Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-05-22 19:00:19    
Wateja wa Marekani wapenda "Made in China"

cri

Mmarekani Mike, ambaye ni mkazi wa Washington, wiki iliyopita alinunua kofia moja. Bw. Mike anaipenda sana kofia hiyo, si kwa kuwa bei yake ni rahisi tu, bali ni kofia iliyotengenezwa vizuri na kusifiwa na watu wengi. Watu wengine kutoka katika familia yake walitaka pia kununua kofia kama yake, baada ya kuangalia nembo yake, na kugundua kumbe kofia hiyo ilitengenezwa nchini China! "Made in China" siyo kitu kigeni kwa wamarekani, maneno hayo yameingia majumbani kwa watu wa Marekani, vitu vilivyozalishwa nchini China vimewanufaisha kihalisi.

Kwenye duka moja kubwa karibu na mji wa Washington, Bw. Mike alimweleza mwandishi wetu wa habari kuhusu kofi aliyonunua. Alisema, anapenda vitu vilivyotengenezwa nchini China.

"Bidhaa za China ni za bei rahisi, tena ni bora. Ni kama bidhaa za Japan zilivyokuwa mwanzoni, bidhaa hizo ni vitu vidogo vidogo na vitu vya kuchezea watoto, lakini hivi sasa bidhaa za China ni nguo na kofia ambazo ni nzuri sana. Nguvu kazi ni ya gharama ndogo, lakini ufundi ni mkubwa."

Bw. Mike alisema, kadiri siku zinavyopita, aina za bidhaa za China pia zinaongezeka, kati ya asilimia 30 na 40 za vitu vinavyohitajika katika maisha yake vinatoka China. Anapenda bidhaa rahisi na bora za China.

Watu wa Marekani wanaopenda bidhaa za China wamekuwa wengi. Bw.Johari Hamilton, ambaye ni mfanyakazi wa teknolojia ya kompyuta, alisema, zaidi ya 50% za bidhaa alizonunua ni kutoka China. Alisema, sababu ya kutumia bidhaa za China ni bidhaa nzuri, hususan ni kuwa wamarekani wanaponunua bidhaa kitu wanachojali zaidi ni bei rahisi. Bidhaa zilizozalishwa nchini China, zinaendana na mahitaji ya wamarekani wengi.

"Tunapenda kuwa na vitu vingi. Wateja wa Marekani wanapenda bidhaa za bei rahisi. Hii ndiyo hali unayoiona katika wikiendi. Ifikapo wikiendi, karatasi za matangazo ya biashara zinaonekana kila mahali. Mama yangu anapenda sana kusoma matangazo hayo, hajali anahitaji vitu gani, anafuatilia vitu vya bei rahisi tu. Ujue kwamba bei rahisi ni muhimu zaidi kuliko mengine yote."

Hivi sasa Marekani imekalia soko la bidhaa za teknolojia ya kisasa na soko la rasilimali, wakati bidhaa zinazosafirishwa na China nchini Marekani nyingi zaidi ni bidhaa za kiwango cha wastani na chini, zinazohusika na maisha ya watu. Sababu za bidhaa za China kupendwa sana na watu ni kuwa bidhaa hizo, zimerahisisha maisha ya wamarekani na kuwanufaisha. Vitu vya bei rahisi kwa wamarekani ni kama kuongezwa pato, na kuwawezesha kuishi vizuri zaidi kwa pato lao lilelile. Takwimu za Benki ya Dunia zinaonesha kuwa, bidhaa zilizosafirishwa na China kwenda Marekani zinaokoa dola za kimarekani bilioni 100 kwa mwaka. Takwimu za wizara ya kazi ya Marekani zinasema, pamoja na kuongezeka kwa bidhaa za China, bei za vitu vinavyouzwa kwa rejareja nchini Marekani zinashuka hivi sasa. Tokea mwaka 1998, bei za televisheni zinapungua kwa 9% kwa mwaka, bei za vyombo vidogo zinapungua kwa 1% kwa mwaka, wakati bei za vyombo vya michezo ya kuimarisha mwili zinapungua kwa 3% kwa mwaka. Katika maisha ya wamarekani walionufaika kutokana na bidhaa za China, hivi sasa hawakubali kukosa bidhaa zilizotoka China.

Uhusiano wa biashara wa China na Marekani unaendana na hali ya masoko. Pande mbili zinaweza kuafikiana kwenye mkataba wa biashara, inaonesha kuwa inaendana na maslahi ya pande mbili. Mfanyakazi wa idara ya biashara ya kimataifa wa Marekani Bw. Surensh alisema, bidhaa za China kuingia nchini Marekani ni kutokana na mahitaji ya soko, ambapo wafanyabiashara wa Marekani walifanya kazi kubwa. Ingawa mwanzoni ubora wa bidhaa za China haukuwa mzuri, lakini uliinuka hapo baadaye, na siku za mbele hakika zitakuwa bidhaa zinazotoa changamoto kwa bidhaa maarufu za duniani.

Bila shaka, pamoja na maendeleo ya uhusiano wa biashara wa China na Marekani, wateja wa Marekani watanufaika zaidi.