Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-06-26 15:57:06    
Barua 0624

cri

Msikilizaji wetu Wabwire Antony Namude wa sanduku la posta 32 Nambale Kenya ametuletea barua akisema kuwa, katika shughuli zake za kutembelea marafiki amegundua kwamba Radio China Kimataifa inazidi kupanda ngazi ya sifa kwa namna inavyosikika na kupeperusha matangazo na vipindi vyake.

Baadhi ya wasikilizaji walisema kuwa Radio China Kimataifa inatoa matagnazo ya kina yasiyo na mwegemeo wowote. Tena wasikilizaji wengine husema kuwa Radio China Kimataifa inajali sana bara la Afrika , hii inatokana na wao kuwa na kipindi kinachosimulia masuala ya bara la Afrika kwa ufasaha, hii hufanya matangazo na vipindi kuwa kamilifu kwa msikilizaji kutoka barani Afrika.

Tunamshukuru sana Bwana Wabwire Antony Namude kwa barua yake ya kutuelezea maoni ya wasikilizaji wetu kuhusu vipindi vyetu, hayo yanatutia moyo sana na kutuhimiza tuchape kazi zaidi.

Msikilizaji wetu Misian A. Anari Msanii wa S.L P 1246 Kisii nchini Kenya ametuletea barua akisema, katika mwaka huu wa 2007 atazidisha na kuboresha zaidi mawasiliano yake na Radio China Kimataifa baada ya kipindi cha mwaka mmoja.

Bwana Anari anasema pamoja na kwamba mwaka uliopita hakuwasiliana na radio china Kimataifa haina maana kwamba alikuwa hafuatilii matangazo ya CRI,sababu hasa iliyomfanya kushindwa kuwasiliana na Radio china Kimataifa ni kutingwa na shughuli za masomo ambapo mwaka jana ulikuwa mwaka wake wa mwisho wa kumaliza elimu ya sekondari.

Hivyo kama mwaka huu atatumiwa bahasha ambazo zimeshalipiwa ataandika barua nyingi na kuijulisha mengi Idhaa ya Kiswahili ya radio China Kimataifa kuhusu utamaduni wa Kenya hasa wa Kisii.

Bwana Anari anaomba wanachama wapya wafuatao watumiwe bahasha, kalenda na kadi za salamu:

Jackline M. Mongare, Lilian K. Nzangaresi, Anari Albert, Zippora Anari, Ezra Mongare, Joel Albert, Albert Misiani, Joel Misiani, Alberto Misiani, Justine N Anari, Abner Anari, Zilpah Anari, Sina Anari, na Joel Anari walioko Kisii Kenya.

Msikilizaji wetu Stephen Magoye Kumalija wa sanduku la posta 1067 Kahama Shinyanga Tanzania ametuletea barua akisema, ni matumaini yake makubwa wafanyakazi wote wa Radio China Kimataifa tu wazima, anapenda kutumia fursa hii kumpongeza mtangazaji wa miaka mingi wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio China Kimataifa mama Chen ambapo hapo awali tuliambiwa kuwa angestaafu mapema mwaka jana, lakini ameamuliwa kuahirisha muda wa kustaafu, na ataendelea kutuletea habari motomoto na nyeti kutoka hapa Radio China Kimataifa.

Msikilizaji wetu huyo anasema, amefurahi mno kusikia kuwa mama Chen ataendelea kuwasomea barua za wasikilizaji zikiwa na maoni mbalimbali katika kipindi cha sanduku la barua.

Mwisho anapenda kutuma salamu zake kwa watangazaji wa kipindi cha sanduku la barua, mama Chen pamoja na Fadhili Mpunji wa Radio China Kimataifa.

Msikilizaji wetu Stephen Lwitiko Noel wa sanduku la posta 11 Mpwapwa Dodoma Tanzania ametuletea shairi aliloandika linaloitwa: Hongera Radio China Kimataifa. Shairi hilo linasema hivi:

