fursa ya kutembelea China wakati wa maadhimisho ya miaka 65 ya CRI.

Ni matarajio yake kuwa mwaka huu wa 2007 watanufaika na mengi na hasa daraja la urafiki litachapishwa tena mwaka huu na CRI itaendelea kuwatumia bahasha zilizolipiwa ili wasikilizaji wazidi kuwasilina na CRI.

Msikilizaji wetu huyu anaendelea kusema kuwa mwaka huu klabu ya Nyakwale Listerners itashiriki katika chemsha bongo na wanashukuru kwa kuwa tayari wameshapokea fomu na bahasha zilizolipiwa na kwa sasa wanajiandaa kutuma majibu haraka iwezekanavyo.

Katika klabu yao kuna wanacha wapya ambao wanatoa pongezi kwa matangazo ya idhaa ya Kiswahili ya CRI na wanapenda kuwa katika orodha ya wasikilizaji, nao ni: Jude Kerubo S.L.B 222 Kisii 40200-Kenya, Daudi Bundi Gusii Institute of Technology S.L.P 222 Kisii 40200-Kenya,Vanice Abuya Abuya Gusii Insitute S.L.P 222 Kisii 40200 Kenya,Mercy Ombati S.L.P 222 Kisii 40200 Kenya

Mseikilizaji wetu Jendeka Vuyiya wa S.L.P 172 Bungoma nchini Kenya anaanza barua yake kwa kutoa salamu nyingi na shukrani nyingi kwa wafanyakazi wote wa idhaa ya Kiswahili ya Radio China Kimataifa, na anayo furaha kubwa kusikia kuwa muda wa Mama Cheni kustaafu umeongezwa.

Kwa muda wa siku kadhaa alikua safarini katika mkoa wa magharibi wa Kenya ambapo alikutana na wasikilizaji wengi wa CRI, na alivyorejea nyumbani alikuta barua mbili ikiwemo kadi ya salamu, kalenda na maswali ya chemsha Bongo ya mwaka huu kuhusu mkoa wa Sichuan ambao amefahamishwa una vivutio vingi vya utalii. Bwana Vuyiya anapenda kutujilisha kuwa atashiriki kikamilifu katika chemsha Bongo na lengo likiwa si lazima awe mshindi bali aweze kuelewa zaidi mkoa wa Sichuan na vivutio vyake.

Msikilizaji wetu anaendelea kusema kua ni idhaa ya Kiswahili ya CRI pekee ulimwenguni yenye uhusiano mzuri na wasikilizaji wake, hivyo anaomba CRI iendelee hivyo hivyo siku zote. Anamalizia barua yake kwa kuwatakia kila heri wafanyakazi wote wa idhaa ya Kiswahili ya CRI

Msikikilizaji wetu Evans Amwai wa S.L.P 37 Maragoli Kenya ametuletea barua akisema Pongezi kwa nchi ya China kwa kuendeleza miradi mingi humu nchini kama vile ujenzi wa Moi International Sport Centre (Kasarani). Barabara ya Kipsigak-Serem-Shamakhokho. Kwa Sababu ya ukosefu wa kazi, sijakuwa nikizikiliza vipindi vya CRI kwa siku za karibuni kwa hivyo Samahani kwa Kutojibu maswali yenu.

Ili Kujifahamisha mengi kuhusu nchi yenu mzuri ya China, naomba kazi kwa kituo chenu cha Radio ili kuendelea kufurahia vipindi vyenu pamoja na kujipatia mkate wangu wa kila siku. Pamoja nina imani tutasaidiana kuendeleza kituo hiki maarufu cha CRI.

Pamoja na hayo, nitafurahi zaidi ikiwa mtanipa nafasi ya kutembelea nchi yenu ya China. Ili kujifahamisha na kuona uzuri wa miji mizuri ya nchi yenu.

Ni tumaini langu ya kuwa mtawasiliana nami wakati wowote kwa nambari hizi za simu 0727850034 au hata kwa barua.

Idhaa ya kiswahili 2007-05-22