Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-07-03 15:00:37    
Hong Kong yaendelea kuwa sehemu yenye uchumi wa soko huria kabisa duniani

cri

Hongkong ni bandari huria maarufu duniani, pia ni moja ya sehemu zinazopata mafanikio duniani katika kutekeleza uchumi wa soko huria. Kwa mujibu wa Sheria ya Kimsingi, baada ya kurudi China, Hongkong inaendelea kutekeleza mfumo wa uchumi wa soko huria wa kibepari. Katika miaka 10 iliyopita, kutokana na msingi wa sera ya "nchi moja mifumo miwili", Hongkong imeendelea kuwa sehemu yenye uchumi wa soko huria kabisa duniani.

Kwa upande wa kaskazini Hong Kong inapakana na sehemu za ndani za China, kusini ni jirani ya nchi za kusini mashariki ya Asia, mashariki inakaribiana na bahari ya Pasifiki, na inaungana na bahari ya Hindi kwa upande wa magharibi. Hivyo Hong Kong ni bandari muhimu ya usambazaji wa bidhaa kati ya sehemu za Amerika na sehemu za kusini mashariki ya Asia, pia ni sehemu muhimu kwa nchi za Ulaya na Amerika, Japan na nchi za kusini mashariki ya Asia kuingia katika soko la China bara.

Kuanzia mwaka 1841, Hongkong ilianzisha bandari na kutekeleza sera ya bandari huria, yaani bandari inayoruhusu bidhaa kuingia na kuuzwa nje kwa uhuru bila kutoza ushuru wa forodha. Sera hiyo inawavutia wafanyabiashara na bidhaa kutoka sehemu mbalimbali duniani kuingia mkoani Hongkong, pia ilihimiza mawasiliano ya kiuchumi na kibiashara kati ya sehemu za ndani za China na sehemu mbalimbali duniani. Mjumbe wa kudumu wa bunge la umma la China Bw. Tsang Hin-Chi, ambaye pia ni mwanaviwanda mashuhuri wa Hongkong alisema,

"Baada ya China kuanza kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango, uchumi wake umepata maendeleo makubwa, na bidhaa nyingi zinasambazwa katika sehemu mbalimbali duniani kupitia Hongkong."

Kutokana na kuwa na sera ya bandari huria, Hongkong siku zote inatekeleza mfumo wa uchumi wa soko huria. Kuchukua uhuru wa kuendeleza viwanda kwa mfano, mtu yeyote anaweza kuanzisha kampuni huko Hong Kong. Serikali haiingilii kati mambo yoyote ya viwanda, bali inaendeleza shughuli chache za umma, kama vile posta, maji ya kunywa na uwanja wa ndege.

Katika upande wa uhuru wa mambo ya fedha, fedha zinaweza kubadilishwa kwa uhuru, na dhahabu zinaweza kununuliwa na kuuzwa kwa uhuru. Sera ya fedha ya Hongkong inavutia mitaji kutoka sehemu mbalimbali duniani, na hivyo kuifanya Hongkong kama kisiwa cha hazina. Kuna msemo unaosema kuwa benki ni nyingi kuliko maduka ya mchele huko Hongkong. Katika utaratibu wa utozaji kodi, Hongkong inatekeleza utaratibu wa kodi nafuu, kila mwaka jumla ya kodi ni chini ya asilimia 10 ya thamani ya uzalishaji mali kwa mwaka.

Baada ya kurudi China, sera ya uchumi wa soko huria ya Hongkong haijabadilika. Sheria ya Kimsingi ya Hongkong inasema: mkoa wa utawala maalumu wa Hongkong unaendelea kuwa bandari huria, isipokuwa hali zinazowekwa katika sheria, haitozi ushuru wa forodha; inatekeleza sera ya biashara huria, na kuhakikisha uhuru wa mzunguko wa bidhaa, mali zisizoonekana na mitaji. Naibu mkuu wa idara ya maendeleo ya biashara ya Hongkong Bw. Alan Wong alisema:

"Hong Kong siku zote inategemea mfumo wa uchumi wa soko huria, na kutokana na mfumo huo tunaweza kupata maendeleo. Ni rashisi kwa Hong Kong kutambua hali katika upande huo."

