Ingawa mpango wa Marekani wa kuongeza askari elfu 30 katika nchi ya Iraq bado haujatimizwa, lakini rais Bush na wasaidizi wake wameonesha kuwa, sasa wanaanza kufikiria sera mpya kuhusu Iraq, baada ya kumaliza kuongeza askari nchini humo, na umuhimu wa sera hizo ni kupunguza idadi ya askari wa Marekani nchini Iraq, endapo mapambano ya madhehebu ya kidini nchini Iraq, yatapata kudhibitiwa baada ya kuongezwa askani, tena itabadilisa jukumu muhimu la askari wa Marekani nchini Iraq, kuwa kushambulia kundi la al-Qaida na kutoa mafunzo kwa jeshi la Iraq.
Kwenye mkutano na waandishi habari uliofanyika tarehe 24 mwezi Mei, rais Bush alisema, anatarajia iko siku moja jeshi la Marekani, litaonekana kwa sura mpya nchini Iraq. Waziri wa ulinzi wa Marekani, Bw. Robert Gates, na mwenyekiti wa mkutano wa wakuu wa majeshi, Bw. Peter Pace, siku hiyo, pia walisema, baada ya amiri jeshi mkuu wa jeshi la Marekani nchini Iraq, Bw. David Petraeus, kutoa taarifa mwezi Septemba kuhusu ufanisi wa sera za kuongeza askari, viongozi wa jeshi la Marekani pia watajadili kuhusu sera mpya ya Iraq. Bw. Gates alisema, jukumu la jeshi la Marekani nchini Iraq, litabadilika kuwa "kutoa mafunzo ya kijeshi na kuzatiti jeshi la Iraq, kupambana na kundi la al-Qaida na kutoa uungaji mkono kwa jeshi la Iraq", ambapo "idadi ya askari inayohitajiwa katika utekelezaji wa sera mpya, itapungua kwa udhahiri, ikilinganishwa na idadi ya askari wa hivi sasa wa jeshi la Marekani nchini Iraq".
Habari zinazotolewa na Washington Post zinasema, balozi wa Marekani nchini Iraq Bw. Ryan Crocker na amiri jeshi mkuu wa jeshi la Marekani nchini Iraq Bw. David Petraeus hivi sasa wanashughulikia utungaji wa mpango huo mpya, ili kuisaidia Iraq kupunguza mapambano ya kisilaha kati ya madhehebu ya kidini. Habari zikikariri maneno ya ofisa wa Ikulu ya Marekani yanayosema kuwa, hivi sasa Ikulu ya Marekani imeanza kujadili kuhusu idadi ya askari wa marekani, watakaopelekwa nchini Iraq. Katika majadiliano hayo, yalitokea maoni ya aina mbili. moja kati yake ni kuwa, idadi ya askari wa jeshi la Marekani, isiongezeke tena, ifikapo mwishoni mwa mwaka 2008; na maoni ya aina nyingine yanasema, jeshi la Marekani litaanza kuondoka tokea mwanzoni mwa mwaka 2008, lakini uamuzi wa mwisho utaamuliwa na hali ya Iraq.
Vyombo vya habari vinasema, sababu ya Ikulu ya Marekani kuanza kubadilisha sera zake kuhusu Iraq, ni shinikizo linaloikabili bunge la taifa la Marekani, kuwa kubwa kadiri siku zinavyopita.
Hivi sasa chama cha democrat kinatunia wingi wa viti katika bunge la taifa, kinanuia kuendelea kuibana Ikulu ya Marekani kwa suala la sheria ya kutenga fedha. Kamati ya utengaji fedha kwa matumizi ya vita ya bunge la chini, inanuia kutenganisha matumizi ya vita ya Iraq na matumizi mengine ya ulinzi, na kutunga muswada wa sheria kuhusu utengaji fedha kwa matumizi ya vita ya Iraq, wakati watakapojadili bajeti ya ulinzi ya msimu wa mwaka 2008. Chama cha Democrat kinaona kuwa, njia hiyo itaweza kushindana bei na Ikulu ya Marekani kuhusu suala la Iraq katika hali ya kutoathiri matumizi mengine ya kijeshi ya Marekani.
Lakini hivi karibuni kamati ya kijeshi ya bunge la seneti ilitangaza muswada wa sheria kuhusu sera za ulinzi za Marekani. Mwenyekiti wa kamati hiyo aliyetoka chama cha Democrat Bw. Carl Levin alisema, wanachama wa chama cha Democrat watadai jeshi la Marekani lianze kuondoka Iraq ndani ya siku 120, baada ya muswada wa sheria kupitishwa. Alisisitiza, "wairaq hawatatambua kuwa mustakabali uko mikononi mwao, ila tu katika hali ya kulazimika". Mbali na hayo, bunge la seneti litabuni muswada wa sheria kuhusu vita vya Iraq katika mwezi ujao, ambao utaweka masharti kwa jeshi la Marekani kuendelea kuwepo nchini Iraq, kutokana na pendekezo la "kikundi cha utafiti kuhusu Iraq".
Licha ya wanachama wa chama cha democrat, baadhi ya viongozi wa chama cha Jamhuri walioko katika bunge la taifa, pia wanatarajia Ikulu, iweze kutoa sera mpya kuhusu Iraq, katika mwezi Septemba mwaka huu. Kiongozi wa wanachama wa chama cha Jamhuri katika bunge la seneti Bw. Mitch McConnell alisisitiza, tutaanzisha mwelekeo mpya tokea mwezi Septemba. Ninatumai rais, ataweza kuongoza mwelekeo huo".
Vyombo vya habari vinaona kuwa, endapo sera za kuongeza askari zikishindwa kudhibiti hali ya Iraq, basi jeshi la Marekani halina sababu ya kudumisha idadi ya askari ya hivi sasa. Kwa hiyo, jeshi la Marekani itawezekana kuondoka Iraq, mwakani bila kujali ya hali halisi ya Iraq.
|