Wakuu wa nchi wa kundi la nchi nane walishiriki kwenye karamu iliyoandaliwa tarehe 6 mwezi Juni usiku kwenye mji mdogo wa Heiligendamm ulioko katika pwani ya mashariki ya Ujerumani kwa ajili ya kufungua rasmi mkutano wa kilele wa kundi la nchi nane mwaka huu. Tokea tarehe 7, viongozi hao wa nchi nane watakuwa na majadiliano ya siku 2 kuhusu hifadhi ya hali ya hewa, usalama wa nishati, misaada kwa ajili ya Afrika na nchi maskini, biashara huria na uwekezaji, hifadhi ya hakimiliki ya ubunifu na usalama wa dunia. Vyombo vya habari vinaona masuala hayo manne kati ya masuala mengi ni muhimu katika mkutano wa kilele mwaka huu.
kwanza, ni suala la ongezeko la joto duniani. Ikiwa ni nchi mwenyekiti wa mkutano wa kilele wa kundi la nchi nane, Ujerumani imekuwa ikijitahidi kupitisha lengo la upunguzaji halisi wa utoaji vitu vinavyoongeza joto la dunia wenye nguvu ya ulazimishaji ndani ya Umoja wa Mataifa. Lengo la Ujerumani ni kuwa, utoaji gesi ya kuongeza joto la dunia ifikapo mwaka 2050 upungue kwa 50% kuliko kiwango cha mwaka 1990, lakini Marekani inapinga siku zote kuweka kiwango cha utoaji gesi. Kabla ya kufanyika kwa mkutano wa kilele, rais Bush wa Marekani alitangaza mkakati wa muda mrefu wa kukabili suala la ongezeko la joto la dunia. Lakini rais Bush bado anasisitiza kuwa, uwiano wa utoaji gesi wa nchi mbalimbali ungeamuliwa na kila nchi yenyewe, ingawa katika mazungumzo kati yake na Chansela Angela Merkel yaliyofanyika tarehe 6 Juni kabla ya kufanyika kwa mkutano wa kilele, alisema, moja ya malengo muhimu ya safari yake hiyo ni kutafuta jawabu la kujenga mfumo baada ya kupitishwa kwa "Mapatano ya kyoto". wachambuzi wanaona, tofauti ya misimamo kati ya Ulaya na Marekani italeta mgongano kwenye mkutano huo wa kilele kuhusu suala hilo.
pili, ni kuhusu suala la kutoa misaada kwa ajili ya Afrika. Suala la kutoa misaada kwa ajili ya Afrika limekuwa mada muhimu kwa mara ya tatu kwenye mkutano wa kilele wa kundi la nchi nane baada ya mkutano uliofanyika mwaka 1999 huko Cologne na mkutano uliofanyika mwaka 2005 huko Gleneagles, Scotland. Hali ya hivi sasa ni kuwa, mkutano wa kilele wa Gleneagles wa mwaka 2005 uliahidi kuongeza fedha za misaada ya maendeleo ya dola za kimarekani bilioni 50 kwa mwaka kabla ya mwaka 2010, lakini fedha za misaada zilizotolewa ni 10% tu ya zile zilizoahidiwa kutolewa. Baadhi ya vyombo vya habari vinasema, ingawa mkutano wa Heiligendamm wa mwaka huu umeweka mkazo katika suala la kutoa misaada kwa ajili ya Afrika, lakini nchi za magharibi zinashikilia nchi zinazopewa misaada zinapaswa kufanya mageuzi ya utawala adilifu kwa kufuata mtazamo wa thamani yao, ambayo yanachukuliwa na nchi zinazopewa misaada kuwa ni uingiliaji kati katika mambo yao ya ndani. Hivyo huenda hakutakuwa na maendeleo yoyote kuhusu suala hilo.
tatu, ni suala la nishati, baada ya mkutano wa kilele wa Sankt Petersburg, mkutano wa kilele wa Heiligendamm wa mwaka huu umelichukua suala la nishati kuwa mada muhimu. Mgogoro wa gesi ya asili kati ya Russia na Ukraine na mgongano kati ya Russia na Belarus uliotokea mwanzoni mwa mwaka uliopita, imeufanya Ulaya kuchunguza sera zake kuhusu nishati ili kuhakikisha usalama wa nishati. Hivyo kutafuta sera za namna moja na tulivu kuhusu nishati na utoshelezaji wa nishati kutoka maeneo mengine ni suala nyeti linalofuatiliwa na Ulaya kwenye mkutano huo wa kilele. Ili kupunguza hali ya kutegemea sana mali-ghafi za nje na kutumia nishati endelevu, Umoja wa Ulaya unazingatia ufanisi wa matumizi ya nishati na kuinua kiwango cha matumizi ya nishati endelevu.
nne, ni ongezeko la uchumi duniani. Ikiwa nchi mwenyekiti wa sasa wa mkutano wa kilele, Ujerumani inatoa mada za mkutano kuhusu kupunguza pengo katika biashara ya nje, kuongeza uwazi wa masoko ya fedha na mitaji, kukuza uhuru katika uwekezaji wa nchi za viwanda na nchi zinazoweka vizuizi katika uwekezaji, kupinga wizi wa haki ya kunakili ikitarajia kutatua suala la kukosa uwiano katika biashara duniani.
Mbali na hayo, mgongano kati ya Marekani na Russia kuhusu Marekani kupanga mfumo wa makombora katika Ulaya mashariki, pamoja na msimamo mkali wa Ufaransa kuhusu ruzuku za kilimo na matumizi ya nishati ya nyuklia, huenda vitaongeza shida katika mkutano huo wa kilele.
|