Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-05-23 18:56:06    
Mji wa Baoding wajitahidi kujenga mji unaotumia nishati ya mionzi ya jua

cri

Hivi sasa, China inajitahidi kuendeleza nishati mpya zikiwemo nishati ya upepo, jua na joto la ardhi, ili kubadilisha hali ya kutegemea nishati za kawaida kama vile makaa ya mawe, mafuta na gesi za kimaumbile. Mji wa Baoding ulioko kaskazini mwa mkoa wa Hebei, nchini China, ni mfano mmoja wa juhudi hizo, kwani unajenga mji unaotumia nishati ya mionzi ya jua.

Kwa kawaida, taa za ishara za barabarani zinatumia umeme. Lakini mjini Baoding, zana moja maaluma yaani ubao wa kukusanya nishati ya mionzi ya jua (solar panel) imewekwa kwenye kila taa za barabarani, zana hiyo inaweza kubadilisha nishati ya mionzi ya jua kuwa umeme, ili kuhakikisha taa hizo zinaweza kufanya kazi kama kawaida.

Taa za ishara za aina hiyo mpya, si kama tu hazihitaji nishati ya umeme, bali pia hazichafui mazingira hata kidogo. Imefahamika kuwa, tangu taa hizo zilipoanza kutumiwa mjini Baoding, mara moja zilikuwa zinafuatiwa na wakazi wa mji huo. Wakazi kadhaa wanasema:

"naona taa za aina hiyo zinapunguza sana matumizi ya umeme, ni nzuri sana."

"kwetu taa zote za ishara za barabarani zimebadilishwa kuwa za aina hiyo. Taa hizo ni nzuri sana, si kama tu hazitumii nishati ya umeme, bali pia hazichafui mazingira. Jambo hilo ni nzuri kwetu sisi wakazi wa hapa na hasa taifa letu zima."

Ofisa husika wa idara ya usimamizi wa mawasiliano barabarani ya huko Bw. Liu Tao alisema, hivi sasa mji wa Baoding umekamilisha kazi ya marekebisho ya sehemu 22 za kupitanisha njia na kuweka taa za ishara za barabarani zinazotumia nishati ya mionzi ya jua kwenye sehemu hizo, ambazo zinachukua asilimia 20 ya sehemu hizo zote mjini humo. Bw. Liu Tao alisema:

"taa za aina hiyo zina manufaa mawili, ya kwanza ni kuwa zimebadilisha njia ya utoaji wa nishati, ya pili ni kuwa taa hizo zinatumia mfumo wa mawasiliano usio na waya."

Mbali na kuweka taa za ishara za aina hiyo kwenye baadhi ya sehemu muhimu mjini, mji wa Baoding pia umeweka taa zinazotumia nishati ya umeme mitaani. Mhandisi mkuu wa idara ya usimamizi wa taa za barabarani wa mji huo Bw. Zhao Wangzeng alieleza, mji huo ulianza kuweka taa za aina hiyo mwaka mmoja uliyopita, mpaka sasa, jumla taa milioni 2 za aina hiyo, zinatumika mitaani. Bw. Zhao Wangzeng alisema:

"kwa kawaida, mitaa ya mji huo inatumia taa za wati 250, kama kila taa ikifanya kazi kwa saa 10 kila siku, kila taa inatumia kilowati saa 3 za umeme . Mwaka jana gharama za matumizi ya umeme kwa ajili ya taa hizo zilifikia zaidi ya yuan milioni 15. kutokana na kuenezwa kwa vifaa vya kupunguza matumizi ya nishati na taa zinazotumia nishati ya mionzi ya jua, gharama za umeme zitapungua kwa kiasi kikubwa."

Kwa mujibu wa Bw. Zhao Wanzeng, mwaka huu idara husika za huko, pia zinapanga kuweka taa 50 za barabarani zinazotumia nishati ya mionzi ya jua kwenye barabara kuu mbili za mji huo, ili kueneza zaidi matumizi ya taa za aina hiyo.

Aidha, idara husika za mji huo pia zimerekebisha taa za barabarani kwenye sehemu nyingi za makazi na bustani, sehemu moja ya makazi inayoitwa Mingchangyuan ni kundi la kwanza la maeneo ya makazi, lililofanyiwa marekebisho hayo. Mzee Zhang anayeishi kwenye sehemu hiyo alisema:

"taa za barabarani zinazotumia nishati ya mionzi ya jua haziathiriwi na kukatika kwa umeme, na zitawaka wakati usiku unapoingia. Taa za aina hiyo zina umbo mzuri, pia zinapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya nishati."

Imefahamika kuwa, shughuli hizo zote za mji wa Baoding haziwezi kuondokana na hali mwafaka ya mwangaza wa jua wa huko. Sekta ya nishati ya mionzi ya jua ya mji huo imeendelea kuchukua nafasi ya kwanza nchini China. Katika miaka ya 90 ya karne iliyopita, kampuni ya nishati mpya ya Tianweiyingli, ambayo ni kiwanda kikubwa kabisa cha kuzalisha betri ya nishati ya mionzi ya jua nchini China, ilianzishwa kwenye eneo la teknolojia mpya na ya hali ya juu la mji wa Baoding.

Hivi sasa, shughuli za marekebisho ya nishati ya mionzi ya jua mjini Baoding zimeleta manufaa kama ilivyotazamiwa. Taa za barabarani na taa za ishara zinazotumia nishati ya mionzi ya jua zote zinaweza kufanya kazi kwa saa 6 hadi 7 usiku kwa kutumia nishati ya mionzi ya jua iliyokusanywa wakati wa mchana. Naibu mkurugenzi wa kamati ya maendeleo na mageuzi ya mji wa Baoding Bw. Cao Jidong alisema, kwenye msingi wa mafanikio hayo yaliyopatikana, katika miaka kadhaa ijayo, mji huo utaeneza kikamilifu matumizi ya jumla ya nishati ya mionzi ya jua katika mifumo ya kutoa mwanga, kutoa maji moto na kuleta joto nyumbani, ili kujenga mji unaotumia nishati ya mionzi ya jua. Bw. Cao Jidong alisema":

"tunapanga kutumia miaka 3 hadi 5 kurekebisha mifumo yote ya kutoa mwanga na kuleta joto nyumbani, hasa kwenye maeneo mapya ya makazi, kuwa ya kutumia nishati ya mionzi ya jua. Tunaamaini kwamba baada ya kufanya juhudi kwa miaka 3 hadi 5, mpango wa ujenzi wa mji unaotumia nishati ya mionzi ya jua hatimaye utatimizwa."