Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-05-23 20:29:20    
Harakati za kupanda miti bilioni 1 duniani zapata mafanikio ya mwanzo

cri

Tarehe 22 Mei mwaka huu ilikuwa ni siku ya aina nyingi za viumbe duniani. Siku hiyo Shirika la mpango wa mazingira la Umoja wa Mataifa kwenye makao makuu yake yaliyopo mjini Nairobi, Kenya lilisema, tangu harakati za kupanda miti bilioni 1 ianzishwe na Umoja wa Mataifa mwaka jana, idadi ya miti ambayo pande mbalimbali ziliahidi kuipanda kote duniani imezidi bilioni 1. Habari hiyo inawatia moyo watu na kuvutia ufuatiliaji wa watu kuhusu suala la kuhifadhi mazingira.

Harakati hizo za kupanda miti bilioni 1 zilianzishwa na Umoja wa Mataifa tarehe 8 Novemba mwaka jana. Katika miezi iliyofuata, nchi mbalimbali zilionesha hamu kubwa ya kushiriki kwenye harakati hizo. Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa shirika la mazingira Bw. Achim Steiner alijumuisha maendeleo ya harakati hizo.

Anasema, "Hadi ilipofikia miezi minne baada ya kuanzishwa kwa harakati hizo, pande mbalimbali zilikuwa zimeahidi kupanda miti zaidi ya bilioni 1, na miti iliyokuwa imeshapandwa ilifikia kati ya milioni 14 na milioni 16. Kwa hiyo kama una shauku yoyote, subiri miezi mingine 10 ambapo utaona kitakachotokea."

Takwimu zinaonesha kuwa, tangu serikali ya Senegal itangulie kutoa ahadi ya kupanda miti milioni 20, pande mbalimbali zimeahidi kupanda miti mingine bilioni 1.012.

Bw. Steiner anasema "Vyombo mbalimbali vikiwemo shule chekechea, makampuni na idara za serikali za mikoa, zimetoa ahadi hadharani. Swali ni kwamba, je ahadi hizo zitatekelezwa? Mimi najibu ndiyo. Kwani watu hawakulazimishwa kutoa ahadi hizo, na nchi mbalimbali kama vile Mexico, Senegal na Mauritania hazikutoa ahadi kwa ajili ya shirika la mazingira au vyombo vya habari, au kwa ajili ya kuwaonesha watu nia ya kutoa ahadi tu, watu na nchi hizo zitakosolewa na watu kwa kushindwa kutekeleza ahadi zao baada ya miezi 12. La hasha! Naona kuhusu suala la upandaji miti, kila mmoja alitoa ahadi kwa makini."

Hivi sasa utekelezaji wa ahadi hizo ni suala linalofuatiliwa sana na watu. Profesa Wangari Maathai kutoka Kenya aliyewahi kupata tuzo ya amani ya Nobel kutokana na kuwaongoza wanawake wa Afrika kupanda miti zaidi ya milioni 30 katika nchi zaidi ya 20 barani Afrika, pia ni mshiriki wa harakati hizo za Umoja wa Mataifa. Alieleza kuwa inatakiwa mtu mmoja mmoja atoe mchango kwa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, mchango huo ni mdogo, lakini ni muhimu. Hili ni lengo la harakati za kupanda miti bilioni 1.

Anasema "Ndiyo, labda miti hiyo bilioni 1 haiwezi kubadilisha hali ilivyo sasa ya kuongezeka kwa joto duniani, lakini shughuli hizo za kupanda miti bilioni 1 ndani ya miezi 12 ni ishara kwamba, binadamu wamekuwa tayari kuchukua hatua kubwa kadhaa. Tunafahamu kuwa, ili kukabiliana na kuongezeka kwa joto duniani, inapaswa sisi tuchukue hatua kubwa zaidi ambazo hazijawahi kutokea, kwani tunafahamu umuhimu wa suala hilo, tunafahamu kuwa hali ya kuongezeka kwa joto duniani haiwezi kuzuiliwa, pia tunafahamu kuwa hali hiyo inaweza kubadilisha hali ilivyo sasa kwa kutumia mbinu za sayansi na teknolojia na upandaji miti."