Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-06-15 15:45:31    
Bw. Abbas atangaza kuvunja serikali ya muungano wa kitaifa ya Palestina

cri

Ili kukabiliana na mabadiliko makubwa ya hali ya sehemu ya Gaza, mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina Bw. Mahmoud Abbas tarehe 14 usiku alisaini amri tatu za mwenyekiti: kuvunja serikali ya muungano wa kitaifa ya Palestina; kutangaza sehemu zote za Palestina zikiwemo sehemu za magharibi ya Mto Jordan na Gaza ziingie katika hali ya hatari; kuunda serikali ya dharura mapema kushughulikia mambo ya serikali ya muungano wa kitaifa ya Palestina. Maamuzi hayo ya dharura yanatangaza kuwa ushirikiano kati ya kundi la Fatah na kundi la Hamas umekomeshwa.

Bw. Abbas siku hiyo aliziambia pande nne husika za suala la Mashariki ya Kati maamuzi yake hayo, na kutoa mwito wa kuwekwa kwa jeshi la kimataifa huko Gaza. Habari zinasema kuwa, sehemu ya magharibi ya Mto Jordan imeanza kusaka nguvu ya siasa kali ya kundi la Hamas. Lakini mwanachama wa kundi la Fatah alisema, sehemu ya Gaza kweli imepotezwa, kutegemea Bw. Abbas au kundi la Fatah tu hakuwezi kubadilisha hali hiyo halisi.

Mwezi Marchi mwaka huu, kundi la Fatah na kundi la Hamas yaliunda serikali ya muungano wa kitaifa, ambapo yalitumai kuwa hatua hiyo itaweza kukomesha mgogoro wa kimabavu ndani ya Palestina, ili kujitahidi kuondolewa kwa vikwazo vilivyowekwa na nchi za magharibi kwa serikali ya Palestina baada ya kundi la Hamas kushika hatamu za serikali mwaka jana. Lakini hadi sasa malengo hayo hayakutimizwa. Kinyume chake, mgogoro wa ndani ya Palestina umezidi kuwa mbaya, ambao umesababisha mafarakano ya kisiasa ya sehemu ya Gaza na sehemu ya magharibi ya Mto Jordan.

Tarehe 14 kundi la Hamas liliteka Gaza, sehemu muhimu ya mwisho ya kijeshi ya Fatah, na kutimiza udhibiti kwa sehemu nzima ya Gaza. Hali hiyo inaimarisha zaidi nguvu za Hamas za kupambana na Bw. Abbas. Kuhusu maamuzi ya Bw. Abbas, msemaji wa kundi la Hamas Bw. Sami Abu Zuhri alisema, " kihalisi, maamuzi hayo hayana thamani yoyote ya kimsingi." Waziri mkuu wa serikali ya muungano wa kitaifa ya zamani Bw. Haniya alisema, serikali itaendelea kufanya kazi kama kawaida.

Hamas kuidhitibi Gaza na kuvunjika kwa serikali ya muungano wa kitafia kunazifanya juhudi za amani za nchi jirani zishindwe. Misri, Jordan na Saudi Arabia siku zote zinafanya juhudi kuhimiza mshikamano wa Hamas na Fatah, ili kukabiliana kwa pamoja na masuala husika ya kuanzisha tena mchakato wa amani kati yake na Israel. Kwa upande mmoja zilimuunga mkono Bw. Abbas, na kumsaidia kutoa mafunzo kwa jeshi la usalama, kwa upande mwingine, zilifanya juhudi ili kulegeza msimamo wa kundi la Hamas. Lakini hali ya hivi sasa hakika ni pigo kubwa kwa juhudi zao.

Nchi hizo jirani zina wasiwasi kuhusu usalama wa sehemu hiyo: kwanza wanahofia sehemu ya Gaza inayoongozwa na Hamas itakuwa kituo imara cha kundi lenye siasa kali; pili wana wasiwai kuwa mgogoro utaenea hadi sehemu ya magharibi ya Mto Jordan, na nguvu za Bw. Abbas zitapunguzwa zaidi. Hali hizo mbili huenda zitasababisha vurugu kubwa zaidi kwenye sehemu hiyo.

Hivi sasa pande zote husika zinafanya juhudi mpya ili kusimamisha mgogoro wa ndani wa Palestina. Katibu mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiarabu Bw. Amr Musa tarehe 14 alitangaza kuwa, Umoja wa Nchi za Kiarabu utafanya mkutano wa dharura wa mawaziri wa mambo ya nje ili kujadili hali ya Palestina. Waziri mkuu wa Israel Bw. Ehud Olmert atafanya ziara nchini Marekani hivi karibuni, ambapo zitajadili pia hali ya Gaza.

Katika hali ya hivi sasa, pande zote zimeimarisha nguvu ya ulinzi kwenye mpaka na Gaza, ambapo zote zinachukua tahadhari sana ili kukwepa hali isizidi kupamba moto, wakati huo huo zinasubiri mkutano husika utakaotoa pendekezo mwafaka la kutatua tatizo la Gaza.

Idhaa ya kiswahili 2007-06-15