Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-06-07 19:17:45    
Wataalamu wa kigeni wanaofanya kazi nchini China

cri

Leo katika kipindi chetu cha Tazama China, tunawaletea maelezo kuhudu wataalamu wa kigeni wanaofanya kazi nchini China. Katika miaka ya hivi karibuni kutokana na China kufungua mlango zaidi kwa nje kwenye sekta mbalimbali, mahitaji ya China kwa wataalamu wa nchi za nje pia yanaongezaka siku hadi siku. Hivi sasa wataalamu zaidi ya 20,000 kutoka ng'ambo wanafanya kazi katika sekta mbalimbali nchini China, ambao wanatoa mchango mkubwa kwa ujenzi na maendeleo ya China, idara husika za China pia zinawapatia huduma bora na kuwafurahisha katika mazingira ya kuishi na kufanya kazi.

"familia yangu inaishi kwa furaha hapa Beijing, watoto wangu wanasoma hapa kwa furaha, pia ninashirikiana vizuri na wenzangu kwenye kazi yangu. Tumeichukua China, na Beijing kuwa maskani yetu ya pili."

Aliyosema hayo ni mtaalamu anayeitwa Abbas Jawad Kdaimy kutoka Iraq. Naye anafanya kazi kwenye chombo kimoja cha habari na anaelekeza kazi ya tafsiri ya kiarabu kwa kichina. Yeye ameishi nchini China kwa miaka minane na anaupenda sana mji wa Beijing. Alitueleza kuwa anaipenda China, na anaipenda Beijing, hivyo aliileta familia yake nchini China.

Hivi sasa wataalamu zaidi ya 20,000 wa kigeni kama Bw. Abbas wanafanya kazi katika sekta za kilimo, viwanda, uchumi, tekenolojia ya Intenet, elimu, vituo vya telivisheni na radio nchini China. Walikuja China kutokana na mahitaji ya kazi, kupenda lugha ya Kichina, hasa kuwa wadadisi na kutamani kuufahamu utamaduni wa China. Lakini sababu kubwa ni kuwa wanaona China ni nchi yenye fursa nyingi za kujiendeleza. Bw. Paul Dixon aliyekuja China mwaka jana kutoka Uingereza, alisema:

" Umuhimu wa China unaonekana kidhahiri siku hadi siku, kabla ya kuja China nilifundishwa kuwa ninapaswa kuelewa umuhimu wa China, kwa sababu karne ya 21 ni karne ya China. Hivyo kuna fursa nyingi nchini China. Kila mwaka wageni wengi wanakuja China kufanya biashara, kutalii au kusoma, wanafurahi sana kuja China.

Bw. Dixon anafanya kazi katika kampuni ya uhusiano, alitueleza kuwa ili aishi na kufanya kazi vizuri nchini China, alijifunza kichina kwenye chuo kikuu baada ya kuwasili China. Alishangazwa kuwa kwenye vyuo vikuu vya China karibu kila mtu anaweza kuongea lugha ya Kingereza. Bw. Dixson anaona kuwa kila mtu anahitaji muda kwa kuzoea mazingira baada ya kuishi kwenye sehemu ya kigeni, lakini baada ya kuja China, muda wake wa kuzoea mazingira ni mfupi zaidi kuliko makadirio yake. Anaona lugha haikuwa kikwazo cha mawasiliano kati yake na watu wengine, sasa amezoea maisha nchini China.

Bw. Mitchell Cooper anayetoka Marekani anafundisha lugha ya Kingereza kwenye chuo kikuu cha tekenolojia cha Beijing, anfurahia sana kazi yake. Alisema,

"ninaifurahia sana kazi yangu na ninapenda kufundisha kwenye chuo kikuu hiki. Mimi na wanafunzi wangu tunakuwa na furaha sana kwenye darasa langu, labda kwa sababu ya kuwa mimi ninaweza kutumia sura na ishara ya mikono ili kulifanya darasa langu kuwa na furaha. Kwa mfano katika darasa moja, nilipojitambulisha nilisema mimi naitwa Cooper, nitakuwa mwalimu wenu, mnaweza kuniita Bw. Cooper, au Cooper au mtu mwenye sura nzuri. Wanafunzi wangu walicheka sana."

