"Ripoti ya mabadiliko ya hali ya hewa ya mwaka 2007" iliyotolewa tarehe 28 Juni na Umoja wa Mataifa inasema kuwa, nchi zenye nguvu dhaifu kabisa duniani hutoa hewa chache kabisa zinazosababisha kuongezeka kwa joto duniani, lakini nchi hizo zinakabiliwa na athari mbaya kubwa kabisa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Ripoti hiyo inatoa mwito wa kuitaka jumuiya ya kimataifa kuzisaida nchi hizo kuongeza uwezo wa kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa duniani.
Kwa mujibu wa vigezo vya Umoja wa Mataifa, nchi ambazo wastani wa mapato ya kila mtu ni chini ya dola za kimarekani 750, nchi zilizoko ndani ya sehemu za bara ambazo hazina milango ya kuelekea baharini, hivyo maendeleo yake ya uchumi yanakwamishwa vibaya, pamoja na nchi zilizoko pembezoni za visiwa vidogo zenye ukosefu mkubwa wa maliasili, zote hizo ni nchi ambazo ziko nyuma kabisa kimaendeleo. Hivi sasa duniani kuna nchi 86 kama hizo ambazo zina uwezo dhaifu kabisa wa kiuchumi, lakini nchi hizo zinaathirika moja kwa moja na mabadiliko ya hali ya hewa. Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa tarehe 28 Juni imethibitisha kuwa, asilimia 90 ya sababu zinazosababisha kuongezeka kwa joto duniani zinatokana na binadamu kutoa hewa nyingi ya carbon dioxide.
Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa imeonesha kuwa, katika utoaji wa hewa zinazosababisha kuongezeka kwa joto duniani, utoaji wa hewa wa Marekani ulichukua asilimia 22.5, utoaji wa Ulaya unachukua asilimia 24.7, na wa nchi zilizoko nyuma kimaendeleo na nchi zinazoendelea za visiwa vidogovidogo ulichukua asilimia 0.02 tu. Lakini nchi hizo zinakabiliwa moja kwa moja athari mbaya ya mabadiliko ya hali ya hewa.
Mabadiliko ya hali ya hewa yamesababisha kuinuka kwa usawa wa bahari, pia kusababisha kuongezeka kwa maafa ya ukame na mafuriko, na uharibifu unaosababishwa na maafa hayo kwa nchi zilizoko nyuma kabisa kimaendeleo, ambapo miundo mbinu inaharibiwa, shughuli za uvuvi kwenye bahari ya karibu zimepata hasara, na ardhi zimeongezeka kuwa na chumvi na zinatishia usalama wa chakula. Aidha maambukizi ya magonjwa ya yanayoambukizwa kwa njia ya maji yanaongezeka, na shughuli za utalii pia zinaathiriwa.
Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya nchi zilizoko nyuma kabisa kimaendeleo, nchi zinazoendelea zilizoko ndani ya bara na nchi zinazoendelea za visiwa vidogovidogo Bwana Anwarul Chowdhury alidhihirisha kwenye Mkutano na waandishi wa habari kuwa, kama hatua hazitachukuliwa kwa wakati, visiwa kadhaa vitazama, ambapo mamia ya watu na maelfu ya familia watapoteza makazi yao, hata visiwa kadhaa vitamezwa kabisa na maji. Bwana Chowdhury alisema mwaka 2004, sehemu ya Caribbean ilikumbwa na maafa makubwa ya kimaumbile, baada ya hapo, Umoja wa Mataifa uliusaidia Umoja wa Caribbean na Benki ya dunia kuanzisha mfuko wa kuokoa watu waliokumbwa na maafa ya Caribbean, mfuko huo ulizinduliwa mapema mwaka huu ili kukabiliana na majira ya kimbunga. Alisema, huu ni mfano mzuri wa kuigwa, na hivi sasa Umoja wa Mataifa unajitahidi kuzihimiza nchi za Asia na Pasifiki zianzishe mfuko kama huo.
Bwana Chowdhury alisema, kwenye Mikutano ya Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa itakayofanyika mwezi Septemba na mwezi Desemba mwaka huu, pamoja na mazungumzo kuhusu kufikia mpango mpya wa kupunguza utoaji wa hewa za carbon dioxide baada ya kukamilisha majukumu yaliyowekwa kwenye "Makubaliano ya Kyoto" kabla ya mwaka 2012, namna ya kuweka mkazo zaidi wa ufuatiliaji kwa nchi zilizoko nyuma kabisa kimaendeleo na nchi zinazoendelea za visiwa vidogovidogo, ni muhimu sana kuzisaidia nchi hizo zichukue hatua zenye ufanisi.
Bwana Chowdhury alisema, kutokana na kuwa nchi hizo hazina uwezo wa kutunga mipango ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, hivi sasa Umoja wa Mataifa unazisaidia kutunga mikakati husika na mpango wa utekelezaji kwa nchi, juhudi hizo zinasaidiwa na Mfuko wa mazingira ya dunia nzima na Mfuko wa nchi zilizoko nyuma kabisa kimaendeleo, lakini hayo yote bado hayatoshi, nchi zilizoko nyuma kabisa kimaendeleo na nchi za visiwa vidogovidogo zinahitaji kujenga uwezo, ujenzi huo unatahitaji misaada mingi zaidi ya jumuiya ya kimataifa.
|