Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-06-12 16:13:07    
Rais Bush amaliza ziara yake barani Ulaya

cri

Tarehe 4 hadi 11 Juni, rais Bush wa Marekani kwa nyakati tofauti alitembelea nchi 6 za Ulaya ambazo ni Czech, Ujerumani, Poland, Italia, Albania na Bulgaria. Wakati wa ziara yake hiyo alihudhuria mkutano wa wakuu wa kundi la nchi nane uliofanyika nchini Ujerumani, na aliafikiana na nchi za Ulaya katika suala la kuwa joto kwa hali ya hewa duniani. Wakati huohuo rais Bush alizishawishi nchi za Ulaya ya mashariki kuunga mkono mfumo wa ulinzi dhidi ya makombora wa Marekani, na kuendelea kuweka shinikizo kwa Russia.

Jambo lililofuatiliwa kabisa katika taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya mkutano wa wakuu wa kundi la nchi nane ni maoni ya pamoja yaliyofikiwa katika suala la mabadiliko ya hali ya hewa. Viongozi wa kundi la nchi nane walikubali "kuzingatia kwa makini" mapendekezo yaliyotolewa na Umoja wa Ulaya, Canada na Japan, kuhusu utoaji wa hewa ya carbon dioxide inayosababisha kuongezeka joto duniani upunguzwe kwa asilimia 50 kuliko mwaka 1990 ifikapo mwaka 2050, na kutumai kuwa nchi zinazotoa kwa wingi hewa ya carbon dioxide inayosababisha hali joto kufanya juhudi kwa ajili hiyo.

Ingawa viongozi wa nchi za Ulaya walifanya juhudi kubwa, lakini rais Bush hakubadilisha msimamo wake katika suala hilo. Ingawa kabla ya ziara yake rais Bush alitoa mpango wa kimkakati kuhusu kudhibiti hali ya kuongezeka joto duniani, lakini hakutoa ahadi yoyote katika hatua halisi. Licha ya hayo, rais Bush bado anashikilia kupunguza utoaji wa hewa ya carbon dioxide kwa kupitia mpango wa soko, sio kupitia hatua za lazima za serikali.

Jambo muhimu la ziara ya rais Bush ni kuishawishi Russia kupokea mpango wa Marekani wa kujenga vituo vya ulinzi dhidi ya makombora barani Ulaya. Vituo hivyo vitajengwa nchini Poland na Czech. Marekani ilisema, lengo la mpango huo ni kukinga mashambulizi ya makombora ya Iran na Korea ya Kaskazini, na kulinda usalama wa bara la Ulaya. Lakini Russia inaona kuwa Marekani itakuwa na uwezo wa kufuatilia na kuzuia makombora ya Russia.

Kwenye mkutano wa wakuu wa kundi la nchi nane, rais Putin wa Russia alitoa pendekezo jipya la kutumia kituo cha rada cha Azerbaijan kuendeleza mfumo wa ulinzi dhidi ya makombora. Baadaye rais Putin alipendekeza kuwa, mfumo wa kuzuia makombora wa Marekani unaweza kuwekwa nchini Uturuki au Iraq. Mapendekezo hayo ni mapya kwa rais Bush, na pande hizo mbili zinakubali kuunda kikundi cha kazi ili kujadili mapendekezo hayo.

Wachambuzi wanaona kuwa, uko uwezekano mdogo kwa serikali ya Bush kuafikiana na nchi nyingine katika suala la mfumo wa ulinzi dhidi ya makombora. Kabla ya hapo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bibi Condoleezza Rice alieleza kwa wazi kuwa Marekani haitaacha mpango wake.

Licha ya kuhudhuria mkutano huo, rais Bush alitumia muda mwingi katika kuzuru nchi za Ulaya ya mashariki, yaani "Ulaya mpya" iliyosema serikali ya Bush. Vyombo vya habari vinachambua kuwa, rais Bush alichukua Czech kuwa ziara yake ya kwanza barani Ulaya, na kuzuru Poland baada ya mkutano wa wakuu wa kundi la nchi nane, pia inaonesha umuhimu wa nchi hizo mbili za Ulaya ya mashariki katika mkakati wa Marekani.

Lengo muhimu la ziara ya rais Bush kutembelea nchi za Ulaya ya mashariki ni kuzishawishi nchi hizo kuunga mkono mfumo wa ulinzi dhidi ya makombora. Lakini watu wa nchi kadhaa za "Ulaya mpya" walifanya maandamano ya kuipinga Marekani, na kupinga vita katika sehemu mbalimbali.

Wachambuzi wanasema, ziara hiyo ya rais Bush inaonesha kuwa Marekani inatilia maanani zaidi maslahi yake ya kimkakati ya sehemu hiyo. Kupitia kuweka mfumo wa ulinzi dhidi ya makombora barani Ulaya, Marekani inataka kubana nafasi ya mkakati ya Russia, na kudumisha hadhi yake ya nchi kubwa yenye mabavu duniani.

Idhaa ya kiswahili 2007-06-12