|
Rais Hu Jintao wa China tarehe 7 Juni huko Berlin, mji mkuu wa Ujerumani alikutana na waziri mkuu wa India Manmohan Singh, rais Luiz Lula da Silva wa Brazil, rais Thabo Mbeki wa Afrika ya kusini na rais Felipe Calderon wa Mexico walioalikwa kuhudhuria Mkutano wa mazungumzo kati ya kundi la nchi 8 na viongozi wa nchi zinazoendelea, ambapo walibadilishana maoni kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na mazungumzo ya Doha, na masuala mengine, baadaye Mkutano huo ulitoa taarifa ya pamoja.
Msemaji wa wizara mambo ya nje ya China Bwana Liu Jianchao alisema:
Kwenye Mkutano huo, viongozi wa nchi hizo 5 walibadilishana zaidi maoni kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, namna ya kukabiliana pamoja na utandawazi wa uchumi duniani, Mazungumzo ya Doha, na kuhimiza nchi zinazoendelea kuharakisha maendeleo.
Rais Hu Jintao kwanza alitoa hotuba akisema, hivi sasa utandawazi wa uchumi duniani unaendelea kwa kina, na uchumi wa dunia uko kwenye duru jipya la kipindi cha ongezeko. Nchi zinazoendelea zinapojitahidi kutafuta njia ya maendeleo inayolingana na hali halisi ya nchi mbalimbali, inaimarisha mshikamano na ushirikiano, kufanya juhudi za kuhimiza dunia iwe na ncha mbalimbali na uhusiano wa kimataifa uwe wa kidemokrasia, nchi zinazoendelea zimekuwa nguvu kubwa katika kulinda amani ya dunia na kusukuma mbele maendeleo ya pamoja. Lakini kwa jumla hali isiyozisaidia nchi zinazoendelea katika mchakato wa maendeleo ya dunia bado haijabadilika, changamoto na taabu kwa nchi zinazoendelea zinazosababishwa na utandawazi wa uchumi duniani pamoja na masuala ya maendeleo ya nchi zinazoendelea bado hayajatatuliwa. Rais Hu Jintao alisisitiza umuhimu mkubwa wa kuimarisha ushirikiano kati ya China, India, Brazil, Afrika ya kusini na Mexico ambazo ni nchi 5 kubwa zinazoendelea duniani. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bwana Liu Jianchao alisema:
Rais Hu Jintao alisisitiza katika hotuba yake kuwa, idadi ya watu wa nchi hizo 5 inachukua asilimia 42 ya ile ya jumla kote duniani, nchi hizo tano zimeonesha hadhi yao muhimu siku hadi siku katika mambo ya uchumi na biashara kote duniani. Nchi hizo 5 zinabeba wajibu wa kushirikiana ili kukabiliana pamoja na hatari zinazosababishwa na utandawazi wa uchumi duniani, ili kulinda maslahi ya pamoja, kuweka mazingira yanayoyasaidia maendeleo ya nchi zinazoendelea, na kusukuma mbele maendeleo sambamba na dunia nzima.
Rais Hu Jintao alisema, China inakubali kuendelea kuimarisha mazungumzo kati ya nchi zinazoendelea na nchi zilizoendelea, wakati huo huo lazima kujitahidi kuongeza sauti ya nchi zinazoendela kuhusu utaratibu wa mazungumzo, mada kwenye mazungumzo na matokeo ya mazungumzo, ili kujitahdii kujenga uhusiano wa kiwenzi wa aina mpya wa maendeleo ya dunia nzima katika hali yenye usawa, kunufaishana na kupata maendeleo ya pamoja.
Suala la mabadiliko ya hali ya hewa ni suala kuu linalojadiliwa kwenye Mkutano huo wa mazungumzo, pia ni suala lililojadiliwa zaidi kwenye Mkutano wa viongozi wa nchi zinazoendelea. Rais Hu Jintao alidhihirisha kuwa, mabadiliko ya hali ya hewa yanahusiana na maendeleo endelevu ya binadamu wote, China inatilia maanani uhifadhi wa mazingira na maendeleo endelevu, na kuweka mkazo katika kudhibiti utoaji wa hewa zinazosababisha kuongezeka kwa jodo duniani. China inatekeleza kwa makini mkataba wa kimataifa, kuchukua sera na hatua mbalimbali kwa kuhimiza marekebisho ya miundo ya uchumi, kubadilisha njia ya kujipatia ongezeko la uchumi, kubana matumizi ya nishati, kuongeza ufanisi wa matumizi ya nishati, kuendeleza nishati endelevu, kutekeleza miradi ya kujenga mazingira ya viumbe na kufanya juhudi kubwa kwa ajili ya kupunguza hali ya kuongezeka kwa joto duniani.
Hotuba ya rais Hu Jintao wa China iliitikiwa na viongozi wa nchi nyingine. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China,Bwana Liu Jinachao alisema:
Viongozi wa nchi mbalimbali walisisitiza kuwa, kuhusu suala la mabadiliko ya hali ya hewa, lazima kufuata kanuni ya "kubeba wajibu wa pamoja na wa tofauti", na kuzihimiza nchi zilizoendelea zitekeleze ahadi zao, na zipunguze kwanza utoaji wa hewa zinazosababisha kuongezeka kwa joto duniani, na nchi zinazoendelea pia zitatoa mchango wao.
|