Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-05-23 19:28:46    
Mapishi ya nyama ya ng'ombe na nyanya

cri

Mahitaji

Nyama ya ng'ombe gramu 300, nyanya gramu 300, pilipili mboga mbili, vitunguu maji gramu 5, vitunguu saumu gramu 5, tangawizi gramu 5, mchuzi wa sosi vijiko viwili, chumvi kijiko kimoja, sukari kijiko kimoja, pilipili manga vijiko viwili, maji ya wanga vijiko viwili.

Njia

1. kata nyama ya ng'ombe iwe vipande, vipande changanya pamoja na vijiko viwili vya mafuta, weka kwenye sufuria na mimina mabakuli matano ya maji, baada ya hapo washa moto, na chemsha kwa saa moja.

2. kata nyanya na pilipili mboga ziwe vipande vipande.

3. washa moto tia mafuta kwenye sufurtia, tia pilipili mboga kwenye sufuria na korogakoroga, halafutia vipande vya vitunguu maji, vitunguu saumu na tangawizi, na korogakoroga, baada ya hapo tia vipande vya nyama ya ng'ombe na nyanya, korogakoroga, kasha tia mchuzi wa sosi, chumvi, sukari na pilipili manga korogakoroga, halafu mimina maji kidogo na chemsha kwa dakika 3, baada ya hapo mimina maji ya wanga korogakoroga na kasha ipakue. Mpaka hpo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.