Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-05-25 19:22:02    
Wachina barani Afrika

cri

Hivi sasa uhusiano kati ya China na Afrika unaendelezwa kwa kasi. Baada ya rais Hu Jintao wa China kufanya ziara barani Afrika mara mbili, na waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao kufanya ziara barani Afrika mwezi June mwaka jana, tarehe 15 mwezi Aprili mwaka huu, mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China Bw. Jia Qinglin aliondoka kutoka hapa Beijing na kufanya ziara nchini Tunisia, Ghana, Zimbabwe na Kenya. Kufanya ziara mara kwa mara barani Afrika kwa viongozi wa China, kunaonesha kuwa China na Afrika zina mawasiliano ya karibu katika sekta ya kisiasa.

Je, uhusiano huo unaoendelezwa kwa kasi unaonesha nini kwa watu wa kawaida? Takwimu husika zinaonesha kuwa, katika miaka sita au saba iliyopita, wachina wapatao laki 7.5 walikwenda barani Afrika kuishi na kufanya kazi huko. Sasa idadi hiyo bado inaongezeka. Sera ya serikali ya China kuhusu kuwekeza barani Afrika na ushirikiano kati ya China na Afrika unaoendelezwa siku hadi siku vimewahimiza wachina wengi zaidi waende barani Afrika.

Hivi sasa kila sehemu barani Afrikan kuna wachina, hata katika nchi za Afrika ambazo bado hazijaanzisha uhusiano wa kibalozi na China. Kati ya wachina hao, wako mabalozi, waandishi wa habari, wanafunzi, askari wa kulinda amani, watu wanaojitolea, wafanyabiashara, wataalamu wa ufundi, wafanyakazi wa ujenzi na mafuta. Shughuli zao zinahusika na sekta mbalimbali zikiwemo siasa, uchumi, utamaduni,elimu na teknolojia.

Kwa sababu ya kuongezeka kwa wachina waliokwenda barani Afrika, masoko mengi zaidi yanayouza bidhaa zilizotengenezwa na China yalianzishwa kwenye sehemu mbalimbali barani Afrika, ambapo imekuwepo mitaa ya wachina wanakoishi. Wachina hao wanatilia maanani kujiunga na jamii ya huko. Kampuni za China barani Afrika zinafanya juhudi ili kuzoea hali halisi ya huko, na wachina barani Afrika wanjifunza kwa hiari lugha za huko na kuelewa desturi za huko.

Wachina wote barani Afrika wana hisia maalumu kwa Afrika, na wanaona kuwa wanabeba jukumu la kulinda urafiki kati ya China na Afrika.

Mabalozi wa China katika nchi mbalimbali za Afrika wanatekeleza jukumu la kulinda urafiki kati ya China na Afrika. Balozi wa China nchini Afrika ya Kusini Bw. Liu Guijin alijiita kuwa ni "mkazi wa Afrika", yeye ni mtaalamu wa masuala ya Afrika, pia ni mtu aliyehimiza ushirikiano kati ya China na Afrika. Balozi wa China nchini Namibia Bw. Liang Yinzhu alishughulikia mambo ya kidiplomasia kwa miaka 36, aliwahi kufanya kazi katika nchi nyingi za Afrika. Ingawa atastaafu siku za mbele, lakini bado anafanya juhudi kwa ajili ya maendeleo ya uhusiano kati ya China na Namibia.

Ili kulinda amani na utulivu wa sehemu za Afrika, maofisa na askari wa China wanaolinda amani barani Afrika wanawajibika ipasavyo na jukumu lao, na kuchapa kazi bila kujali kutokwa na jasho jingi hata kujitolea mhanga. Afrika ni sehemu ambapo China ilituma maofisa na askari wengi kabisa wa kulinda amani, pia ni sehemu yenye hatari kubwa. maofisa na askari wa China wanaolinda amani barani Afrika walisifiwa na majeshi ya kulinda amani ya nchi za nje, kuwa "hawaogopi matatizo, hawaogopi kuchoka na hawaogopi hatari."

Wanamakampuni wa China barani Afrika, wana imani kwa mustakabali wa Afrika, na wanatilia maanani urafiki kati ya China na Afrika. Mwaka 2002, vita vya ndani nchini Angola vilivyodumu kwa miaka 27 vilikomeshwa, wakati ule msingi wa kilimo wa nchi hiyo ulipokuwa dhaifu sana, vyakula vingi zaidi vilitegemea kununuliwa kutoka nchi za nje. Mkurugenzi wa mradi wa kampuni ya ujenzi wa umeme na maji ya China nchini Angola Bw. Sun Yanhua aliona kuwa, mradi wa ushirikiano wa kilimo kati ya China na Angola bila shaka utabadilisha hali hiyo. Alisema kuwa ni muhimu sana kuwa na imani kwa nchi hiyo, huu ni msingi wa kufanya ushirikiano na kupanua ushirikiano. tukiwasaidia waangola kupata maji mashambani, kilimo cha Angola kitapata maendeleo ya haraka.

Wafanyakazi wa China wanaoshughulikia miradi mbalimbali barani Afrika walishinda matatizo mengi, na kutoa mchango mkubwa kwa kuendeleza na kuboresha ujenzi wa miundo mbinu wa huko. Katika sehemu ya Sahara, halijoto ya huko inafikia juzi joto 50?C, katika mazingira magumu kama hayo, wafanyakazi wa kampuni ya barabara na madaraja ya China bado wanashikilia kufanya kazi za ujenzi huo, hata wafanyakazi kadhaa walipoteza maisha ya ujana wao barani Afrika.

Bila shaka makampuni na wafanyabiashara wa China wanataka kupata faida katika shughuli zao barani Afrika, lakini wanaelewa na kufuata kanuni ya kimsingi, yaani kwa ajili ya kujipatia faida hawakuruhusiwi kuharibu maslahi ya nchi za Afrika. Serikali ya China itasimamia zaidi shughuli za makampuni na wafanyabiashara wa China barani Afrika, na kushughulikia vizuri uhusiano kati ya maslahi ya makampuni, taifa la China na nchi za Afrika. Kampuni yoyote au mtu yoyote, kama akitaka kujiendeleza kwa muda mrefu barani Afrika, anapaswa kutoa mchango kwa jamii ya huko.

Katika historia ya miaka zaidi ya elfu moja tangu China na Afrika zianzishe mawasiliano, hakuna vitendo vya unyang'a nyaji kati yao. Katika miaka zaidi ya mia moja iliyopita ambayo ni muda wa kupata uhuru na kujenga nchi ya kisasa, pia hakuna vitendo vya mashambulizi na ukoloni kati ya China na nchi za Afrika.

Katika wimbi la utandawazi wa uchumi duniani, China na Afrika zinaungana mkono, kushirikiana na kuzidisha ushirikiano wa kunufaishana kati yao siku hadi siku. Kila mchina anayeshiriki kwenye ushirikiano huo, anajenga maisha mazuri ya Afrika, na kueneza urafiki kati ya China na Afrika,.

Katika kipindi cha wiki zijazo, tutawaletea maelezo mengi zaidi kuhusa wachina barani Afrika.

Idhaa ya kiswahili 2007-05-25