Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-06-27 15:14:22    
Mapishi ya supu ya tufaha na nyama nofu

cri

Mahitaji:

Tufaha moja, nyama nofu gramu 50, karoti moja, tende gramu 10, uyoga mweupe gramu 10, chumvi kijiko kimoja

Njia:

1. kata nyama nofu iwe vipandevipande, ondoa punje ya tufaha na kata tufaha iwe vipande, kata karoti iwe vipande vipande.

2. washa moto, tia mafuta kidogo kwenye sufuria, halafu tia vipande vya nyama nofu, korogakoroga, vipakue.

3. washa moto tena, mimina maji bakuli 6 kwenye sufuria, tia vipande vya nyama nofu, tufaha, karoti na tende kwenye sufuria, korogakoroga, baada ya kuchemka punguza moto, iendelee kuchemka, baada ya dakika 10, tia uyoga mweupe, endelee kuchemsha kwa dakika 20. tia chumvi, halafu ipakue. Mpaka hapo supu hiyo iko tayari kuwakunywa.