Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-06-20 18:42:25    
Mtandao wa Internet wa njia pana zinastawi nchini China

cri

Kutokana na maendeleo ya kasi ya teknolojia ya mtandao wa Internet na mahitaji ya watu kufanya kazi nyingi zaidi kwenye mtandao, mtandao wa Internet wa njia pana ambao unaweza kukidhi vizuri zaidi mahitaji hayo umechukua nafasi ya mtandao wa zamani, na teknolojia hiyo imekuwa inafuatiliwa zaidi katika sekta ya upashanaji wa habari. Ingawa China ni nchi inayoendelea, lakini mtandao wa Internet wa njia pana umeshapata maendeleo makubwa nchini China.

Basi mtandao wa Internet wa njia pana ni wa namna gani? Wataalamu wanaeleza kuwa, hivi sasa mtandao wa Internet wa njia pana una ngazi tatu, yaani mtandao mkuu, mtandao kati ya miji na mtandao unayounganisha maeneo ya makazi mijini, ngazi hizo za mtandao zinafanana na zile za mtandao wa barabara za mwendo kasi, barabara kati ya miji na barabara zinazounganisha maeneo ya makazi. Kwa kawaida, mtandao ambao ufanisi wa mtandao mkuu unaweza kufikia 2.5G kwa sekondi, na ule wa mtandao ya ngazi ya tatu unaweza kufikia 1m kwa sekondi, unachukuliwa kuwa mtandao wa Internet wa njia pana.

Kwa mfano, kama mtandao wa Internet unachukuliwa kuwa ni barabara, basi kutokana na manedeleo ya teknolojia ya mtandao, magari yanayosafiri kwenye barabara hiyo yameongezeka sana. Mtandao wa Internet wa njia pana ndio ni barabara pana ambayo inayowezesha magari mengi zaidi kusafiri bila msongamano.

Mtandao wa Internet wa njia pana umekuwa miundombinu muhimu wa mtandao wa upashanaji wa habari duniani, na unatumika katika kupashana habari za sekta za siasa, uchumi na utamaduni. Mtandao wa Internet wa njia pana pia umeendelea kwa kasi nchini China, naibu mkuu wa taasisi ya uhandisi ya China Bw. Wu Hequan alisema:

"idadi ya watumiaji wa mtandao wa Internet wa njia pana inachukua asilimia 70 ya ile ya watumiaji wa mtandao wa Internet, na idadi hiyo pia inaongezeka kwa asilimia 1 kila mwezi."

Wataalamu wanaeleza, sekta ya upashanaji wa habari ikiwa ni sekta ya kimsingi inayounga mkono na kuelekeza maendeleo ya uchumi wa taifa, inatoa mchango mkubwa katika kuhimiza maendeleo ya uchumi wa China na kuinuka kwa kiwango cha maisha ya watu wa China, katika siku za baadaye, mtandao wa Internet wa njia pana utaweza kutoa huduma mbalimbali za kurahisisha maisha ya watu, zikiwemo kuagiza video unazotaka kuziona, mawasiliano ya simu kwa njia video, tele-conference kwa njia ya video, biashara kwenye mtandao, kufanya kazi za ofisini kwenye mtandao, kupata matibabu na elimu kupitia mtandao. Wakazi wanaweza kuagiza kuonesha kwa hiara matangazo au filamu zilizowekwa kwenye database, hata kama watu mia kadhaa au zaidi ya elfu moja wakiagiza huduma hiyo kwa wakati mmoja, haitaathiri hata kidogo kasi ya maonesho hayo. Ili kutimiza lengo hilo, waziri wa upashanaji wa habari wa China Bw. Zhang Xinsheng alisema:

"wakati wa kueneza matumizi ya mtandao wa internet wa njia pana, China pia inapaswa kuendelea kusukuma mbele marekebisho ya mtandao wa internet uliopo, na kutumia kikamilifu teknolojia ya uunganishaji wa mtandao bila waya ili kuendelea kusukuma mbele shughuli za kuongeza uwezo wa mtandao wa Internet wa njia pana, kuboresha muundo wa mtandao na kuendelea kuinua ufanisi wa mtandao huo."

