Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-06-29 19:50:43    
Benki ya China yapata mafanikio barani Afrika

cri

Miaka kumi iliyopita, benki ya China ilifungua tawi lake huko Lusaka, mji mkuu wa Zambia, na kuwa tawi la kwanza la benki ya China barani Afrika. Lakini kutokana na shughuli za kiuchumi za Zambia siyo nyingi na kutokuwepo kwa mazingira mazuri ya biashara, kabla ya mwaka 2003 benki hiyo iliendeshwa kwa hasara. Lakini benki hiyo iliendelea kuwepo katika mazingira magumu na kujiendeleza. Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na uhusiano kati ya China na Zambia kuzidi kuimarika siku hadi siku, na ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kwa nchi hizo kuongezeka zaidi, benki ya China nchini Zambia imekuwa inafanya uvumbuzi na kupata maendeleo, na kazi zake mbalimbali zimepata mafanikio makubwa.

Ingawa benki hiyo ina tawi moja tu nchini Zambia ambalo lina wafanyakazi wachina na wazambia 13 tu, pia linakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka katika benki za Citibank, Standard Chartered na benki nyingine zilizowekezwa na wageni. Katika miaka mitatu iliyopita, thamani ya mitaji ya benki hii ilichukua nafasi ya nane kati ya benki 13 zilizopo nchini Zambia, na kuwa benki yenye nguvu kubwa ya maendeleo katika soko la fedha la Zambia.

Takwimu zifuatazo zinaonesha kidhahiri hali ya maendeleo ya benki ya China nchini Zambia katika miaka ya hivi karibuni: mwaka 2003 benki hiyo ilipata hasara ya dola za kimarekani laki 1.07; mwaka 2004 ilipata faida ya dola za kimarekani elfu 12; mwaka 2005 faida yake iliongezeka mara 10 kuliko mwaka uliopita, na kufikia dola za kimarekani laki 1.3; mwaka 2006 faida iliongezeka na kuwa dola za kimarekani milioni 1.02. mwishoni mwa mwaka 2006, thamani ya mitaji ya benki hii ilifikia zaidi ya dola za kimarekani milioni 90 ikilinganishwa na thamani ya mwaka 2003, iliyokuwa dola za kimarekani milioni 12. Hali hii ya mabadiliko ya benki ya China nchini Zambia inatokana na kuimarika kwa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Zambia, na pia inathibitisha kuwa wafanyakazi wa benki hii wana ujasiri wa kuiendeleza benki hiyo kwa mbinu mpya.

Idara ya biashara ya ubalozi wa China nchini Zambia imefahamisha kuwa, hadi sasa makampuni 200 yenye mitaji ya China yanafanya shughuli nchini Zambia, ambayo yamewekeza katika sekta za uchimbaji wa madini, nguo, kilimo, ujenzi, mawasiliano ya habari, matibabu na mikahawa. Thamani ya jumla ya uwekezaji katika mikataba imefikia zaidi ya dola za kimarekani milioni 525. China imekuwa nchi ya tatu iliyowekeza kwa wingi nchini Zambia, baada ya Afrika ya Kusini na Uingereza. Aidha, katika miaka ya karibuni biashara kati ya China na Zambia pia imekuwa ikiongezeka kwa kasi.

Kutokana na hali hiyo, benki ya China nchini Zambia inatumia nafasi hii, kujiendeleza kwa njia mpya, ili kupanua shughuli zake siku hadi siku, na faida zake zimekuwa zinaongezeka mwaka hadi mwaka. Baada ya kufanya uchunguzi kuhusu soko, benki hiyo imegundua sehemu muhimu ya kuendeleza shughuli zake, yaani kutegemea maendeleo ya uchumi na biashara kati ya China na Zambia, kufanya shughuli zake hasa katika mashirika yaliyowekezwa na wachina. Kutokana na juhudi zake, benki hiyo inaweza kumudu ushindani kwenye soko la fedha la nchi hiyo na kupata mafanikio.

Wafanyakazi wa benki ya China nchini Zambia, wanafanya juhudi kutafuta njia mpya kwa shughuli za benki hiyo, kutoa huduma za aina mpya, kujitahidi kupata wateja wapya na kutoa kipaumbele katika kuendeleza shughuli zake siku zote. Wakati huo huo, benki hii imeongeza aina ya huduma zake, kuinua sifa ya huduma na kufanya mipango mbalimbali kwa mujibu wa mahitaji ya wateja tofauti. Kutokana na juhudi za wafanyakazi wote, benki hiyo sio tu imeongeza wateja wake kutoka katika makampuni yaliyowekezwa na wachina, bali pia imepata wateja wapya wa nchi hiyo. Miaka mitatu iliyopita, benki ya China nchini Zambia ilianzisha shughuli zake katika malipo ya kimataifa, malipo ya kibiashara na shughuli za uuzaji wa rejareja, shughuli za wakala wa benki hiyo zimeendelezwa sana, na huduma zake nzuri zinasifiwa na wateja wake wa makampuni yaliyowekezwa na wachina nchini humo.

Aidha, benki ya China nchini Zambia inashirikiana na matawi mengine ya benki ya China katika nchi nyingine ili kusaidiana. Mwaka 2006, benki ya China nchini Zambia ilifungua akaunti za dola za Marekani na Randi ya Afrika ya Kusini katika tawi la Jorhannesburg nchini Afrika ya Kusini, ili kutoa huduma ya fedha hizo kwa wateja wake wa Zambia. Kitendo hicho kinaonesha kuwa, shughuli za tawi la Jorhannesburg la benki ya China zimeingia nchini Zambia, sio tu kuleta manufaa kwa benki hizo mbili, bali pia kutoa urahisi kwa makampuni na kukidhi mahitaji ya wateja wao.

Mkuu wa benki ya China nchini Zambia Bw. Du Qiang alisema mafanikio ya benki hiyo katika miaka ya karibuni yamepatikana kutokana na ushirikiano mzuri na moyo ya kujitolea wa wafanyakazi wote. Alisema kwenye nchi kadhaa za Afrika hakuna usalama wa kutosha na kuna magonjwa mengi, mazingira ya maisha na kazi hayaridhishi, lakini wafanyakazi wanaona kuwa wanapaswa kupiga hatua kubwa kusonga mbele, kufanya juhudi ili kutimiza lengo la Benki ya China "kutafuta ufanisi mkubwa, na kuijenga benki hiyo iwe ya kiwango cha juu duniani".

Kukumbusha hali ya miaka kumi iliyopita, benki ya China nchini Zambia ilifanya mageuzi makubwa na kupata mfanikio katika bara la Afrika ambalo lina fursa nyingi. Mkuu wa benki kuu ya Zambia Bw. Caleb Fundanga alitoa pongezi kwa benki ya China nchini Zambia kuadhimisha miaka 10 tangu ifungue tawi lake nchini Zambia, baada ya juhudi za miaka kumi, Benki ya China sasa imejikita nchini Zambia. Ni matumaini yetu kuwa benki hiyo itapata mafanikio makubwa zaidi nchini humo.