Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-07-05 15:09:09    
China yatoa mafunzo kwa makada wanawake wa sehemu ya magharibi

cri

Shirikisho kuu la wanawake la China mwezi Mei mwaka huu lilifanya semina ya wiki moja iliyowashirikisha makada wanawake 170 wa mashirikisho ya wanawake ya ngazi ya wilaya kutoka mikoa kumi ya magharibi mwa China.

Naibu spika wa bunge la umma la China, ambaye pia ni mwenyekiti wa shirikisho kuu la wanawake la China Bi. Gu Xiulian alipokutana na makada wanawake hao aliwataka wafuate maagizo yaliyotolewa na kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China, kutekeleza wazo la kujiendeleza kwa njia ya kisayansi, kuimarisha ujenzi wa uwezo wao, na kuwahimiza makada wanawake kuwaongoza vizuri kina mama kutoa mchango mpya katika shughuli za kuendeleza sehemu ya magharibi, ujenzi wa vijiji vya aina mpya na jamii yenye masikilizano kwa kufuata fikra na hatua za kufanya uvumbuzi ili kuleta maendeleo mapya.

Hii ni semina ya 12 kwa makada wanawake wa ngazi ya wilaya nchini China. Wana semina walipitia ripoti ya "kuimarisha ujenzi wa sheria ya kidemokrasia ya kijamii na kukamilisha mfumo wa sheria wa kuhakikisha haki na maslahi ya wanawake" na "kupanga na kuhimiza kazi ya kuendeleza shughuli za wanawake kutokana na wazo la kujiendeleza kwa njia za kisayansi".

Wana semina hao walieleza kuwa, watafuata na kutekeleza wazo la kujiendeleza kwa njia ya kisayansi, kuongeza uwezo wao wa kuwaongoza kina mama kujiendeleza, kuwashirikisha wanawake kujenga maskani mazuri ya sehemu ya magharibi, ili kutoa mchango mpya katika kujenga vijiji vya aina mpya na jamii yenye masikilizano.

Inasemekana kuwa katika miaka ya karibuni, shirikisho kuu la wanawake limeweka mkazo kutekeleza mpango wa kutoa mafunzo wa "5123", yaani katika kipindi cha kumi na moja cha miaka mitano itatoa mafunzo kwa wanawake elfu 50 kuhusu namna ya kuendesha shughuli, kutoa mafunzo ya kazi za ufundi kwa mawakala elfu 10 wa wakulima wanawake, kutoa mafunzo kwa makada wanawake elfu 20 waliohamishwa kazi, na kutoa mafunzo kwa makada wanawake zaidi ya 3000 wanaoshughulikia mambo ya wanawake na watoto katika ngazi ya wilaya.

Habari nyingine zinasema katika muda mfupi uliopita, wilaya moja ya mkoa wa Henan ilifanya uchunguzi kuhusu hali ya haki na maslahi ya wanawake vijijini. Uchunguzi huo unaonesha kuwa, wanawake wa vijijini wanakosa mwamko wa kushirikisha kwenye mambo ya kisiasa na shughuli za kijamii. Ili kubadilisha hali hiyo, wilaya hiyo imechukua hatua kadhaa, kama vile kusikiliza maoni ya wanawake, kutoa kipaumbele kisera katika kuwashirikisha wanawake katika mambo ya kisiasa, kuweka data za makada wanawake wenye sifa bora, na kutoa mafunzo kwa wanawake vijijini ili kuongeza mwamko na uwezo wao wa kushiriki katika mambo ya kisiasa, na mashirika ya wanawake yanatakiwa kufanya kazi vizuri ipasavyo kutoa mafunzo kwa wanawake vijijini.

Idhaa ya kiswahili 2007-07-05