Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-05-31 21:02:58    
Baraza la usalama lapitisha azimio la kuunda mahakama ya kimataifa kuhusu mauaji ya Rafik Hariri

cri

Tarehe 30 mwezi Mei, baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio No. 1757 kwa kura 10 za ndiyo, ambapo kura 5 hazikupigwa, likiamua kuunda mahakama maalumu ya kimatiafa kushughulikia kesi ya mauaji ya Rafik Hariri aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon. Kuhusu suala hilo, baadhi ya nchi zimekuwa na wasiwasi kuwa, azimio hilo limekiuka mchakato wa utungaji wa sheria wa Lebanon, na huenda litaweka mfano wa baraza la usalama kuingilia kati mambo ya ndani ya nchi moja yenye mamlaka.

Muswada wa azimio hilo ulitolewa na nchi za Marekani, Uingereza na Ufaransa unaona tukio la mauaji ya Hariri ni kitendo cha ugaidi, ambao unatishia amani na usalama wa kimataifa, na unataka bunge la Lebanon kuidhinisha kabla ya tarehe 10 mwezi Juni mwaka huu makubaliano yaliyofikiwa na Umoja wa Mataifa na serikali ya Lebanon kuhusu kuunda mahakama maalumu, iwapo haitachukua hatua hadi ifikapo siku hiyo, makubaliano hayo yataanza kufanya kazi, na baraza la usalama litachukua hatua kutokana na ibara ya 7 ya Katiba ya Umoja wa Mataifa kulilazimisha kutekeleza mapatano yatakayoweza kuunda mahakama chini ya mwendesha mashitaka na majaji wa kimataifa. Azimio hilo pia linataka katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon kushauriana na serikali ya Lebanon kuchukua hatua haraka iwezekanavyo na kuunda mahakama maalumu, tena na kutolewa taarifa ndani siku 90 na kila baada ya muda maalumu hapo baadaye kuhusu maendeleo yake.

Tarehe 14 mwezi Februari mwaka 2005, Bw. Hariri na msafara wake wenye watu 22 kwa jumla waliuawa na shambulio la mabomu yaliyotengwa ndani ya gari. Uchunguzi wa mwanzo wa kamati huru ya uchunguzi iliyokabidhiwa mamlaka na Umoja wa Mataifa unasema, maofisa wa ngazi ya juu wa Lebanon na Syria walituhumiwa na tukio hilo, lakini Syria imekataa kuhusu jambo hilo. Mwezi Desemba mwaka huo, baraza la usalama lilipitisha azimio likitaka kuunda mahakama maalumu ya kimataifa kusikiliza kesi hiyo. Hapo baadaye, Umoja wa Mataifa na serikali ya Lebanon zilifikia mapatano kuhusu suala hilo, isipokuwa mapatano yataweza kufanya kazi baada ya kuidhinishwa na bunge la Lebanon. Makundi mbalimbali ya nchini Lebanon yana misimamo tofauti kuhusu uundaji wa mahakama ya kimataifa, hivyo hadi sasa bunge la Lebanon bado halijaidhinisha mapatano hayo. Kundi la wabunge walio wengi katika bunge la Lebanon liliutumia barua Umoja wa Mataifa likitaka baraza la usalama kuidhinisha kuunda mahakama ya kimataifa. Waziri mkuu wa Lebanon Bw. Foud Siniora naye pia alimtumia barua katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ikisema, mchakato kuhusu kuunda mahakama maalumu nchini Lebanon umekwama, na kutaka baraza la usalama lifanye uamuzi wenye nguvu ya kulazimisha. Lakini rais Emile Lahoud alipinga, akionya kuwa, kuunda mahakama hiyo kutaleta vurugu nchini Lebanon.

Kikanuni, kupitishwa kwa azimio la baraza la usalama kunahitaji kura tisa kwa uchache kabisa kati ya kura 15 za wanachama wake, tena bila kupingwa na nchi yoyote moja ya mjumbe wa kudumu wa baraza hilo. Azimio hilo lilipitishwa kwa wingi mdogo wa kura, hii inaonesha kuwa kulikuwa na nchi nyingi, ambazo zina wasiwasi kuhusu mafanikio ya azimio hilo. Nchi tano za Russia, China, Qatar, Indonesia na Afrika ya kusini hazikupiga kura kuhusu suala hilo kwa kuhofia azimio hilo huenda litaweza kuleta matokeo mabaya ya kisheria na kisiasa. Mjumbe wa kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa Bw. Vitaly Churkin alisema, Russia haipingi kuunda mahakama maalumu, ila tu kuwa na maoni tofauti kuhusu jinsi ya kuunda mahakama maalumu na kwa mchakato wa aina gani. Kuilazimisha Lebanon kuchukua hatua kwa azimio la baraza la usalama, ni sawa na kutenda vitendo badala ya bunge la nchi moja, jambo ambalo litaleta matokeo mabaya ya kisheria na kisiasa.

Mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Matiafa Bw. Wang Guangya alitoa tamkokabla ya upigaji kura huo, akisema, jambo la kuunda mahakama maalumu ni la Lebanon yenyewe, na msingi wake ni sheria ya nchi ya Lebanon. Hivyo linatakiwa kufuata mchakato wa katiba na sheria ya nchi hiyo.