Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-06-20 18:52:31    
Hekalu la Jokhang--Fahari ya kabila la Wa-tibet

cri

 

Katika sehemu ya kati kati ya Lahsa, mji mkuu wa mkoa unaojiendesha wa Tibet kuna Hekalu kubwa la Jokhang linalojulikana sana. Hekalu la Jokhang lilijengwa mwanzoni mwa karne ya 7, ni jengo lilojejengwa kwa mbao la mtindo wa makabila ya Wa-han na Wa-tibet wenye historia ndefu kabisa mkoani Tibet. Baada ya kupanuliwa na kufanywa ukarabati kwa mara nyingi, hivi sasa Hekalu la Jokhang limekuwa na eneo la mita za mraba 25000. Jengo kuu la hekalu hilo lina ghorofa tatu, paa la jengo hilo linafunikwa kwa vigae vya rangi ya dhahabu kwa mtindo pekee wa kabila la Wa-tibet, linang'aa chini ya mwangaza wa jua, na kulifanya hekalu hilo lionekane utukufu wake. Naibu mkurugenzi wa kamati ya usimamizi wa Hekalu la Jokhang, ambaye pia ni sufii mkuu wa hekalu hilo Bwana Nimachiren alipozungumzia thamani ya utamaduni na historia ya hekalu hilo alisema:

"Kutokakana na utamaduni wa binadamu duniani, Hekalu la Jokhang ni hekalu adimu lenye thamani kubwa, katika hekalu hilo kuna sanamu ya Buddha Sakyamuni yenye ukubwa unaolingana na kimo chake alipokuwa na umri wa miaka 12, Buddha Sakyamuni alikuwa mwanzilishi wa dini ya kibudha, sanamu hiyo ni adimu sana duniani, waumini wote wa dini ya kibudhaa wanaona sanamu hiyo ni kama budha wa kweli."

Inafahamika kuwa, sanamu hiyo imekuwa na historia ya miaka zaidi ya 2500. Inasemekana kuwa, wakati Budha Sakyamuni alipokuwa hai zilitengenezwa sanamu zake tatu zenye sura za umri tofauti, sanamu iliyohifadhiwa katika Hekalu la Jokhang ni sanamu iliyohifadhiwa vizuri zaidi duniani, hivyo ina thamani kubwa mno. Waumini dini kutoka sehemu mbalimbali wanakwenda Lahsa kufanya hija, wanasema wakiona sanamu hiyo wanahisi kama wamekutana na Budha Sakyamuni mwenyewe.

Hekalu la Jokhang lilijengwa na mtawala wa Tibet Songzain Ganbo katika karne ya 7 katika enzi ya Tang. Songzain Ganbo kwa nyakati tofauti aliwaoa binti Chizun wa mfalme wa Nepal na binti Wencheng wa mfalme wa Tang. Binti wa mfalme wa Nepal na binti Wenchen walipokwenda Tibet kuolewa nao kila mmoja alileta sanamu moja ya Sakyamuni yenye thamani kubwa. Sanamu ya shaba yenye rangi ya dhahabu ambayo ukubwa wake unalingana na kimo cha Sakyamuni alipokuwa na umri wa miaka 12 ililetwa na Binti Wencheng, sanamu hiyo inaonesha hali ya Sakyamuni alipokuwa mwana mfalme, inahifadhiwa katika Hekalu la Jokhang. Na sanamu nyingine ya Budha Sakyamuni ambayo ukubwa wake unalingana na kimo cha budha Sakamuni alipkuwa na umri wa iaka minane inahifadhiwa katika hekalu lingine. Mwongozaji wa utalii wa Hekalu la Jokhang Bi. Li alisema:

"Sanamu hiyo ya Budha Sakyamuni inaonekana ni kubwa zaidi kuliko kimo chake halisi alipokuwa na umri wa miaka 12, kwa sababu waumuni wengi wa dini ya Budha walipaka rangi ya dhahabu halisi kwenye sanamu hiyo."

Licha ya sanamu ya Budha Sakyamuni, katika Hekalu la Jokhang pia kuna sanamu ya mwanzilishi wa hekalu hilo Mtawala Songzain Ganbo. Mioyoni mwa wakazi wa kabila la Wa-tibet, Songzain Ganbo na wake zake wawili wote ni mabuddha, ni waokoaji wao.

Zaidi ya hayo katika Hekalu la Jokhang pia kunahifadhiwa kikamilifu fremu ya mlango iliyotengenezwa kwa mbao za msandali na nguzo za mbao za karne ya 7. Mwongozaji Li alifahamisha kuwa, nguzo moja ya msandali iliyobaki kutoka wakati wa kujenga hekalu hilo imechukuliwa na watu wa kabila la Wa-tibet ni nguzo yenye uwezo wa kuleta bahati nzuri, kila mhujaji anapoigusa kwa mkono na kupaka samli nguzoni, hivyo ndivyo nguzo hiyo inavyoonekana ya ulaini. Jambo la kushangaza zaidi ni kuwa katika nguzo hiyo yamewekwa meno ya binadamu. Mwongozaji Li alisema:

"Waumini wa dini wenye moyo dhati husujudu na kutoa heshima kubwa kwa mabudha kwa kulala kifudifudi kwa miguu na mikono kugusa ardhi kutoka maskani yao hadi Lahsa. Baadhi yao wanatumia muda wa mwaka mmoja hadi miaka misaba kumaliza safari yao ya hija, baadhi yao hata walikufa njiani kutokana na udhaifu na kuugua magonjwa, baadhi ya mahujaji kabla ya kufa njiani waling'oa meno yao yapelekwe mjini Lahsa na wenzao na yaingizwe kwenye nguzo hiyo, kama wao wenyewe wamefika huko kuabudu."

Kila siku Hekalu la Jokhang linajaa mahujaji wanaoabudu Budha. Msichana Qing Qing ameishi mjini Lahsa kwa miaka mitatu, yeye anapenda kutembelea Hekalu la Jokhang pamoja na kamera yake. hisia zake huguswa na vitendo vya waumini dini. Alisema:

"Wanakuja hapa kutoka maskani yao huulala kifudifudi kwa miguu na mikono hugusa ardhi njia nzima. Waumini wengi wa dini wa aina hiyo ni wafugaji, kabla ya kuondoka nyumbani, wafugaji hao huuza mali zao na mifugo yao. Badala ya kuona maumivu, waumini hao wanafurahia safari yao ndefu ya kuabudu Budha bila kujali taabu njiani."