Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-06-27 14:48:50    
Sayansi na teknolojia mpya zakaribia maisha ya watu

cri

Roboti inayoweza kupika chakula, msala unaojisafisha kwa kutumia lita moja ya maji, ubao wa kuandikia wa kitarakimu ambao unaweza kuonesha maandishi na michoro moja kwa moja kwenye kompyuta, teknolojia hizo zote zimeoneshwa kwenye maonesho ya bidhaa za teknolojia ya Beijing, China.

Kwenye majumbe ya maonesho hayo, roboti inayoweza kupika chakula iliwavutia watazamaji wengi. Mtoa maelezo Bi. Chen Fang alisema, ukiweka mbogo kwenye kikaango au kijisanduku maalum, roboti hiyo inaweza kupika mwenyewe kwa kufuata programu zilizowekwa kwenye kompyuta yake. Kama ukiitaka iweze kupika kwa kufuata mapishi yako, pia unaweza kuagiza programu kuhusu njia ya kupika na aina za vitambato vinavyotiwa kwenye chakula. Hivi sasa, roboti hiyo inaweza kupika vyakula vya aina zaidi ya mia moja. Bi. Chen Fang alisema:

"orodha ya mapishi ya vyakula imewekwa kwenye kompyuta yake, unachagua chakula unachotaka tu na kuweka mbogo na vitambato katika roboti, itapika mwenyewe."

Bi. Chen Fang alisema, ni rahisi sana kuendesha roboti hiyo, kwa kawaida, nyama inapikwa kwa dakika 7 au 8 na kwa mboga za majani, dakika tatu zinatosha.

Bw. Zheng Hong baada ya kusikiliza maelezo hayo, alishangaa sana akisema:

"sikuwahi kusikia tenolojia hiyo, kwa kweli inarahisisha maisha ya watu na kuwakomboa kutoka kwenye kazi mbalimbali. Zamani kazi hizo lazima zifanywe na watu lakini hivi sasa roboti zinaweza kuzifanya, inaleta manufaa hasa kwa wafanyakazi vijana."

Ndiyo kama Bw. Zheng Hong alivyosema, maendeleo ya sayansi na teknolojia yameleta mabadiliko makubwa kwa maisha ya binadamu. Mambo mengi ambayo hata hayakufikiriwa zamani hivi sasa yametokea kwenye maisha halisi. Bw. Zheng Hong alionesha matumani kuwa iko siku vyombo vinavyooneshwa kwenye maonesho hayo vitaweza kutumiwa nyumani kwake.

Maonesho hayo yana majumba 10, bidhaa zilizooneshwa ni pamoja na vifaa na teknolojia husika za michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008, bidhaa hizo zimewavutia watazamaji wengi. Maonesho hayo pia yamekusanya bidhaa nyingi zinazohusika na maisha ya watu. Mtazamaji Bw. Cheng Peng alisema, alitembelea majumba kadhaa, na bidhaa zinazomvutia zaidi ni zile zinazohusiana na maisha ya watu.

Katika jumba jingine, mwandishi wetu wa habari aliona mwelezaji akiwafahamisha watazamaji kuhusu ubao wa kitarakimu wa kuchora. Ubao huo unaonekana kama ni ubao mweupe wa kawaida wa kuchora pamoja na kalamu. Bw. Lu Haoqian wa kampuni ya teknolojia ya Hanwang iliyosanifu ubao huo alieleza kuwa, ubao huo unasanifiwa kwa ajili ya watu wanaopenda kuchora kwa kutumia kompyuta, na ukiunganishwa kwenye kompyuta, michora inaweza kuoneshwa mara moja kwenye srini ya kompyuta. Bw. Lu Haoqian alisema:

"kalamu hiyo haiunganishwi na ubao kwa waya, inachora kutokana na kuathiriana kati ya umeme na usumaku."

Watazamaji wengi walikuwa na hamu kubwa ya kujaribu ubao huo. Mzee Wei Gang mwenye umri wa miaka 65 alisema:

"naona hii ni nzuri, zamani ukichora kwa kutumia mouse, si rahisi kuidhibiti vizuri. Lakini kutumia kalamu ni rahisi zaidi. Ninapenda kuchora, pia nafuatilia teknolojia ya juu. Natembelea maonesho hayo kila mwaka. Mwaka huu kuna bidhaa nyingi zaidi za teknolojia ya juu na zenye uvumbuzi."

Tukizungumzia uvumbuzi, hatuwezi kuacha eneo la sayansi na teknolojia la Zhongguancun linalolenga kufanya uvumbuzi kwa kujitegemea. Hii ni mara ya tisa kwa eneo hilo kushiriki kwenye maonesho hayo, bidhaa zaidi ya elfu moja zilizotolewa na makampuni zaidi ya 140 ya eneo hilo zilioneshwa kwenye maonesho hayo. Bidhaa nyingi ni zenye teknolojia muhimu na nguvu ya ushindani duniani.

Kampuni ya teknoljia ya Zhongchuangqingfeng ya Beijing ni mojawapo kati ya makampuni ya eneo hilo. Maneja mkuu wa kampuni hiyo Bw. Yang Wenming alimfahamisha mwandishi wetu wa habari kuhusu mashine ya kuangamiza vijidudu. Alisema, mashine hiyo inaweza kuangamiza vijidudu kwenye chumba kwa mionzi ya ultraviolet, lakini mionzi hiyo inadhibitiwa ndani ya mashine hiyo, haitadhuru afya ya binadamu. Bw. Yang Wenming alisema, mashine hiyo inawasaidia watu kukinga na magonjwa ya kuambukiza. Alisema:

"mashine hiyo ilisanifiwa na kampuni yetu kwa kujitegemea, ni bidhaa iliyovumbuliwa nchini China, sisi tuna hakimiliki ya ubunifu."