Mazungumzo ya pili ya uchumi wa kimkakati kati ya China na Marekani yamemalizika tarehe 23 Mei huko Washington. Katika mazungumzo hayo ya siku mbili, pande hizo mbili zilibadilishana maoni kuhusu huduma za fedha, nishati na uhifadhi wa mazingira, na ongezeko la uwiano la uchumi, na zilifikia maoni mengi ya pamoja.
Mjumbe maalumu wa rais Hu Jintao wa China ambaye pia ni naibu waziri mkuu wa China Bibi Wu Yi alipotoa hotuba kwenye ufungaji wa Mkutano wa mazungumzo alisema, chini ya juhudi za pande zote, mazungumzo ya pili yamepata mafanikio. Alisema:
Pande mbili zilijadili kwa kina masuala ya uchumi wa kimkakati yanayohusika na mambo yote ya muda mrefu ya China na Marekani, pia zilijadili masuala kadhaa yanayofuatiliwa zaidi kuhusu uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani kwa hivi sasa, matokeo halisi yamepatikana kwenye mazungumzo.
Bibi Wu Yi alisema, ushirikiano wa nishati na uhifadhi wa mazingira ni masuala muhimu yaliyojadiliwa kwenye mazungumzo hayo, pande hizo mbili zina maslahi mengi ya pamoja katika sekta hizo, ambapo zimefikia maoni mengi ya pamoja, na kuahidi kufanya juhudi halisi. Hii ina umuhimu mkubwa kwa hali ya hivi sasa ambayo watu wa dunia nzima wanafuatilia usalama wa nishati na uhifadhi wa mazingira.
Suala kuhusu uvumbuzi lilijadiliwa zaidi kwenye mazungumzo hayo. Hivi sasa China inafanya juhudi katika kujenga nchi inayofanya uvumbuzi, na Marekani imekuwa na uzoefu mkubwa katika sekta hiyo, ambayo inaweza kufanya maingililano na China, na uzoefu wake unastahili kuigwa na China. Mazungumzo hayo yameweka msingi kwa kuzidisha ushirikiano kati ya pande hizo mbili kwenye sekta hiyo.
Bibi Wu Yi alisema, mawaziri 33 wa China na Marekani wameshiriki kwenye mazungumzo hayo, hii imeonesha vilivyo kwamba, China na Marekani zinatilia maanani sana maendeleo ya utaratibu wa mazungumzo ya kimkakati na maendeleo mazuri ya utulivu ya uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili.
Katika hotuba yake, Bibi Wu Yi alidhihirisha pia kuwa, uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani unahusika na sekta nyingi mbalimbali, hivyo matatizo ya kiuchumi na kibiashara yaliyotokea katika uhusiano huo, yanatakiwa kushughulikiwa ,badala ya kutoa tishio na vikwazo. Alisema:
Uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani ni moja kati ya uhusiano wenye utatanishi mkubwa kabisa duniani kwa hivi sasa. Uhusiano huo unahusiana kwa kina na sekta nyingi mbalimbali kuliko uhusiano wowote wa kiuchumi na kibiashara duniani. China na Marekani zina uhusiano mkubwa, ambao unahusiana na mambo mengi kabisa karibu na kila kitu, tukitaka kushughulikia vizuri uhusiano huo, na kusukuma mbele maendeleo ya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani, tunapaswa kufanya mashauriano na mazungumzo ya moja kwa moja.
Mjumbe maalumu wa rais Bush, ambaye pia ni waziri wa fedha, Bwana Henry Paulson, alipohutubia, alidhihirisha kuwa, katika mazungumzo hayo, China imeonesha vilivyo msimamo wake wa ufunguaji mlango na juhudi zake hizo, zimeipa Marekani kumbukumbu nyingi. Alisema:
Pande mbili za Marekani na China zimefikia maoni mengi ya pamoja kuhusu huduma za fedha, nishati, mazingira na safari za ndege za abiria. Ingawa tunatakiwa kufanya kazi nyingi siku zijazo, lakini mpaka sasa tumepata matokeo kadhaa halisi, matokeo hayo ni ishara kubwa katika njia ya ushirikiano wa kimkakati wa muda mrefu kati ya Marekani na China, ambayo yameimarisha imani ya pande zote mbili na kutuhimiza tuendelee kusonga mbele.
Bwana Paulson alisema, uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya Marekani na China unaendelea kwa kufuata njia sahihi, hili ni jambo la kubwa la muhimu kwa wananchi wa nchi hizo mbili na uchumi wa dunia. Marekani na China zinatakiwa kufanya mawasiliano mara kwa mara, kuondoa migongano, kudumisha maendeleo ya uwiano ya uhusiano wa kiuchumi, kujitahidi kutimiza lengo la kunufaishana na kuhimiza ongezeko la uchumi wa nchi hizo mbili na uchumi wa dunia.
|