Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-06-08 19:48:00    
Askari wa China wanalinda amani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo

cri

Tarehe 21 mwezi Machi, mwaka 2007, askari 218 wa kikosi cha kulinda amani cha China nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo waliokuwa watakamilisha jukumu lao walipawa nishani za kulinda amani ya Umoja wa Mataifa. Bi. Sun Jie mwenye umri wa miaka 22 alikuwa askari mwanamke mweye umri mdogo zaidi katika kikosi cha helmeti ya bluu cha Umoja wa Mataifa.

Bibi. Sun Jie ni mwuguzi wa kikundi cha matibabu cha hospitali ya sehemu ya kijeshi ya Lanzhou. Mwezi Agosti mwaka 2006 na wenzake wa kikundi cha matibabu cha kikosi cha kulinda amani cha China waliwasili Bukavu, mji mkuu wa mkoa wa Kivu ya kusini ulioko mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

Wakati Bibi Sun Jie alipozungumzia hali ya sehemu hiyo, alisema "kabla ya kuondoka nyumbani, niliambiwa kuwa kuna magonjwa mengi ya kuambukiza nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, magonjwa ya Malaria ambayo yalitokomezwa nchini China bado yapo kila mahali nchini humo. Watu wa nchi hiyo wameanza kuishi katika hali ya utulivu baada ya vita vya muda mrefu, lakini hali ya usalama bado ni ngumu. Mji wa Bukavu ni sehemu inayogombewa na jeshi la serikali na jeshi la upinzani la nchi hiyo, matukio ya kimabavu yanatokea mara kwa mara. Usiku wa siku moja, nilisikia mlio wa bunduki kwenye sehemu karibu na kituo cha kikundi chetu cha matibabu.".

Sun Jie anasema, alipokuwa nyumbani China yeye akiwa mwuguzi anatakiwa kufanya vizuri kazi ya kawaida, lakini akiwa nchi ya nje kulinda amani siyo tu anapaswa kufanya vizuri kazi ya mwaguzi bali pia anapaswa kutilia maanani vitendo vyake, kwa sababu yeye anaonesha sura ya mwanajeshi wa China.

Sun Jie na wenzake walipata heshima na urafiki kutokana na kazi zao zenye umakini. Kapteni Sarkisian wa kikosi cha kulinda amani cha Uraguay alimwambia mwandishi wa habari kuwa, mwezi Januari mwaka 2007 alipata ugonjwa wa malaria na kutibiwa kwenye hospitali ya China nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Wakati huo yeye alikuwa anatapika sana na kuwa na homa kali. Sun Jie alimwangalia hadi saa 9 asubuhi ya siku lifuta. Baada ya Bw. Sarkisian kupona na kurudi katika jeshi lake, alikwenda hospitali ya China mara kwa mara kumtembelea Bibi Sun Jie na wenzake, kila mara analeta maua kuonesha shukura ni yake kwa marafiki wa China.

Sun Jie alisema, alikwenda uwanja wa ndege wa Kavumu na chuo kikuu cha Bukavu kupokea na kusindikiza wagonjwa mara kwa mara. Lakini kituo cha kikundi cha matibabu cha China kiko sehemu yenye umbali wa kilomita 30 kutoka uwanja wa ndege, na njia kati ya sehemu hizo mbili ina vipengele.

Baba yake wa Sun Jie aliwahi kuwa mwanajeshi, aliunga mkono sana chaguo la binti yake. Aliona kuwa, akiwa mwanajeshi, ni fahari kubwa kupata nafasi ya kwenda nchi ya nje kulinda amani, na kuonyesha sura ya wanajeshi wa China. Mama yake wa Sun Jie alielewa uchaguzi wa binti yake, lakini ana wasiwasi sana, hata hawezi kulala kila usiku.

Sun Jie aliona safari hii ya kulinda amani kwenye nchi ya nje ni somo muhimu zaidi katika maisha yake. Alisema kuwa, niliona wasichana wengi wa rika yangu wenye sura nzuri mjini Bukavu ambao walibeba mizigo mizito ya maisha. Vita ya muda mrefu ilileta maafa makubwa kwa nchi hiyo ya Afrika, watu wa nchi hiyo wanajitahidi kuishi katika hali ya umaskini. Wanajeshi wa China walikwenda katika nchi hiyo kwa ajili ya kuisaidia nchi hiyo kujitoa kutoka kwenye balaa, kutibu majeraha ya watu wa nchi hiyo, na kuwafanya watu hao waishi maisha kwa heshima.

Wasikilizaji wapendwa, Bibi Sun Jie ni mwanajeshi mmoja wa kikosi cha kulinda amani cha China nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, na wanajeshi wengine kutoka China pia walifanya juhudi katika kazi zao na kuwasaidia wenyeji wa sehemu mbalimbali za nchi hiyo.

Naibu kiongozi wa kikosi cha uhandisi cha China cha jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo Bw. Zhang Yongheng alimwabia mwandishi wa habari kuwa, wakati walipofanya kazi, watu wenye silaha wasiojulikana hujitokeza mara kwa mara karibu na sehemu waliyofanya kazi, walinda usalama wenye silaha walishika bunduki kila wakati, na kukaa macho juu ya watu hao wenye silaha. Lakini katika hali hii ngumu, wanajeshi wa China walikamilisha jukumu lao kwa muda uliowekwa na tume maalumu ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, na kusifiwa na maofisa wa Umoja wa Mataifa.

Kikosi cha uhandisi cha China kilifanya kazi ya kulinda miradi 20 ikiwemo ujenzi wa sehemu ya kuegesha ndege, kwenye uwanja wa ndege. ujenzi wa madaraja, na ukarabati wa barababara. Kilitengeneza barabara yenye urefu wa kilomita zaidi ya 50, kuondoa matope mita za mraba zaidi elfu 2, kufanya uchunguzi wa miradi kwa mara 15, na kukagua barabara zaidi ya kilomita 2700.

Kikundi cha matibabu cha China kiliwatibu majeruhi na wagonjwa 1188, na kutoa huduma nzuri ya matibabu kwa maofisa na askari wa kulinda amani wa tume maalumu ya Umoja wa Mataifa nchini humo. Wanajeshi, madaktari na wauguzi wa China wamejenga daraja la urafiki kati ya wananchi wa China na wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

Kamanda wa jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo Lieutenant General Babaca Geyer tarehe 26 mwezi Juni alipokagua kikundi cha uhandisi cha China cha kikosi cha kulinda amani alisema, wanajeshi wa helmeti ya bluu wa China walipata mafanikio makubwa wakati walipofanya kazi ya kulinda amani, na kufanya kazi muhimu kwa kusukuma mbele mchakato wa amani ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Alisema kuwa, Wanafuata nidhamu kwa makini na kuwatendea kirafiki watu wa nchi hiyo, hivyo walipata heshima na uaminifu.