Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-07-04 17:30:06    
Sayansi na teknolojia zitatoa mchango muhimu katika shughuli za utoaji habari kwenye michezo ya Olimpiki ya Beijing

cri

Mwaka 2008 unakaribia siku hadi siku, shughuli za maandalizi ya michezo ya Olimpiki ya Beijing zimeendelea hatua kwa hatua. Ili kuandaa vizuri michezo hiyo, kamati ya maandamizi ya michezo ya Olimpiki ya Beijing ilitoa kauli mbiu ya "Olimpiki ya kisayansi na kiteknolojia". Namna ya kupashana habari za michezo ya Olimpiki kwa njia ya kisayansi na kiteknolojia imekuwa shughuli moja muhimu kati yake.

Hivi karibuni, mkutano wa tatu wa baraza la vyombo vya habari kuhusu sayansi na teknolojia limefanyika mjini Beijing, wajumbe wa vyombo mbalimbali vya habari vya China, wataalamu wa teknolojia ya upashanaji habari na wajumbe wa makampuni walijadiliana kuhusu namna ya kuunga mkono shughuli za utoaji habari wa michezo hiyo kwa njia ya kisayansi na kiteknolojia.

Baraza hilo linalenga kuwafahamisha wajumbe kuhusu hali ya maandalizi ya teknolojia zinazohusiana na shughuli za utoaji habari katika michezo hiyo ya Olimpiki, kuweka mpango wa maandalizi ya teknolojia ya matangazo ya kitarakimu ya michezo hiyo na matangzao ya kwenye mtandao, ili kufanya maandamizi kwa shughuli za utoaji habari za michezo hiyo.

Naibu mkurugenzi wa shirika la habari la taifa la China Xinhua Bw. Lu Wei alitoa hotuba kwenye baraza hilo akifafanua athari za maendeleo ya teknolojia kwa utoaji habari, na kusisitiza umuhimu wa sayansi na teknolojia kwa michezo ya Olimpiki. Bw. Lu Wei alisema:

"Olimpiki ya kisayansi na kiteknolojia" ni msingi, sayansi na teknolojia ni uhakikisho na uungaji mkono kwa michezo ya Olimpiki. Kuandaa michezo ya Olimpiki ya kiwango cha juu kunahitaji sayansi na teknolojia za kiwango cha juu. Michezo ya Olimpiki imeendelea kwenye msingi ya sayansi na teknolojia, ikiwa bila ya maendeleo ya sayansi na teknolojia, michezo hiyo haitakuwa na athari na kiwango cha hivi leo."

Imefahamika kuwa, katika michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008, kamati ya maandamizi ya michezo ya Olimpiki ya Beijing itatumia teknolojia mpya kuhudumia vyombo vya habari. Kama vile, itatoa huduma za upashanaji habari, huduma za utoaji wa matokeo ya michezo, sauti na picha za michezo na huduma za usimamizi wa mawimbi ya radio.

Huduma hizo zinahusisha teknolojia kadhaa mpya. kwa mfano, huduma za upashanaji habari zitategemea teknolojia ya kisasa ya 3G. mbali na hayo, vifaa vipya pia vitatolewa vikiwemo magari ya mawasiliano yenye uwezo wa kufanya kazi mbalimbali. Magari hayo ni kama vituo vya usimamizi vinvyoweza kuhamahama, yanaweza kufika haraka mahali palipotokea matukio na kushughulikia usimamizi na uratibu wa jumla.

Ili kuhakikisha utoaji wa huduma kamili za teknolojia ya juu kwa vyombo vya habari, vigezo vya matangazo ya Mobile Multimedia CMMB vilivyosanifiwa na idara kuu ya radio, filamu na televisheni ya taifa la China SARFT pia vitahudumia michezo ya Olimpiki ya Beijing mwaka 2008. vigezo hivyo ambavyo vigezo vya kwanza vilivyosanifiwa na China kwa ajili ya vyombo vinayohamahama vikiwemo simu za mikononi na kompyuta za laptop, vinaweza kutangaza vipindi 25 vya televisheni na vipindi 30 vya radio kote nchini China kwa kupitia mawimbi za saitelaiti. Hivi sasa, mtandao wa jaribio la vigezo hivyo umeanzishwa mjini Beijing, na katika muda wa michezo ya Olimpiki, vigezo hivyo vitatoa huduma kwa miji mitano inayoshiriki kwenye maandalizi ya michezo hiyo yaani Beijing, Shanghai, Tianjin na Shenyang.

Aidha, mtandao wa Internet wa njia pana pia utahudumia shughuli mbalimbali za michezo ya Olimpiki. Mtandao huo unaweza kuhakikisha mawasiliano yenye ufanisi na usalama. Naibu maneja mkuu wa idara ya usimamizi wa mawasiliano ya michezo ya Olimpiki katika kampuni ya Netcom ya China anayeshugulikia kazi hiyo Bw. Zhang Ling alisema:

"tunatoa huduma tofauti kwa vyombo vya televisheni na magazeti, kwa vyombo vya televisheni, tunatumia optical fiber ili kuhakikisha ubora wa matangazo. Kwa vyombo vya magazeti, tunatoa huduma za mtandao wa internet wa njia pana, na pia kuweka mtandao maalum wa Olimpiki mwenye ufanisi wa 150m kwa kila sekondi. Waandishi wa habari wanaweza kutumia habari nchi za nje kwa kupitia mtandao huo. Nadhani kuwa huduma hizo zitaweza kutoa uhakikisho imara kwa shughuli za upashanaji habari za vyombo vya habari katika michezo ya Olimpiki."

Mbali na huduma za mtandao wa Internet mwenye waya, Beijing pia itaweka mtandao wa njia pana bila waya. Imefahamika kuwa, ili kuandaa michezo ya Olimpiki, ujenzi wa mtandao wa kasi bila waya unaendelea hatua kwa hatua. Kabla ya robo la pili la mwaka 2008, viunganisho zaidi ya elfu 9 vya mtandao huo pamoja na vituo 150 vya huduma za mtandao huo vitawekwa kwenye eneo la kilomita 275 mjini Beijing ambalo linafunika asilimia 90 ya mitaa ya mji huo. Ufanisi wa mtandao bila waya utakuwa ni mara tatu hadi nne kuliko ule wa kawaida, ambao utakidhi kikamilifu mahitaji kwa mtandao kwenye michezo ya Olimpiki.

Kampuni ya upashanaji habari ya ZTE ya China iliwajibika na ujenzi wa mfumo wa mtandao wa njia pana katika michezo ya Olimpiki ya Athens mwaka 2004, mtandao umefunika miundombinu yote ya Olimpiki, ikiwemo uwanja mkuu wa michezo, kituo cha matangazo ya moja kwa moja ya televisheni cha kimataifa, kituo cha utoaji habari na hoteli za waandishi wa habari. Naibu mwenyekiti wa bodi ya kompuni hiyo Bw. Xu Ming alisema, teknolojia za kampuni hiyo zinaweza kutimiza kikamilifu mahitaji ya michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008.