Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-05-30 16:04:35    
Mapishi ya bilinganya

cri

Mahitaji

Bilinganya gramu 150, paja la ash la nguruwe gramu 50, pilipili mboga moja, pilipili hoho moja, chumvi gramu 10, sukari gramu 2, mchuzi wa sosi gramu 5, sosi ya chaza gramu 5, chembechembe za kukoleza ladha gramu 8, tangawizi gramu 5, maji ya wanga gramu 10, mafuta ya ufuta gramu 2.

Njia

1. kata paja la ash la nguruwe liwe vipande vipande, ondoa gamba la bilinganya halafu uikate iwe vipande, kata pilipili mboga na pilipili hoho ziwe vipande, kata tangawizi iwe vipande.

2. washa moto halafu tia mafuta kwenye sufuria, tia vipande vya tangawizi, pilipili mboga na pilipili hoho, chumvi, korogakoroga, halafu tia vipande vya paja la ash la nguruwe.

3. tia bilinganya, chembechembe za kukoleza ladha, sosi ya chaza, mchuzi wa sosi, korogakoroga, mimina maji ya wanga, mimina mafuta ya ufuta, korogakoroga. Ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.