Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-07-04 17:56:35    
Bara la Afrika litaendelea kusukuma mbele utandawazi

cri

Mkutano wa 9 wa wakuu wa Umoja wa Afrika uliofunguliwa tarhe mosi Julai, ulifungwa tarehe 3 huko Accra, mji mkuu wa Ghana. Usiku wa siku hiyo presidium ya Mkutano huo ilitoa Taarifa ya Accra ikisema kuwa, Afrika itaendelea kusukuma mbele utandawazi wa Afrika.

Katika siku tatu zilizopita, viongozi wa nchi 53 wanachama au wawakilishi wao walijadili zaidi suala kuhusu kuanzishwa kwa nchi ya shirikisho ya Afrika. Aidha Mkutano huo ulijadili suala la Darfur, suala la Somalia, usalama wa Afrika na umuhimu wa Kamati ya amani, haki za binadamu, watoto wa Afrika na suala la umaskini. Kuhusu suala la kuanzisha nchi ya shirikisho ya Afrika, yaani kuujenga Umoja wa Afrika kuwa Shirikisho la Afrika, nchi nyingi za Afrika zinaunga mkono wazo hilo, lakini kuhusu namna ya kutekeleza suala hilo, kuna migongano mingi, zaidi ni kuhusu kuanzishwa kwa "serikali ya shirikisho ya Afrika" ni kuimarisha madaraka ya Kamati ya Umoja wa Afrika uliopo au kuunda muundo mwingine; ni kuanzisha mara moja shirikisho hilo au kutunga kwanza ratiba halafu kutimiza lengo hatua kwa hatua.

Kiongozi wa Libya Bw Muamar Gaddafi ni mtetezi mwenye juhudi kubwa wa kusukuma mbele utandawazi wa Afrika. Mwishoni mwa mwezi uliopita, Bw Gaddafi alifanya matembezi ya mfululizo nchini Mali, Guinea, Sierra Leone na Cote D'ivoire, akijitahidi kuwashawishi viongozi wa nchi mbalimbali za Afrika kukubali wazo lake la kuanzisha serikali ya shirikisho ya Afrika halafu kuanzisha "nchi ya shirikisho ya Afrika" kwenye Mkutano wa wakuu. Kwenye mikutano ya hadhara iliyofanyika huko Conakry, mji mkuu wa Guinea, na Abidjan, Cote D'ivoire alisema, kila nchi ya Afrika haiwezi kuishi peke yake, isipokuwa tu kwa kuanzisha serikali ya pamoja, kuunda jeshi lenye askari milioni 2, kutoa fedha na pasipoti za pamoja, halafu kuanzisha nchi yenye nguvu ya shirikisho ya Afrika, ndipo Afrika itakapokuwa na mustakabali mzuri. Rais Abdoulaye Wade wa Senegal ana maoni ya pamoja na Gaddafi, na wote hao wanatumai kuanzisha mara moja "serikali ya shirikisho" badala ya Kamati ya Umoja wa Afrika, ili kutunga sera za pamoja za kidiplomasia na biashara za Afrika. Rais Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia pia aliutaka Mkutano upitishe wazo la "nchi ya shirikisho ya Afrika", na kuzielekeza nchi wanachama zitunge mpango wa kutimiza lengo hilo.

Ingawa sauti ya kuunga mkono utandawazi wa Afrika ni kubwa sana, lakini nchi nyingi za Afrika bado zinashikilia msimamo wa kusukuma mbele utandawazi huo hatua kwa hatua. Rais Umaru Yar'aadua wa Nigeria alidhihirisha kwenye mkutano huo kwamba, nchi za Afrika zinatakiwa kufuatilia kwa dharura kuhimiza usimamizi wa serikali na maendeleo ya uchumi wa nchi mbalimbali za Afrika, pamoja na kuhimiza utandawazi wa uchumi wa sehemu mbalimbali. Amezitaka nchi za Afrika zichukue njia ya kutimiza lengo kwa utaratibu na hatua kwa hatua. Rais Yar'adua alisema, sehemu mbalimbali za Afrika zinakabiliwa na matatizo ya aina mbalimbali kama vile hali duni ya miundo mbinu, upungufu wa nishati, ugonjwa wa ukimwi na ugonjwa wa kifua kikuu. Kama matatizo hayo hatataweza kutatuliwa kwanza, hakika yatakwamisha utandawazi wa kisiasa na kiuchumi wa bara la Afrika.

Rais Yoweri Museveni wa Uganda pia haungi mkono maoni ya kuandalia mara moja ili kuanzisha serikali ya shirikisho ya Afrika. Rais Museveni alisema kutimiza utandawazi wa uchumi barani Afrika kutafanikiwa, lakini haiwezekani kutimiza utandawazi wa kisiasa barani Afrika. Kwani kuna tofauti kubwa ya utamaduni kati ya sehemu mbalimbali za Afrika, kama watu wa sehemu hizo watalazimishwa kutimzia utandawazi wa kisiasa huenda kutasababisha hali wasiwasi katika uhusiano kati ya nchi na nchi.

Aidha, nchi nyingine kadhaa zinachukua tahadhari kuhusu suala la "serikali ya shirikisho", ambazo zinaona kuwa madaraka ya serikali ya shirikisho ya Afrika yanapaswa kuzuiliwa kwa kufaa. Rais Omar Bongo wa Gabon alisema ni lazima kuondoa wasiwasi wa nchi za Afrika kuhusu mamlaka yake katika mchakato wa kuanzishwa kwa serikali ya shirikisho, na madaraka ya serikali ya shirikisho hayapaswi kupita kiasi cha mamlaka ya kila nchi.

Na nchi za Afrika zilizohudhuria Mkutano huo mwishoni zimefikia maoni ya pamoja ya kufanya utafiti kuhusu masuala husika huku kufanya juhudi za kuelekea kuanzishwa kwa nchi ya shirikisho ya Afrika.