Steven Noel naja, Radioni andikia

Mengi nitawaeleza, hakika yatawafaa

Radio inaongoza, Kuonya yasiyofaa

Hongera Radio China Kimataifa inaongoza

Tokea ilipoanza, Mengi imetuletea

Ni mengi imetufunza, Uelewa tumepata

Na urafiki umekua, daraja tumepata

Hongera Radio China Kimataifa inaongoza

Iko mstari wa mbele, habari katupatia

Ya enzi iliyopita, tuweza kuyaelewa

Stephen naye pita, nao bila sahauliwa

Hongera Radio China Kimataifa inaongoza

Ukipata kitumie ukikosa kijutie

Yatupasa tutulie, radio tuipokee

Ya ndani tusikie, ya nje tuyaelewe

Hongera Radio China Kimataifa inaoongoza

Wahusika radioni, shukrani zangu pokea

Kwa habari na shairi, hakika mwapangilia

Mapambo pia mapishi kweli yanafaa sana

Hongera Radio China Kimataifa inaongoza

Namalizia kusema, kwa kumuwomba Rabana

Kituo kipe salama, wasiingie wafitina

Tanzania na China tuzidi kushirikiana

Hongera Radio China Kimataifa inaongoza

Msikilizaji wetu mwingine Bw.Julias Tocta Ngoja wa kanisa katoliki-Reha sanduku la posta 129 Kilimanjaro Tanzania anaanza barua yake kwa salamu nyingi sana kwa wafanyakazi wote wa Radio China Kimataifa,na ansema yeye na wenzake pia ni wazima kabisa na wanaendelea kusikiliza Radio China Kimataifa.Kuhusu historia fupi ya huko kwao anasema yeye anaishi katika tarafa ya Tarakae wilaya ya Rombo.Anaishi chini ya mlima Kilimanjaro ambako kunapatikana kabila la wachaga.

Anaendelea kusema kuwa mazao yanayolima ni ya chakula na biashara.Mazao hayo ni pamoja na kahawa,ndizi, mahindi, maharage,ulezi,viazi,mihogo na magimbi.matunda wanayolima ni pamoja na maembe,maparachichi,mananasi,machungwa na mapapai.Na mlima unaojulikana kwa urefu kuliko yote katika bara la Afrika ni mlima Kilimanjaro.Kwa upande wa elimu anasema mkoa wa Kilimanjaro unaongoza nchini Tanzania kwa kuwa na shule nyingi za sekondari.Huduma nyingine kama vile simu na umeme zinaendelea kusambazwa. Pia barabara zinaendelea kujengwa ikiwemo ile inayoelekea mpakani mwa Kenya(Tarakea ? Kamwanga) inayojengwa na kampuni ya China inayoitwa SIETCO.

Anasema yeye binafsi anafurahi kuwaona hao wachina kila siku huko Tarakea kwani huwa wanawauzia vitu mbali mbali.Kuhusu Radio China Kimataifa anasema yeye amekuwa msikilizaji kwa muda mrefu na alipofanikiwa kuwasiliana na Radio China Kimataifa alifurahi sana.Ndipo alipoanza kuchukua hatua ya kuitangaza Radio China Kimataifa huko kwao.

Anasema kwa sasa huko kwao wasikilizaji ni wengi sana na wale ambao wameshaweza kuwasiliana na Radio China Kimataifa ni hawa wafuatao: Jonsia Karani,Latino Rogasiani,Joseph Feto,Julias Joseph,Julias Faustin Innocent Gaudence,Priska Julias,Hilaria Festo James Julias,Gasto Shayo,Janet Julias,Godfrey Bazili,Felichismi Vitalis,Filimon Luka,Kenedi William,Petro Erasmi na Mariana Jenes.Anasema wote hawa wanatumia sanduku la posta 129 Tarakea hukutana katika kanisa katoliki Reha.

Kwa upande wa vipindi vya Radio China Kimataifa anasema kwa sababu ya kusikiliza vipindi vya Radio China Kimataifa ameshapata faida kubwa sana kwani ameshajifunza mambo mengi kuhusu china.ombi lake kwetu anaomba zawadi yoyote yenye nembo ya Radio China Kimataifa ili anapotembelea huko kwao aweze kitangaza vyema zaidi Radio China Kimataifa.Mwisho anasema hana mengi kwa leo ila tu ni kututakia kazi njema.

Tunawashukuru wasikilizaji wetu Stephen Magoye Kumalija, Stephen Lwitiko Noel, na Julias Tocta Ngoja kwa barua zao na maoni yao kuhusu matangazo yetu. Ni matumaini yetu kuwa tutadumisha mawasiliano na urafiki kati yetu.

Idhaa ya kiswahili 2007-06-26