Imefahamika kuwa, hivi sasa China ina watumiaji milioni 97 wa mtandao wa Internet wa njia pana, ambayo idadi hiyo inachukua nafasi ya pili baada ya Marekani kote duniani. Asilimia 74 ya watumiaji wa mtandao huo duniani wako katika nchi zilizoendelea, watumiaji wa China wanachukua asilimia 17.5, na watumiaji walioko nchi nyingine zinazoendelea wanachukua asilimia 10 hivi tu.

Inakadiriwa kuwa, ifikapo mwaka 2010, thamani ya jumla ya soko la mtandao wa Internet wa njia pana nchini China itafikia yuan bilioni 221.5, soko hilo lina mustakabali mkubwa wa maendeleo. Kutokana na hali hiyo nzuri, China imeweka mkazo katika kuendeleza mawasiliano ya mtandao wa Internet wa njia pana ili kutimiza lengo la kuwa nchi yenye uwezo mkubwa katika sekta ya upashanaji wa habari duniani.

Lakini mtandao wa Internet wa njia pana nchini China si kama tu unakabiliana na fursa za maendeleo, bali pia unakabiliwa na changamoto kubwa na ushindani kati ya nchi mbalimbali duniani. Kuhusu hali hiyo, wataalamu husika wanaona, kufungua mlango huduma za mtandao wa Internet wa njia pana, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na kutimiza hali ya kunufaishana kibiashara ni chaguo moja kizuri. Mkurugenzi wa idara ya sekta za teknoloji za juu katika kamati ya maendeleo ya mageuzi ya taifa ya China Bw. Xu Qin alisema:

"kuifanya sekta ya upashanaji wa habari iwe ya kimataifa ni njia ya pekee kwa maendeleo ya sekta hiyo, uvumbuzi wa China wa kujitegemea unafungua mlango kwa nje. Tunaunga mkono makampuni ya China na ya nchi za nje kuimarisha mawasiliano na ushirikiano katika utafiti wa teknolojia, utungaji wa vigezo na upanuzi wa huduma, ili kutimiza lengo la kunufaishana na kusukuma mbele kwa pamoja maendeleo ya sekta na teknolojia ya mtandao wa Internet wa njia pana duniani."

Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008 itakayofanyika mjini Beijing ni fursa nzuri kubisa na pia changamoto kubwa kabisa zinazoukabili mtandao wa Internet wa njia pana wa China. China imeahidi kuandaa mizhezo ya kwanza ya Olimpiki inayotumia kikamilifu mtandao wa Internet wa njia pana katika historia, na shughuli hiyo pia imechukuliwa kuwa ni sehemu ya mpango wa "Olimpiki ya sayansi na teknolojia" uliotolewa na China. "Michezo ya Olimpiki kwa Internet wa njia pana" inalenga kutumia mtandao wa Internet wa njia pana katika shughuli za kutuma picha, video na data za michezo hiyo, ili kuwapatia kila mtu huduma kamili za mawasiliano zenye ufanisi na usalama katika michezo hiyo.

Kwa mujibu wa kampuni ya NETCOM ya China, hivi sasa kampuni hiyo imeanzisha kazi mbalimbali za maandalizi, zikiwemo kuanzisha huduma za kuunganisha mtandao wa Internet wa njia pana kati ya nchi au sehemu mbalimbali, kujenga mtandao wa njia mbili wa mawasiliano kati ya mabara ya Asia na Ulaya, na kuunganisha kwa mtandao na makampuni zaidi ya mia moja ya huhuma za internet duniani, maandalizi hayo kwa uhakika yataweza kukidhi mahitaji ya mawasiliano katika michezo ya Olimpiki.