Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-06-11 17:44:56    
Mazungumzo kati ya Iran na Umoja wa Ulaya yatakwamua utatuzi wa suala la nyuklia la Iran?

cri

Naibu katibu wa kamati ya usalama ya taifa ya Iran Bw. Javad Vaidi pamoja na msaidizi wa Bw. Javier Solana, mwakilishi wa ngazi ya juu wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia sera za kidiplomasia na usalama, wamekuwa na mazungumzo tarehe 11 mwezi Juni. Hayo ni mazungumzo ya ngazi ya juu yaliyofanyika kwa mara nyingine tena katika muda usiozidi wiki mbili baada ya mazungumzo ya Madrid kati ya pande hizo mbili.

Vyombo vya habari vimeona kuwa, kabla ya kufanyika kwa mazungumzo hayo, misimamo ya pande husika haikuwa na dalili ya kulegea. Hivi karibuni ofisa mmoja wa Umoja wa Mataifa, ambaye anataka jina lake lihifadhiwe, alisema, hadi hivi leo Iran imefunga mashine pewa 2,000 katika zana zake za nyuklia, na itaweza kutimiza lengo lake la kufunga mashine pewa 3,000 hadi mwezi ujao, ambapo itafikia kiwango halisi cha kuweza kuzalisha nishati ya nyuklia kiwandani. Endapo maneno ya ofisa huyo wa Umoja wa Mataifa ni ya kweli, basi kinadharia, Iran itaweza kuzalisha uranium nzito safi kiasi cha kuweza kutengeneza bomu moja la atomiki ndani ya muda wa mwaka mmoja.

Marekani na nchi marafiki wa muungano wao zimekuwa zikiishuku Iran kujiandaa kutengeneza silaha za nyuklia kwa kisingizio cha kuzalisha nishati ya nyuklia kwa matumizi ya kiraia, zikitaka baraza la usalama la Umoja wa Mataifa liiwekee Iran vikwazo vikali vikiwemo vikwazo vya kiuchumi.

Mkutano wa kilele wa kundi la nchi nane ulitoa taarifa tarehe 8 mwezi Juni kuhusu suala la nyuklia la Iran, ikisema, endapo Iran haitaki kufanya usuluhishi kuhusu suala la nyuklia, basi kundi la nchi nane litachukua hatua kali dhidi yake. Pamoja na hayo, taarifa inasema, endapo Iran itaweza kuidhirisha jumuiya ya kimataifa kuwa, mpango wake wa nyuklia utatumika kwa lengo la amani, basi uhusiano kati ya kundi la nchi nane na Iran katika maeneo mbalimbali utafungua ukurasa mpya, ambao siyo tu eneo la nishati la nyuklia peke yake, bali ni pamoja na maeneo mengine ya siasa, uchumi na teknolojia.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Seyed Mohamma-Ali Hosseini alitoa taarifa tarehe 9 ikieleza masikitiko kuhusu taarifa iliyotolewa na mkutano wa kilele wa kundi la nchi nane kuhusu suala la nyuklia la Iran. Katika taarifa hiyo Ali Hosseini alisema, "Hadi hivi sasa Iran imekuwa ikidumisha uhusiano mzuri wa ushirikiano na sehemu mbalimbali duniani pamoja na jumuiya ya kimataifa likiwemo shirika la nishati la atomiki la dunia, inafuata 'mkataba wa kutoeneza silaha za nyuklia', na kuendeleza teknolojia ya nyuklia kwa matumizi ya amani. Sisi tumesikitishwa taarifa iliyotolewa na mkutano wa kilele wa kundi la nchi nane. Alisema Iran itaendelea kufanya mazungumzo ya kidiplomasia ili kuondoa mashaka ya jumuiya ya kimataifa kuhusu shughuli za nyuklia za Iran, sasa Iran iko tayari kushiriki mazungumzo yoyote yasiyokuwa na masharti ya kabla.

Siku hiyo hiyo, mwenyekiti wa kamati ya uthibitishaji wa manufaa ya taifa aliyekuwa rais wa zamani wa Iran Bw. Akbar Hashemi Rafsanjani alisema, Iran inapuuza taarifa ya kundi la nchi nane. Alisema, "Nchi hizo za viwanda siyo mara ya kwanza kukusanyika pamoja kuitaka Iran iache shughuli za nyuklia. Lakini hivi sasa Iran imekuwa na akili na tahadhari za kutosha za kupita katika kipindi hicho chenye shida.