Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-05-29 18:46:20    
China yaimarisha zaidi kupiga marufuku uvutaji wa sigara kwenye sehemu za umma

cri

Ofisa wa wizara ya afya ya China tarehe 29 hapa Beijing amesema, serikali ya China inafanya juhudi kutekeleza "Mkataba wa udhibiti wa tumbaku", na imeanza kurekebisha "Vifungu vya usimamizi wa hali ya afya ya sehemu za umma", baada ya marekebisho hayo, China itaimarisha zaidi kupiga marufuku uvutaji wa sigara kwenye sehemu za umma.

Kutumia mbinu za kisheria kwa kuimarisha kazi ya kupiga marufuku uvutaji wa sigara ni sehemu muhimu ya shughuli za kupiga marufuku uvutaji wa sigara nchini China. Naibu mkurugenzi wa ofisi ya kikundi cha uongozi wa kazi ya utekelezaji wa "Mkataba wa udhibiti wa tumbaku" Bibi Yang Gonghuan amesema:

Kutunga sheria ni hatua muhimu ya kupiga marufuku uvutaji wa sigara kwenye sehemu za umma. Tunaweza kuona kuwa, katika nchi mbalimbali duniani, sheria ya kupiga marufuku uvutaji wa sigara kwenye sehemu za umma ikitekelezwa, na wavutaji wa sigara kwenye sehemu za umma wamepungua kidhahiri.

Takwimu zilizokusanywa zimeonesha kuwa, idadi ya watu waliopata madhara kutokana na wavutaji wa sigara imefikia milioni 540, na kila mwaka idadi ya watu wanaokufa kwa sababu hiyo inazidi laki moja. Hivi sasa nchi za Ireland, New Zealand na Italia zilipitisha sheria kwa kuimarisha kazi ya kupiga marufuku uvutaji wa sigara kwenye sehemu za umma, na zimepata mafanikio mazuri.

Ingawa nchini China kuna sheria mbalimbali zinazohusu pia marufuku ya uvutaji wa sigara kwenye sehemu za umma, lakini hakuna sheria moja maalumu ya kupiga marufuku uvutaji wa sigara kwenye sehemu za umma, tena sheria zinazohusu pia jambo hili hazielezwi bayana, ambazo hazina nguvu kwa utekelezaji na kupata ufanisi. Uchunguzi uliofanyika umeonesha kuwa, kutunga sheria ya kupiga marufuku uvutaji wa sigara kwenye sehemu za umma, kumekuwa na maoni ya pamoja ya wananchi wa China, uchunguzi huo uliofanyika katika miji 7 ukiwemo Beijing umeonesha kuwa, karibu asilimia 50 ya wavutaji wa sigara wanaunga mkono pia, kupiga marufuku uvutaji wa sigara kwenye mikahawa au baa.

Naibu waziri wa afya wa China Bwana Wang Longde alisema, kutunga sheria kwa kuimarisha kazi ya kupiga marufuku uvutaji wa sigara, pia ni juhudi halisi za China katika kutekeleza "Mkataba wa udhibiti wa tumbaku", kufanya hivyo, pia kunaisaidia China kuanzisha kampeni ya "kuandaa Michezo ya Olimpiki katika mazingira yanayoondokana na uvutaji wa sigara" mwaka 2008, mjini Beijing. Bwana Wang alisema:

China ni nchi ya kwanza itakayoandaa Michezo ya Olimpiki baada ya "Mkataba wa udhibiti wa tumbaku" kuanza kufanya kazi. Wizara ya afya ya China inatoa mwito wa kuitaka miji mbalimbali inayoandaa Michezo ya Olimpiki itoe mpango wa utekelezaji kuhusu "kuandaa Michezo ya Olimpiki katika mazingira yanayoondokana na uvutaji wa sigara", na kutekeleza mpango kwa hatua halisi. Kwa kupitia kampeni kama hiyo kutahimiza kazi ya kujenga mazingira ya umma yanayoondokana na uvutaji wa sigara na mazingira safi ya kufanya kazi.

Habari zinasema kuwa, wakati wa Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008 mjini Beijing, China itatekeleza sera ya kupiga marufuku kwenye viwanja na majumba yote ya michezo, na kupiga marufuku matangazo yote yanayohusika na tumbaku. Aidha, Beijing inatazamiwa kuanzisha kampeni ya kudhibiti uvutaji wa sigara kwenye mikahawa na mahoteli, ambapo mahoteli yaliyotia saini makubaliano husika na Michezo ya Olimpiki, viwanda na majumba ya Michezo ya Olimpiki pamoja na mikahawa kwenye Kijiji cha Michezo ya Olimpiki, vyote hivyo vitapiga marufuku uvutaji wa sigara, kabla ya mwezi Juni mwaka 2008.

Ofisa wa Shirika la afya duniani anayeshughulikia miradi ya ngazi ya juu Bwana Cris Tunon alisema, Shirika la afya duniani litaiunga mkono China kuandaa Michezo ya Olimpiki kwenye mazingira yanayoondokana na uvutaji wa sigara. Alisema:

China imeahidi kuandaa Michezo ya Olimpiki kwenye mazingira yanayoondokana na uvutaji wa sigara. Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008, itakayofanyika mjini Beijing, itakuwa fursa ambayo ni nadra kupatikana katika miaka mingi kwa China, ili kuimarisha kazi ya kudhibiti uvutaji wa sigara. Shirika la afya duniani litatoa msaada kwa China katika kazi yake hiyo.