Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-06-15 16:59:58    
"Darasa la matangazo la Confucius" laanzishwa huko Nairobi Kenya

cri

"Darasa la matangazo la Confucius" limezinduliwa rasmi asubuhi ya tarehe 8 Juni huko Nairobi, Kenya. Darasa hilo lilianzishwa kwa ushirikiano kati ya Ofisi ya kikundi cha uongozi wa kazi ya uenezaji wa lugha ya Kichina cha taifa la China na Radio China Kimataifa.

Asubuhi ya tarehe 8, maonesho hayo murua yalikaribishwa sana na wageni waliohudhuria sherehe ya kuzinduliwa kwa "Darasa la mtangazao la Confucius"

Naibu waziri wa elimu wa China Bwana Yuan Guiren, naibu waziri wa habari na mawasiliano wa Kenya Bwana Koigi Wamwere, balozi wa China nchini Kenya Bwana Zhang Ming na naibu mhariri mkuu wa Radio China Kimataifa Bwana Ding Bangying walihudhuria sherehe ya kuzinduliwa kwa "Darasa la matangazo la Confucius". Bwana Ding Bangying alipojulisha mradi huo alisema,

"darasa hilo ni mradi wa huduma za mafunzo ya lugha ya Kichina zisizotafuta faida, mafunzo hayo yatatolewa kwenye matangazo ya Kiingereza na Kiswahili ya 91.9 FM ya Radio China kimataifa ili kukidhi mahitaji ya watu wa sekta mbalimbali wa Nairobi Kenya, na kuongeza mawasiliano na ushirikiano kati ya China na Kenya pamoja na mashirika mbalimbali ya kimataifa."

Naibu waziri wa elimu wa China aliyefanya ziara nchini Kenya Bw. Yuan Guiren alipongeza kuanzishwa kwa "darasa la matangazo la Confucius", akisema,

"Darasa la matangazo la Confucius limeanzishwa rasmi leo, kwa njia ya radio, litatoa huduma kwa watu wa Kenya hata watu wa sehemu mbalimbali barani Afrika wanaojifunza lugha ya Kichina na utamaduni wa China, na kuridhi mahitaji ya wakenya ya kutaka kuelewa China. Darasa hilo litakuwa daraja kubwa la kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano wa kirafiki kati ya China na Kenya, na kuongeza urafiki kati ya wananchi wa nchi hizo mbili."

Siku hiyo waziri wa elimu wa Kenya pia alipongeza kuanzishwa kwa Darasa hilo kwa kupitia mjumbe wake. Mjumbe wake alisema,

"Mradi huo ulianzishwa kwa wakati mwafaka, na unaambatana na matakwa ya aina mbalimbali ya kupata mafunzo ya lugha, pia unatoa njia mpya ya kujifunza lugha ya Kichina, ili watu waweze kujifunza lugha ya Kichina kwa urahisi bila kuzuiliwa na mabadiliko ya sehemu."

Naibu waziri wa habari na mawasiliano wa Kenya Bwana Koigi Wamwere alisema kwenye sherehe hiyo kuwa, kutoa mafunzo kwa njia ya radio ni mfano wa kuigwa kwa Kenya, Alieleza matumaini yake kuwa Shirika la utangazaji wa Kenya KBC litaiga mfano huo na kutoa mafunzo radioni ya lugha za Kichina, Kiingereza na Kiswahili.

Balozi wa China nchini Kenya Bw. Zhang Ming kwenye sherehe ya kuzinduliwa kwa "darasa la matangazo la Confucius " alisema,

"nina matumaini kuwa "darasa la matangazo la Confucius" linaweza kutoa huduma kwa wakenya wengi zaidi wanaojifunza lugha ya Kichina. Nina matumaini kuwa darasa hilo linaweza kutoa fursa nyingi zaidi kwa watu wanaojifunza lugha ya Kichina."

Bi. Susan ni Mpenzi wa lugha ya kichina, kwenye sherehe hiyo alisema kwa kichina kisicho sanifu akisema,

"Naona kuwa baada ya kuanzishwa kwa "Darasa la matangazo la Confucius", ni rahisi kwetu kujifunza lugha ya kichina, na gharama ya kujifunza itapungua."

Naibu mhariri mkuu wa Radio China Kimataifa Bwana Ding Bangying alijulisha kuwa, "Darasa la matangazo la Confucius" litatoa mafunzo ya lugha ya Kichina kwenye matangazo ya kiingereza na Kiswahili ya Radio China Kimataifa kila siku, baadaye litafanya shughuli mbalimbali za kusaidia mafunzo ya kichina, kama vile kutoa vitabu vya mafunzo vya matangazo, kufanya shughuli za mawasiliano kuhusu kujifunza lugha ya Kichina, kutazama filamu za Kichina na vipindi vya televisheni ya Kichina, kufanya maonesho ya utamaduni wa China n.k.

Hivi sasa "Darasa la matangazo la Confucius" limeanzishwa katika nchi mbalimbali za Asia, Afrika, Ulaya na Amerika, ambalo linakaribishwa sana na wasikilizaji wa nchi mbalimbali.

Idhaa ya kiswahili 2007-06-15