Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-06-13 21:10:25    
Watu wanaotunza Kasri la Potala

cri

Kwenye mlima mwekundu wa Lahsa, mji mkuu wa mkoa unaojiendesha wa Tibet, kusini magharibi mwa China kuna Kasri la Potala linalojulikana sana duniani. Ili kuhifadhi kasri hilo takatifu la kabila la Watibet, na kuwawezesha watu dunia kujionea utakatifu na uzuri wa kasri hilo, wafanyakazi na watawa wa idara ya usimamizi wa Kasri la Potala wamefanya juhudi kubwa katika kulitunza kasri hilo.

Kasri la Potala lilianza kujengwa katika karne ya 7, mwanzoni liliitwa "kasri la mlima mwekundu", ambalo liliharibika siku hadi siku kutokana na kuzorota kwa enzi ya ufalme wa Tufan. Katika karne ya 17, Dalai Lama wa tano alijenga kasri kubwa yaani "Kasri la Potala" kwenye sehemu iliyokuwa ya "kasri la mlima mwekundu". Baadaye Kasri la Potala limekuwa kituo cha siasa na dini cha Tibet. Mwaka 1994 Kasri la Potala liliorodheshwa kuwa urithi wa utamaduni duniani na shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO kutokana na usanii wake wa kiujenzi wa kabila la Watibet, na mkusanyiko mkubwa wa mabaki ya kale ya utamaduni yenye thamani kubwa.

Kasri la Potala lilianza kufanyiwa ukarabati mwaka 1994, mabaki mengi ya kale ya utamaduni yaliyoko ndani ya kasri hilo yalipaswa kuhamishwa, na namna ya kuyahamisha mabaki hayo ya utamaduni yenye thamani kubwa kulifuatiliwa sana na watu idara mbalimbali. Ili kufanya kazi hiyo vizuri, wafanyakazi wa idara ya usimamizi wa kasri hilo walikuwa wamejifunza kwa makini sheria na utaratibu husika wa China kuhusu mabaki ya kale ya utamaduni na ujuzi wa kuhifadhi mabaki hayo. Naibu mkuu wa idara hiyo Bwana Ding Changzheng alifahamisha akisema:

"Tunaongeza nguvu kazi ya kutunza, kusimamia na kufanya utafiti kuhusu mabaki ya kale ya utamaduni ya Kasri la Potala, kuimarisha hifadhi ya kila siku, kufanya ukarabati kamili kwa madirisha ya nje ya jengo kuu la kasri jekundu, na kufanya ukarabati kwa baadhi ya michoro ya rangi ukutani, kupaka dhahabu kwenye sanamu zote za kale za mabudha zilizo katika ukumbi wa Dalai lama wa 13, kukarabati sanamu ndogo 640 za mabudha, na kukamilisha kazi ya kubainisha na kuorodhesha misahafu.

Kuhamisha sanamu za mabudha na misahafu ni kazi kubwa sana. Kwa sababu sanamu za mabudha na vitabu vya msahafu yote ni mabaki ya kale yenye thamani kubwa, hivyo vinapaswa kuhamishwa na watu moja baada ya nyingine kutoka ghorofa moja hadi nyingine. Baadhi ya sanamu za mabudha ni kubwa sana, tena zilifinyangwa kwa udongo, ni rahisi kuharibika, na katika baadhi ya ukumbi kuna sanamu elfu kadhaa za mabudha, sanamu zote kabla ya kuhamishwa zinapaswa kuwekwa alama na kuthibitishwa sifa yake, baada ya ukarabati wa ukumbi kukamilika, sanamu hizo zitarudishwa kama zilivyokuwa. Kutokana na juhudi kubwa walizofanya kwa makini wafanyakazi wa idara ya usimamizi ya Kasri la Potala na watawa wa kasri hilo, mwaka jana sanamu za mabudha na mabaki ya kale ya utamaduni 4800 na vitabu zaidi ya 1000 vilihamishwa kwa mafanikio. Naibu mkuu wa idara ya usimamizi wa Kasri la Potala Bwana Wang Duo alisema:

"Tukishirikiana na kamati ya usimamizi wa kidemokrasia ya hekalu la Jokhang, tumemaliza kazi za kurudufu, kuhamisha na kurudisha misahafu zaidi ya mia moja. Ili kushirikiana na idara husika za serikali na mkoa wa Tibet kufanya uchunguzi kuhusu misahafu ya 'Beiye', yaani misahafu iliyoandikwa kwenye majani ya miti ya Shell, mwaka jana idara ya usimamizi wa Kasri la Potala iliwatuma watu maalum kuandaa orodha ya misahafu 108 ya "Beiye", kupima ukubwa wake na kuripoti tarakimu husika kwa idara husika."

Ili kusimamia vizuri zaidi Kasri la Potala, idara hiyo ya usimamizi pia imekusanya takwimu kuhusu hali ya vyumba, milango na madirisha na nguzo za kasri hilo, kuorodhesha misahafu elfu kumi, kuweka namba na kuihifadhi ipasavyo. Kazi za kuorodhesha mabaki ya kale ya utamaduni kwenye Kasri la Potala zimefanyika kwa miaka zaidi ya kumi, kwa kweli kazi hiyo ni kubwa zaidi na yenye utatanishi zaidi hata kuliko mradi wa ukarabati wa kasri hilo lenyewe. Baada ya kukamilika kwa kazi hiyo, takwimu zilizowekwa zitatoa huduma kwa watafiti wa nchini China na nchi za nje na watalii wa duniani.

Wakati wa kufanya ukarabati wa Kasri la Potala na kuorodhesha mabaki ya kale ya utamaduni, idara ya usimamizi wa Kasri hilo pia inatilia maanani kazi za kulinda usalama. Licha ya kuweka kamera za kusimamia, mkuu wa idara ya usimamizi wa kasri hilo Bwana Jiangbagesan kila siku anashikilia kufanya doria kwenye hekalu hilo. Akisema:

"Ingawa tumeweka vifaa vya kisasa vya kusimamia hali ilivyo, lakini lazima tuwe na tahadhari ili kulinda vizuri zaidi mabaki ya kale ya utamaduni kwenye Kasri la Potala."

Ili kueneza utamaduni wa Kasri la Potala, baadhi ya wafanyakazi na watawa ingawa wamezeeka, lakini wanaendelea kuchangia ujenzi wa kasri hilo na kuwaandaa warithi wao. Si kama tu wanajifunza misahafu, bali pia wanajifunza lugha ya Kichina na Kiingereza, kila wakiulizwa na mahujaji au watalii wa nchini China na nchi za nje huwa wanawajibu kwa uchangamfu nao wameitwa kuwa kamusi hai ya Kasri la Potala.