Jioni tarehe 13, kundi la Hamas lilifanya mashambulizi dhidi ya vituo vitatu muhimu vya jeshi la ulinzi la taifa linaloongozwa na kundi la Fatah katika mji wa Gaza, mgogoro kati ya makundi hayo mawili umeingia katika kipindi kipya cha mapambano. Hivi sasa kundi la Hamas limedhibiti ukanda wa Gaza. Hali hiyo imedhihirisha wazi zaidi hatari ya kutokea kwa mfarakano nchini Palestina kama wataalamu walivyobashiri.
Katika siku hiyo ya tarehe 13, kundi la Hamas lilipambana na kundi la Fatah katika maeneo yote ya ukanda wa Gaza na kwa haraka lilidhibiti maeneo mengi. Katika sehemu ya katikati, vikosi vya Hamas vilifyeka makao makuu ya jeshi la ulinzi la taifa na kisha vilidhibiti kambi kadhaa za wakimbizi, na katika mapambano yote hayo vikosi hivyo vilipata upinzani mdogo tu. Katika sehemu ya kusini ya ukanda wa Gaza, baada ya kuuteka mji wa Khan Yunis saa chache baadaye, kundi la Hamas lilidhibiti miji kadhaa ya pwani. Habari zilizotangazwa katika siku hiyo zilisema, kundi la Hamas limedhibiti sehemu muhimu za kusini na kaskazini za ukanda wa Gaza, iliyobaki ni mji wa Gaza tu. Siku hiyo kwenye ukurasa wa kwanza wa Gazeti la Jerusalem Post kilichapishwa kichwa cha habari kikisema, "Gaza imekuwa ikizama kuwa Hamastina". Hali ambayo Palestina inakabiliwa na hatari ya mfarakano imekuwa ya kweli.
Vyombo vya habari vinaona kuwa kama kweli ukanda wa Gaza ukijitenga na Palestina na kutawaliwa na kundi la Hamas lenye itikadi kali, hakika itasababisha Israel kuuwekea vikwazo vikali zaidi ukanda huo, kwani kundi hilo ambalo linakataa kanuni tatu za "kuacha nguvu za kisilaha, kuitambua Israel na kukubali makubaliano ya amani kati ya Palestina na Israel" ni hatari kubwa kwa Israel. Baada ya kundi la Hamas kushika madaraka, vikwazo kutoka nchi za magharibi vimesababisha theluthi mbili ya watu wa ukanda wa Gaza kuwa maskini. Vikwazo vikiwa vikali zaidi hakika vitasababisha hali mbaya zaidi.
Pili, hali ya usalama wa Israel itakuwa mbaya zaidi. Wakati huo Israel itakabiliwa na tishio la nchi za Iran na chama cha Hezbollah kinachoungwa mkono na Syria kaskazini ya nchi hiyo, na katika sehemu ya kusini magendo ya silaha kwenye mpaka kati ya Misri na Gaza yatakuwa vigumu kudhibitiwa, na kundi la Hamas pengine litaacha vikosi vyake kama vinavyotaka kuishambulia Israel kwa makombora.
Tatu, mazungumzo ya amani kati ya Palestina na Israel yatabadilika. Kwa sababu mwenyekiti wa mamlaka ya Palestina Bw. Mahmoud Abbas hataweza kuwakilisha tena Palestina, na sera zake pia hazitaweza kutekelezwa katika ukanda wa Gaza.
Lakini wafafanuzi wanasema kuwa kutokana na hali ilivyo mfarakano wa Palestina unazuiliwa na pande mbalimbali za ndani na nje ya Palestina. Hivi sasa jumuyia ya kimataifa inatambua tu mamlaka ya kitaifa ya Palestina. Baada ya vita kutokea, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na nchi mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Ulaya, Ujerumani, walitoa taarifa ikimuunga mkono mwenyekiti wa mamlaka ya Palestina Abbas. Kwa kutumia nguvu za kijeshi kundi la Hamas limedhibiti ukanda wa Gaza na kusababisha hali mbaya katika ukanda huo, hatua hiyo hakika haitakubaliwa na jumuyia ya kimataifa.
Mgogoro huo ulichochewa na waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Palestina Bw. Mahmoud Zahar na brigeidi ya Qassam ya Hamas. Na waziri mkuu wa mamlaka ya Palestina anakaa kimya, na alizitaka pande mbili ziwe na uvumilivu na kufanya mazungumzo. Zaidi ya hayo, kundi la Hamas limetoa ushauri wa kusimamisha mapambano kwa masharti. Kwa hiyo hali ya ukanda wa Gaza na uhusiano kati yake na ukingo wa magharibi wa mto wa Jordan bado haijakuwa wazi
Idhaa ya kiswahili 2007-06-14
|