Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-07-04 19:23:18    
Mapishi ya mbavu za nyama ya nguruwe na nanasi

cri

Mahitaji

Mbavu za nyama ya nguruwe gramu 500, nanasi gramu 150, vitunguu maji gramu 25, tangawizi gramu 25, mchuzi wa sosi gramu 30, sukari gramu 20, mvinyo wa kupikia gramu 20, sosi ya nyanya gramu 40, chembechembe za kukoleza ladha gramu 2, mafuta gramu 50

Njia

1. changanya mbavu za nyama ya nguruwe pamoja na mchuzi wa sosi na mvinyo wa kupikia,

2. washa moto tia mafuta kwenye sufuria, tia mbavu za nyama ya nguruwe kwenye sufuria zikaange mpaka ziwe rangi za hudhurungi na kasha zipakue.

3. washa moto tena tia vipande vya vitunguu maji na tangawizi korogakoroga, halafu mimina mchuzi wa sosi, sukari, mvinyo wa kupikia, sosi ya mnyanya na maji korogakoroga, na kasha tia mbavu za nyama ya nguruwe, baada ya kuchemka punguza moto kidogo, endelea kuchemsha kwa dakika 40, baada ya hapo tia vipande vya nanasi, na kasha baada ya dakika 10 ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.