|
Mkutano wa 6 wa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ulifanyika tarehe 19 huko Geneva. Mkutano huo umepitisha mpango wa uundaji wa utaratibu wa baraza hilo jipya na kuthibitisha kanuni mpya za kufanya ukaguzi na mazungumzo baada ya kila muda maalumu. Hii inaonesha kuwa shughuli za haki za binadamu za Umoja wa Mataifa zimeingia katika kipindi kipya.
Moja ya agenda muhimu za mikutano 5 iliyopita ya baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ilikuwa ni kujadili kuhusu kufanya ukaguzi baada ya kila muda maalumu, utaratibu maalumu, wataalamu kujibu maswali pamoja na agenda na kanuni za majadiliano ya baraza hilo. Baada ya majadiliano marefu ya mwaka mmoja, pande mbalimbali zilieleza maoni na mambo yanayofuatilia ,hatimaye mwenyekiti wa kwanza wa baraza la haki za binadamu ambaye ni mwakilishi wa Mexico katika Umoja wa Mataifa, Geneva, Bw. Luis Alfonso de Alba alitoa mpango uliozingatia maoni ya pande mbalimbali.
Mgongano kuhusu uundaji wa utaratibu wa baraza uko katika pande mbili, wa kwanza ni kuhusu suala la kuendelea kubaki au la kwa utaratibu wa kuweka mtu maalumu kutoa ripoti kuhusu haki za binadamu. Nchi nyingi zinazoendelea zinaona, miswada zaidi ya 100 iliyotolewa kuhusu nchi mbalimbali duniani, yote ilizilenga nchi zinazoendelea, ambayo inakwenda kinyume cha lengo lililowekwa kuhusu kuhimiza na kuhakikisha haki za binadamu, miswada hiyo ilikuwa chombo cha kisiasa cha nchi za magharibi kuzibana nchi hizo, hivyo zinataka kuibatilisha, wakati baadhi ya nchi zilizoendelea zinataka kubakia kwa utaratibu huo. Pili, ni njia kamili kuhusu utaratibu wa kufanya ukaguzi baada ya kila muda maalumu, nguvu za kisheria za maazimio husika na ni kutumia au la njia ya upigaji kura. Baadhi ya nchi zinazoendelea ikiwemo China, zinaona, ili kuzuia utoaji taarifa kuhusu hali ya haki za binadamu ya nchi mbalimbali usiwe chombo cha kisiasa, kulenga baadhi ya nchi tu na kutumia vigezo vya aina mbili, utoaji wa taarifa hizo unatakiwa kupitishwa kwa kibali cha zaidi ya theluthi mbili za nchi wanachama.
Toka kufanyika kwa mkutano wa 5 wa baraza la haki za binadamu tarehe 11 mwezi Juni, kumetokea mvutano mkali kuhusu masuala hayo mawili. Washiriki wa mkutano walikuwa na majadiliano makali hadi dakika ya mwisho ya mazungumzo, yaani saa 6 usiku wa tarehe 18 Juni, ambapo washiriki walifikia kwenye maafikiano kuhusu mpango uliotangazwa na mwenyekiti wa baraza hilo Bw. Luis Alfonso de Alba. Kuhusu suala la nchi watoa ripoti, mpango huo umeamua kuwa, muda wa watoa ripoti wa nchi za Cuba na Russia umetimia, hivyo kazi zao zimekwisha. Kazi za nchi nyingine kumi za watoa ripoti zitaendelea hadi kutimiza muda wake wa miaka sita. Kuhusu miswada ya nchi watoa ripoti, mpango mpya unataka miswada yao iungwe mkono na nchi nyingi, na itakuwa vyema zaidi kama itasainiwa na nchi 15 wanachama. Kuhusu utaratibu wa kufanya ukaguzi baada ya kila muda maalumu, mpango huo unataka nchi zote ziwe sawa, na zikaguliwe baada ya kila miaka minne ziwe nchi zilizoendelea au nchi zinazoendelea.
baraza la haki za binadamu liliitisha mkutano wa 6 katika tarehe 19 mwezi Juni, ambapo mpango mpya ulipitishwa kwa kura 46 za ndiyo na kura moja ya kupinga. Kiongozi wa ujumbe wa China Bw. Cheng Jingye akitoa hotuba alisema, ingawa mpango huo siyo mzuri sana, lakini unajitahidi kuonesha maoni ya pande mbalimbali. Maendeleo hayo hayakupatikana kwa urahisi, bali ni matokeo ya jitihada na akili za kisiasa za wawakilishi wa nchi mbalimbali. China inatoa pongezi kwa jitihada za pande mbalimbali. Mbali na hayo, alisema, China inatarajia pande mbalimbali ziendelee kufanya mazungumzo na ushirikiano, kufuata kanuni za kuonesha maoni ya nchi nyingi, haki, ukweli wa mambo na bila ubaguzi ili kutimiza lengo la awali la baraza la haki za binadamu la kuhimiza na kulinda haki za binadamu.
Nchi nyingi zinazoendelea zinasifu na kuunga mkono msimamo wa China wa kushikilia kanuni na kuwa na unyumbufu katika uundaji wa utaratibu wa baraza la haki za binadamu.
|