Viongozi wa kundi la nchi 8 tarehe 7 Juni walifanya Mkutano huko Heligendamm, Ujerumani, wakijadili masuala mengi yakiwemo uhifadhi wa hali ya hewa, usalama wa nishati, misaada kwa Afrika, na maendeleo ya uchumi wa kimataifa. Katika hali isiyotarajiwa na watu , kundi hilo la nchi 8 lilifikia maoni ya pamoja kuhusu masuala mengi makubwa ambayo yalidhaniwa kuwa na maoni tofauti.
Kwanza kundi la nchi 8 lilipata maendeleo makubwa kuhusu uhifadhi wa hali ya hewa. Viongozi wa nchi mbalimbali za kundi hilo wanaona kuwa wanapaswa kuzingatia kuweka malengo ya lazima kupunguza hewa zinazosababisha kuongezeka kwa joto duniani, yaani ifikapo mwaka 2050 utoaji wa hewa upungue kwa zaidi ya asilimia 50 tofauti na kiwango cha mwaka 1990. Baada ya Mkutano, Chansela wa Ujerumani Angela Merkel alisema, nchi wanachama wa kundi hilo zimekubaliana kuwa kwenye Mkutano wa mazingira wa Umoja wa Mataifa utakaofanyika kwenye Kisiwa cha Bali nchini Indonesia mwishoni mwa mwaka huu, pande mbalimbali zitajadili suala la mabadiliko ya hali ya hewa kwenye mfumo wa Umoja wa Mataifa. Kabla ya Mkutano huo, kutokana na migongano mikubwa kati ya nchi za Ulaya na Marekani kuhusu malengo ya kupunguza utoaji wa kiasi gani wa hewa ya carbon dioxide, hata hakuna mtu aliyeweza kufikiri kuwa pande mbili ziliweza kufikia maoni ya pamoja katika majadiliano ya saa kadhaa tu. Lakini jumuia fulani za kimataifa ziliona kuwa, makubaliano yaliyofikiwa na nchi 8 yanaonekana si ya wazi sana, na Marekani haijabadilisha kimsingi msimamo wake. Marekani itaweza kuchukua hatua zenye nguvu zaidi au la kuhusu mabadiliko ya hali hewa, hii itajulikana kwenye Mkutano wa hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Aidha, mabadiliko yasiyotarajiwa yametokea katika suala la Marekani kuweka mfumo wa ulinzi dhidi ya makombora kwenye Ulaya ya kati. Kabla ya Mkutano huo, Russia ililaani hatua hiyo ya Marekani, hata rais Putin alitishia kuwa ulaya itakuwa shabaha yamakombora ya Russia . Lakini kwenye Mkutano wa rais Putin na rais Bush, rais Putin alitoa wazo linalomshangaza Bush na dunia nzima, alisema Marekani inaweza kujenga mfumo wa ulinzi dhidi ya makombora nchini Azerbainjian, nchi jirani ya Iran, ili kupambana na tishio la makombora ambayo huenda yatarushwa kutoka Iran, kufanya hivyo Marekani haina haja ya kuweka mfumo kama huo kwenye Ulaya ya kati, na makombora ya Russia pia hayatalenga shabaha halisi dhidi ya Ulaya. Rais Bush hakujua kama wazo hilo la Putin ni zuri au la, ila tu alisema kuwa shauri hilo la Putin "ni lenye maana sana", bora kuanzisha ushirikiano kuliko kuzusha hali ya wasiwasi. Habari zilisema kuwa, marais hao wawili walikubaliana kuwa, Tarehe 1 Julai mwaka huu wakati rais Putin atakapotembelea Marekani, pande hizo mbili zitajadili zaidi suala hilo. Ndiyo maana mkwaruzano kati ya Russia na Marekani kuhusu mfumo wa ulinzi dhidi ya makombora umetowekwa kwa muda.
Zaidi ya hayo, kundi la nchi 8 limetoa uchambuzi wenye juhudi kubwa kuhusu hali ya uchumi wa dunia kwa hivi sasa. Kabla ya mkutano, wataalamu fulani waliona kuwa, dunia inakabiliwa na hali isiyo ya uwiano katika mambo ya uchumi, pengo la biashara la nchi za Ulaya na Marekani, urali wa biashara wa nchi zinazoendeleza kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni, pamoja na suala la kuongezeka kwa thamani ya fedha za Asia, yote hao yanatazamiwa kutatuliwa kwa haraka. Lakini taarifa iliyotolewa baada ya Mkutano wa wakuu wa kundi la nchi 8 imeona kwa kauli moja kuwa, hali ya uchumi wa dunia inaendelea vizuri, sehemu mbalimbali za uchumi duniani zimepata ongezeko zuri la uwiano . Maendeleo endelevu yameonekana zaidi katika mambo ya uchumi wa Marekani, na uchumi wa Ulaya na Japan pia umepata nguvu ya uhimizaji wa ongezeko. Taarifa hiyo pia imezisifu nchi za Asia zenye maendeleo ya kasi kwa kupiga hatua ya kwanza katika kutekeleza sera ya ubadilishaji wa fedha wenye unyumbufu.
Na Mkutano huo pia umefikia maoni ya pamoja kuhusu kuimarisha mazungumzo kati yao na nchi kubwa zinazoendelea. Viongozi wa kundi la nchi 8 wameona kwa kauli moja kuwa, lazima kushirikiana na nchi hizo kubuni kwa pamoja mpango kuhusu mchakato wa utandawazi wa uchumi duniani.
|