Inaonekana kuwa Bw. Cooper anafurahia kufundisha kwenye chuo kikuu hicho. Ameishi nchini China kwa miaka mitatu, alitueleza kuwa anataka kuishi nchini China kwa muda mrefu pamoja na wanafunzi wake. Alisema maendeleo ya uchumi wa China yanawaletea fursa nyingi zaidi za kupata ajira, pia yanaweza kuyafanya makampuni ya China yaweze kuwalipa mishahara mizuru. Sasa makampuni makubwa, vyuo vikuu kadhaa vya China na idara nyingine zinaweza kutoa mishahara zaidi ya kiwango cha nchi za ng'ambo.

Kuboresha huduma siku hadi siku kwa wataalamu wa kigeni nchini China pia ni sababu moja inayowavutia kuja nchini China. Idara ya wataalamu wa kigeni ya China kila mwaka inafanya maonesho kuhusu kutafuta kazi na mkutano wa mawasiliano ya wageni hodari ya kimataifa, kutoa urahisi kwa wataalamu wa kigeni kutafuta kazi nchini China; idara ya wataalamu wa kigeni ilianzisha tovuti ili kutangaza habari za ajira katika miji mikubwa ya China. Pia idara hiyo ilifanya juhudi kutoa urahisi mbalimbali kwa wataalamu wa kigeni, pamoja na kutoa huduma maalum. Kwa mfano kutoa bima ya matibabu kwa wataalamu wageni na wanaweza kuchagua hospitali wanaoiamini ili kupata matibabu. Hospitali hizo zina uwezo wa matibabu yanayohusiana na wageni, madaktari na wauguzi wanaweza kuwasiliana na wageni hao kwa lugha za kigeni.

Shirika la maingiliano ya wataalamu duniani la China ni jumuia moja ya idara ya wataalamu wa kigeni ya China inayoshughulikia maingiliano na wageni wenye ujuzi. Bw. Xiabing wa shirika hilo alisema katika kazi za kawaida, yeye na wenzake wameona wataalamu wengi wa kigeni wanaotaka kuja China kufanya kazi. Wataalamu wengi wanasema wanataka kuja China kufanya kazi kutokana na kuwa China ina fursa nyingi za ajira, mazingira mazuri ya kijamii, utaratibu bora wa huduma na wananchi wake wana urafiki mkubwa. Bw. Xiabing alisema,

"wataalamu wa kigeni wanaoishi na kufanya kazi katika nchi za nje wanataka kubadilisha mazingira ya maisha, China ni nchi ya kwanza wanayochagua, kwa sababu hapa ni salama zaidi na kuna utulivu, na pia kuna fursa nyingi ya kujiendeleza."

Ili kuwashukuru wataalamu hao wa kigeni waliotoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya China, serikali ya China ilianza kufanya shughuli za kuwapongeza kuanzia miaka 50 karne iliyopita. Hasa kuanzia miaka ya 90 ya karne iliyopita, kila mwaka China inatoa tuzo ya urafiki ya Jamhuri ya watu wa China kwa wataalamu 50 wa kigeni, ili kuwashukuru kutokana mchango waliotoa nchini China. Bw. Abbas alisema tuzo hiyo inamaanisha sifa kubwa kabisa kwa wataalamu hao wa kigeni. Alisema: "

"nina rafiki mmoja aliyewahi kupewa tuzo hiyo, mimi pia nina matumaini makubwa ya kupewa tuzo hiyo, kwa sababu tuzo hiyo ni fahari kubwa kwa mtu anayeipewa. Ninafanya juhudi ili kupewa tuzo hiyo kwa sababu ina umuhimu mkubwa kwangu. Hasa kwa sababu tuzo hiyo ilitolewa na serikali ya China na wachina, kila mtu anayepewa tuzo hiyo anaona fahari kubwa."

Hivi sasa China inaendelea kuboresha hatua za kuingiza wataalamu wa kigeni na kuinua kiwango cha kutoa huduma kwa wataalamu hao na kufanya juhudi kuwapatia wataalamu hao mazingira mazuri ya kazi na maisha.