Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-05-30 16:21:48    
Tiba na dawa za kitibet zinazotumia sayansi na teknolojia ya hali ya juu

cri

Kutokana na maendeleo ya kasi ya sayansi na teknolojia ya kisasa, kati ya mifumo minne ya matibabu ya jadi yaliyowahi kuleta athari kubwa kwa binadamu duniani, yaani matibabu ya jadi ya kichina, matibabu ya kitibet, matibabu ya kale ya India na matibabu ya kale ya kiarabu, ni matibabu ya jadi ya kichina na ya kitibet tu ambayo yamehifadhiwa kikamilifu hadi leo, na kupata maendeleo na uvumbuzi bila kusita, matibabu hayo yametoa mchango mkubwa katika kuwasaidia binadamu kupambana na magonjwa na kujenga mwili.

Chuo kikuu cha matibabu cha Tibet kiko karibu na sehemu ya hifadhi ya kimaumbile ya ardhi oevu ya Lalu mjini Lahsa. Naibu mkuu wa chuo kikuu hicho Bwana Chilai Wanjie alisema:

"Tiba na dawa za kitibet ni sehemu moja muhimu ya utamaduni wa kabila la watibet, ambao umeiga mambo mengi kutoka kwa matibabu ya jadi ya kichina na matibabu ya kale ya India, na kuunda mfumo wake pekee kutokana na hali yake maalum ya kuwepo kwenye uwanda wa juu wa Tibet, matibabu ya kitibet yana historia ya miaka 2800."

Bwana Chilai Wanjie alisema katika zama hii ambapo matibabu ya kisasa yanaendelea kwa haraka sana, wakazi wa kabila la watibet bado wanaamini tiba ya kitibet kutokana na mfumo wake kamili na wa kipekee wa kubainisha ugonjwa na kutibu, mitishamba yote ya dawa za kitibet haina vitu vyenye uchafuzi.

"Ili kuendeleza tiba na dawa za kitibet, serikali ya China imetoa sera zinazotoa kipaumbele katika kuokoa na kuendeleza utamaduni wa tiba na dawa za kitibet, kuidhinisha kwa umaalum na kuanzisha chuo kikuu cha matibabu ya kitibet zaidi ya miaka 10 iliyopita."

Hivi sasa, chuo kikuu cha matibabu ya kitibet ni chuo kikuu kidogo kabisa nchini China, kina wanafunzi zaidi ya 700 na walimu na wafanyakazi 140 hivi, kina kozi mbili za matibabu ya kitibet na dawa za kitibet, na kinaweza kuwaandaa wanafunzi wa shahada ya pili. Hadi leo chuo kikuu hicho kimewaandaa madaktari elfu kadhaa kwa mikoa ya Tibet, Qinghai, Gangsu na Sichuan.

Zaidi ya hayo, chuo kikuu cha tiba ya kitibet pia kimeanzisha kituo cha utafiti wa dawa za kitibet na kiwanda cha kutengeneza dawa za kitibet, ambacho kinaweza kutengeneza aina 24 za dawa zenye ufanisi maalum wa kutibu magonjwa maalum kama vile ugonjwa wa kisukari, na homa ya maini aina ya B, na dawa nyingine zaidi ya 200 za kawaida. Pia kimefanya mawasiliano na vituo vya utafiti na vyuo vikuu vya matibabu vya nchini na nchi za nje na sifa yake inainuliwa siku hadi siku duniani.

Katika hospitali ya Tibet, waandishi wetu wa habari walimkuta mgonjwa anayeitwa Langjie Chiren aliyekuwa na tatizo la shinikizo la damu, na mkuu wa hospitali hiyo Bwana Gesan Pingcuo. Mgonjwa Chiren alipofika hospitali, alikuwa na kizunguzungu na alikuwa anashindwa kupumua vizuri, mgongo wake ulikuwa una maumivu makali, hata alishindwa kutembea peke yake. Alisema baada ya kupewa tiba ya kitibet kwa wiki tatu, shinikizo lake la damu lilishuka na kutulia. Alisema:

"Mkuu wa Hospitali hiyo Bwana Gesan anakagua wadi kila siku, na kila akiwa na wakati huzunguka na kuuliza hali ya maendeleo ya wagonjwa. Usimamizi wa hospitali hiyo na ustadi wa madaktari wa kuwatibu wagonjwa ni mzuri, unaniridhisha sana."

Matibabu ya dawa za kitibet aliyopewa Bw. Chiren yameonesha teknolojia maalum ya matibabu ya kitibet, yaani daktari wa kitibet si kama tu anatakiwa kuwa na uwezo wa kubainisha ugonjwa na kutoa tiba kwa wagonjwa, bali pia anatakiwa kutambua na kutengeneza dawa za kitibet. Baada ya maendeleo ya miaka 1000, utengenezaji wa jadi wa dawa za kitibet umeacha njia ya kutumia mikono, sasa dawa zainatengenezwa kwenye kiwanda cha kisasa. Kiwanda cha dawa za kitibet cha Qizheng cha Linzhi mkoani Tibet ni maarufu sana katika kutengeneza dawa za kitibet. Mwaka 2001 kilipata cheti cha GMP, yaani kuthibitishwa na idara ya upimaji wa dawa duniani. Mkuu wa kiwanda hicho Bwana Cairang Zhaxi alisema, njia sahihi ya kuendeleza dawa za kitibet za jadi ni kutumia teknolojia ya hali ya juu ya kisasa na kujiingiza katika soko huria. Alisema:

"Kupata mafanikio kwa dawa za chapa ya Qizheng kunategemea kuunganishwa kwa dawa za jadi za kitibet na mbinu ya utengenezaji wa kisayansi."

Bw. Cairang alisema dawa za jadi za kitibet hutengenezwa kuwa vidonge, ambayo ina dosari kadhaa ambazo zinaathiri ufanisi wake. Sasa wametumia teknolojia ya kisasa na kuongeza ufanisi wake ipasavyo. Kwenye karakana ya kufunga dawa ya kiwanda cha dawa za kitibet cha Qizheng, waandishi wetu wa habari wameona aina tofauti za dawa kama vile dawa za vidonge, unga, kuchua na za kubandika. Dawa hizo zote zilitengenezwa na kufungwa kwa mitambo, mchakato wake unafanana na uzalishaji wa dawa za magharibi.

Idhaa ya kiswahili 2007-05-30