Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-06-22 17:08:22    
Marekani yaharakisha hatua za kutatua suala la nyuklia la Peninsula ya Korea

cri

Mkuu wa ujumbe wa Marekani wa mazungumzo ya pande sita kuhusu suala la nyuklia la Peninsula ya Korea Bw. Christopher Hill ambaye pia ni msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa Marekani, tarehe 21 alifanya ziara nchini Korea ya Kaskazini, hii ni ziara ya kwanza kwa ofisa mwandamizi wa Marekani kuzuru Korea ya Kaskazini katika muda wa miaka mitano iliyopita. Ziara hiyo ina maana ya kuwa msimamo wa Marekani wa kutofanya mazungumzo ya ana kwa ana na Korea ya Kaskazini umebadilika, na pia imeonesha kuwa Marekani inataka kuharakisha hatua za kutatua suala la nyuklia la Peninsula ya Korea.

Bw. Hill alifanya ziara nchini Korea ya Kusini baada ya kumaliza ziara yake tarehe 18 nchini China, kisha alitembelea Japan kwa siku mbili. Hapo awali kutokana na mpango, tarehe 20 alitakiwa kurudi nchini Marekani, lakini kwa ghafla alibadilisha mpango huo, na tarehe 21 alirudi tena Korea ya Kusini na adhuhuri ya siku hiyo aliondoka Korea ya Kusini kwenda Korea ya Kaskazini.

Katika kipindi wakati Bw. Cliton alipokuwa rais wa Marekani aliwahi kumtuma waziri wa mambo ya nje Bibi Madeleine Albright kufanya ziara nchini Korea ya Kaskazini. Lakini baada ya Bw. Gorge Bush kuwa rais, hakuna ofisa mwandamizi wa Marekani aliyetumwa kuitembelea Korea ya Kaskazini kutokana na sera za kibabe kuhusu Korea ya Kaskazini. Baada ya kufika Pyongyang, mji mkuu wa Korea ya Kaskaizni, Bw. Hill alisema mchakato wa mazungumzo ya pande sita unapaswa kuendelea na kufidia muda uliopotezwa.

Tarehe 13 Februari mwaka huu, mazungumzo ya pande sita yalipitisha waraka wa pamoja wa "mpango wa utekelezaji wa taarifa ya pamoja" yaani "waraka wa tarehe 13 Februari". Waraka huo unahusu kufunga zana za nyuklia, kualika wakaguzi wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki kurudi tena nchini Korea ya Kaskazini na pande mbalimbali zitoe misaada ya nishati kwa Korea ya Kaskazini. Lakini kutokana na kuwa dola za Kimarekani milioni 25 za Korea ya Kaskazini zilizuiliwa katika benki ya Macau, waraka huo haukutekelezwa.

Kutokana na juhudi za pande mbalimbali, tarehe 18 mwezi huu ubalozi wa Korea ya Kaskazini nchini Russia ilitangaza kuwa fedha za Korea ya Kaskazini zilizozuiliwa zimehamishiwa kwenye benki kuu ya Russia. Tarehe 21 vyombo vya habari vya Russia vilithibitisha kuwa fedha hizo za Korea ya Kaskazini zimekabidhiwa kwa Korea ya Kaskazini.

Kabla ya hapo, wizara ya mambo ya nje ya Korea ya Kaskazini iliwahi kutangaza kuwa kama fedha zilizozuiliwa zikiachiliwa, Korea ya Kaskazini itasimamisha shughuli za nyuklia na kuualika ujumbe wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki kutembelea Korea ya Kaskazini, na pia itafanya mazungumzo na Marekani kwa kina kuhusu hatua zitakazofuata baada ya kusimamisha shughuli za nyuklia.

Vyombo vya habari vya Marekani vinafafanua kuwa sababu ya Marekani kutaka kuharakisha hatua za kutatua suala la nyuklia la Peninsula ya Korea ni kwamba, Marekani inakumbwa na matatizo mengi katika sera yake ya mambo ya nje ambayo yanatakiwa kutatuliwa haraka, matatizo hayo yakiwa ni pamoja na matatizo ya Iran na Iraq. Kuhusu suala la Iraq askari wa Marekani wanazidi kuuawa, na Marekani haina uwezo wowote wa kutatua suala hilo. Kuhusu suala la nyuklia la Iran, Marekani inaelewa kwamba haitapata mafanikio yoyote. Katika hali kama hiyo, serikali ya rais Bush ambayo imebaki na mwaka mmoja tu, inataka kuthibitisha kwa wananchi wake kuwa ina uwezo wa kutatua matishio yanayoikabili Marekani angalau moja, tishio hilo ni suala la nyuklia la Peninsula ya Korea. Hii ndio sababu ya Bw. Hill kufanya ziara ya ghafla Korea ya Kaskazini.

Habari zinasema Bw. Hill ana matumaini kuhusu mazungumzo ya pande sita yatakayofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao. Alisema kama Korea ya Kaskazini ikiacha mpango wake wa nyuklia, basi serikali ya Marekani itakubali kuanzisha uhusiano wa kawaida na Korea ya Kaskazini mwishoni mwa mwaka huu.

Lakini kuweza au kutoweza kupata maendeleo katika utatuzi wa suala la nyuklia la Peninsula ya Korea, licha ya kutegemea vitendo vya Korea ya Kaskazini, pia kunategemea jinsi Marekani itakavyorekebisha msimamo wake kwa mujibu wa hali itakavyokuwa.