Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-06-06 20:29:38    
Mapishi ya matango na kamba-mwakaje

cri

Mahitaji

Matango gramu 100, kamba-mwakaje gramu 300, pilipili hoho gramu 5, tangawizi gramu 5, vitunguu saumu gramu5, chumvi gramu 5, chembechembe za kukoleza ladha gramu 2, maji ya wanga gramu 5.

Njia

1. ondoa magamba ya matango halafu katakata liwe vipande vidogo vidogo. Osha kamba-mwakaje, na ondoa gamba lake.

2. washa moto, mimina maji kwenye sufuria, baada ya kuchemka, tia kamba-mwakaje kwenye maji korogakoroga halafu pakua.

3. Washa moto tena, tia mafuta kwenye sufuria, tia vipande vya tangawizi, vitunguu saumu na pilipili hoho, halafu korogakoroga, baada ya hapo tia vipande vya matango na kamba-mwakaje, na korogakoroga, halafu tia chumvi, chembechembe za kukoleza ladha, korogakoroga, na kisha mimina maji ya wanga, na korogakoroga na halafu pakua. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.