Tukichukulia mfano wa uhuru wa kuendeleza viwanda, Hong Kong inafungua mlango katika uwekezaji mkoani humo, hakuna vizuizi kwa mitaji kutoka nje. Ukitaka kuanzisha kampuni mpya huko Hong Kong, kwa wastani inahitaji siku 11 tu za kazi. Baadhi ya viwanda na makampuni yaliyohamishiwa nje ya Hong Kong wakati Hong Kong iliporudi China, mengi yamerudi tena Hong Kong. Katika miaka 10 iliyopita baada ya kurudi China, Hongkong bado ni "kituo cha kimkakati" cha wawekezaji wa kigeni kama vile Marekani na Japan kusimamia mambo yao ya kikanda. Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2006, makao makuu na ofisi ya kikanda ya makampuni ya sehemu mbalimbali za China na ya nchi za nje huko Hongkong yalizidi 6,300.

Katika uhuru wa mambo ya fedha, Hong Kong bado ni kituo cha fedha duniani. Muda mfupi baada ya Hong Kong kurudi China, mgogoro wa fedha barani Asia uliikumba Hongkong, katikati ya mwezi Julai mwaka 1997 hadi mwezi Agosti mwaka 1998, walanguzi wa kimataifa walivamia soko la hisa na soko la fedha za kigeni la Hong Kong, na serikali ya Hong Kong ambayo ilikuwa inatekeleza sera ya kutoingilia kati mambo ya sokoni ilitumia akiba ya fedha za kigeni "kwenye soko", na kufanikiwa kuwashinda walanguzi hao. Baadhi ya watu waliona kuwa, hii inaonesha kuwa serikali ya Hong Kong haitatekeleza uchumi wa soko huria, lakini mkuu wa idara ya usimamizi wa fedha ya Hongkong Bw. Joseph. Yam alikuwa na maoni tofauti:

"Hakika soko huria ni zuri. Lakini uzoefu wetu wa kukabiliana na mgogoro wa fedha barani Asia uliotokea mwaka 1997 hadi 1998 ni kuwa, soko huria pia linaweza kuwa ni soko linalodhibitiwa kwa uhuru, hivyo katika usimamizi, pia inahitaji kufuatilia tahadhari masoko ya hayo, kama yanadhibitiwa, basi inapaswa kuchukua hatua, ni lazima kufuata sheria ya soko."

Bw. Joseph Yam alisema, sio rahisi kutafuta uwiano kati ya usimamizi na uhuru, na kila uamuzi unaotolewa na idara ya usimamizi unachukuliwa kwa tahadhari, ili kutotoa shinikizo kwa viwanda, na kufanya majadiliano na watu wa soko. Kwa ujumla, kiwango cha usimamizi na uingiliaji wa serikali ya Hong Kong kwa shughuli za utoaji huduma wa fedha ni wa chini na utaratibu wa usimamizi ni wa wazi.

Ofisa mkuu wa mkoa wa utawala maalumu wa Hongkong Bw. Donald Tsang alisema, Hong Kong kurudi China hakuathiri uhuru wa uchumi wa Hong Kong:

"Uhuru tunaopenda, sheria tunayozingatia, jamii yenye haki na mzunguko wa fedha, mambo hayo katika miaka 10 hayakudhoofisha, bali yameimarishwa."

Baada ya Hong Kong kurudi China, katika mwongozo wa Sheria ya Kimsingi ya Hong Kong, sera ya bandari huria haibadiliki, na Hong Kong bado inatekeleza mfumo wa uchumi wa soko huria. Sasa Hong Kong inayozidi kustawi imesimama kidete, na katika siku za mbele Hong Kong itaendelea kuwa bandari huria.

Idhaa ya kiswahili 2007-07-03