Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-06-05 18:59:48    
Ujenzi wa miji yenye eneo kubwa misitu wapata maendeleo

cri

Katika hali ya kawaida, misitu iko kwenye sehemu za milimani ambazo ziko mbali na miji, ambayo ni nadra inaonekana mijini. Lakini katika miaka ya hivi karibuni, upandaji wa miti mijini unavuma sana katika miji mingi nchini China ili kuboresha mazingira ya kuishi. Watu husika walisema mwelekeo huo utasaidia maendeleo endelevu ya miji, na kuzalisha kuleta mali nyingi za viumbe.

Katika mwezi uliopita, mkutano wa nne wa baraza la misitu mijini ulifanyika mjini Chengdu, mkoani Sichuan. Kwenye mkutano huo, miji minne ikiwemo mji wa Chengdu ilipewa sifa ya "mji wa misitu wa kitaifa". Mpaka sasa miji saba imepata sifa hiyo, na imekuwa mifano ya kuigwa katika kujenga miji yenye eneo kubwa la misitu. Kwenye mkutano huo ofisa anayeshughulikia mradi wa kiwango cha juu wa sekretarieti wa baraza la misitu la Umoja wa Mataifa Bw. Mahendra Joshi alizisifu kazi za upandaji wa miti nchini China. Alisema:

"Ninajua kuwa serikali za miji mbalimbali na serikali kuu ya China zimefanya juhudi kubwa kwa kuongeza maeneo yanayofunikwa na miti nchini."

Kutokana na maneno yake, tunaweza kujua mafanikio makubwa ya mji wa Chengdu katika kuongeza eneo linalofunikwa na miti mjini humo.

Habari zinasema mji wa Chengdu siku zote unafanya juhudi kuboresha na kuhifadhi mazingira. Katika miaka 20 iliyopita, eneo linalofunikwa na miti mjini liliongezeka kuwa asilimia 36 kutoka asilimia 23. Ongezeko hilo ni kubwa zaidi kuliko miji mikuu mingine ya mikoa nchini China. Miti hiyo inawapatia wakazi wa mji huo matunda mengi, kusaidia mavuno ya nafaka na mboga kuongezeka kwa asilimia 15, na kupunguza matumizi ya nishati kwa asilimia 10 hadi 15.

Miji mingi ya China inapenda kupewa sifa ya "mji wa misitu wa kitaifa" kama mji wa Chengdu. Kwa ujumla mameya au wajumbe kutoka miji 14 wamehudhuria mkutano huo, na wanafuatilia sana upandaji wa miti mijini. Meya wa mji wa Lhasa wa mkoa unaojiendesha wa Tibet Bw. Duojicizhu alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, lengo lao la kuhudhuria mkutano huo ni kujifunza kutoka kwa uzoefu wa mji wa Chengdu, na kuongeza eneo linalofunikwa na miti na kuboresha mazingira ya kuishi mjini Lhasa. Alisema,

"Mji wa Lhasa ukiwa mji muhimu wa kulinda usalama wa viumbe nchini China, unafanya juhudi kujenga mji mwenye mtindo wa kipekee wa kikabila kwenye uwanda wa juu. Baada ya kujifunza uzoefu wa mji wa Chengdu, tutaweka msingi imara kwa kupewa sifa ya "mji wa misitu wa kitaifa". Tutaufanya mji wa Lhasa uwe na mazingira mazuri zaidi."

Bw. Li Zhijian kutoka idara ya misitu ya mji wa Xiamen ulioko mashariki ya China alisema, wakati ujenzi wa miji unapata maendeleo ya haraka na upungufu wa ardhi umekuwa mkubwa zaidi nchini China, mji wa Chengdu bado unatumia eneo kubwa la ardhi nyingi kwa kuboresha mazingira ya viumbe, huu ni mfano wa kuigwa kwa mji wa Xiamen.

Bw. Li alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, katika miaka ya karibuni, makampuni makubwa maarufu duniani yalijenga makao makuu yao mjini Xiamen. Jambo hilo limeupatia mji huo fursa nyingi za maendeleo ya uchumi. Alisema licha ya mji wa Xiamen kuwepo kwenye pwani, mazingira mazuri ya kuishi ya mji huo pia ni sababu kubwa kwa makampuni hayo kujenga makao makuu yao mjini humo.

"Sababu ya kwanza ni kuwa mji wa Xiamen uko kwenye sehemu nzuri nchini China, na mazingira mazuri ya mji huo pia ni sababu moja. Makampuni kadhaa ya nchi za nje yakiwemo makampuni ya Dell na Kodak yameanzisha matawi yao mjini Xiamen katika miaka ya hivi karibuni, na yametoa mchango mkubwa kwa ongezeko la thamani ya uzalishaji ya mji huo. Kwa mfano thamani ya uzalishaji ya kampuni ya Dell ni yuan bilioni kumi kadhaa kwa mwaka."

Wataalamu walisema, licha ya ufanisi wa uboreshaji wa mazingira ya viumbe, ufanisi wa kiuchumi kutokana na upandaji wa miti mijini pia ni mkubwa wa kidhahiri, kwa sababu upandaji wa miti unaweza kuboresha mazingira ya kuishi, halafu kuwavutia wawekezaji na wataalamu, na kusukuma mbele maendeleo endelevu ya miji. Meya wa mji wa Chengdu Bw. Ge Hongling anaona kuwa, upandaji wa miti mjini Chengdu umesukuma mbele maendeleo ya uchumi wa mji huo. Bw. Ge alisema,

"Mji wa Chengdu uko magharibi mwa China, zamani wawekezaji wengi kutoka nje pamoja na watu wa makampuni makubwa duniani waliona kuwa uchumi wa mji wa Chengdu wa sehemu hiyo uko nyuma kimaendeleo. Na waliposikia mji huo uko kwenye sehemu ya magharibi, walikuwa hupata taswira kuhusu upepo wa mchanga unaovuma, walidhani mjini humo hakuna miti milimani, na maji ya mito pia si safi, lakini walipokuja Chengdu, waligundua hali halisi ni tofauti kabisa. Mji wa Chengdu ni moja ya miji yenye mazingira mazuri zaidi nchini China."

Kama Bw. Ge alivyosema, mazingira ya mji wa Chengdu ni mazuri, ambayo yanafaa kwa ukuaji wa mimea mbalimbali. Mtaalamu wa taasisi ya sayansi ya misitu ya China Prof. Peng Zhenhua alisema mazingira ya mji wa Chengdu yanafaa sana kwa ukuaji wa miti. Lakini pia alisema umaalumu wa miji mbalimbali ni tofauti, hivyo ni lazima kutunga mipango tofauti ya kupanda miti mijini.

Ofisa wa ofisi ya hifadhi ya misitu ya shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa Bibi. Michelle Gauthier pia anaona kuwa, kupanda miti mijini ni jambo zuri, lakini ni lazima kupanda miti kwa mujibu wa hali halisi ya miji mbalimbali. Alisema.

"Kutokana na hali tofauti, miji mbalimbali zinaweza kutafuta utatuzi unaoendana na hali zao, ili kuhakikisha mitindo tofauti ya miji."

Mwishoni wajumbe waliohudhuria mkutano huo walipitisha azimio likisema kuwa, China itachukua hatua kadhaa zikiwemo kutunga mpango, kupanda miti na kufanya usimamizi kwa mujibu wa sayansi na kanuni husika ili kusukuma mbele upandaji wa miti katika miji. Tunaamni kuwa upandaji wa miti mijini utaendelea kuvuma nchini China.