Ili makampuni yalete maendeleo endelevu ya uchumi na yawajibike kwa jamii, miaka saba iliyopita Umoja wa Mataifa ulianzisha harakati za "makubaliano ya dunia kwa makampuni" (Global Compact). Tarehe tano Julai Umoja wa Mataifa ulifanya mkutano mkubwa wa kilele kwenye kasri la Umoja wa Mataifa katika makao makuu yake mjini Geneva.
Harakati za makubaliano ya dunia kwa makampuni zilianzishwa na katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Bw. Kofi Annan. "Makubaliano" hayo yanamaanisha vigezo muhimu kumi vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya shughuli za kamampuni, vigezo hivyo vikiwa ni pamoja na kutetea haki za wafanyakazi, kukataa kuajiri watoto, na kwa kiwango kikubwa kupunguza uchafuzi wa mazingira na kuheshimu sheria za kimataifa, kukomesha wizi wa fedha na rushwa, na kujipatia imani ya bidhaa. Kama kampuni fulani ikikubali kanuni hizo inaweza kuwa mwanachama wa "makubaliano ya dunia kwa makampuni", katika miaka ya karibuni harakati hizo zimekuwa haraka na makampuni wanachama yamekuwa elfu kadhaa kutoka zaidi ya 40 hapo awali. Katibu mkuu wa sasa wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon anaona kuwa kanuni za "makubaliano ya dunia kwa makampuni" zinakubaika sana duniani.
"'Makubaliano ya dunia kwa makampuni' yamepata mafanikio makubwa, angalieni orodha hii, makampuni wanachama yamefikia zaidi ya 4,000 ambayo yanapatikana kila sehemu ya dunia, kwa hiyo harakati hizo zimekuwepo duniani kote."
Kwenye mkutano huo wa siku mbili, wakuu wa serikali na makampuni pamoja na wajumbe wa vyama vya wafanyakazi karibu elfu moja walipeana uzoefu na kuelezana mikakati ya maendeleo endelevu. Kwenye karatasi ya uchunguzi, kuhusu tishio kubwa kwa maendeleo ya kampuni, makampuni mengi yanaona kuwa ni tatizo la mazingira kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Bw. Ban Ki-moon alisema, mkutano huo umegusia suala la hifadhi ya mazingira safi, anaona faraja kuhusu suala hilo.
"Katika siku za mkutano, washiriki wa mkutano sio tu wamefahamu uzoefu wa kisasa wa kutekeleza kanuni za makubaliano, bali jambo linalonifurahisha zaidi ni kwamba mkutano huo utajadili suala la mabadiliko ya hali ya hewa, na kujadili namna ya kuwajibika kutokana na uchafuzi wa mazingira, kujadili namna ya kuimarisha hifadhi ya mazingira safi. Na wakati wa mkutano, umepangwa kufanya mkutano wa wakuu wa makampuni ili kubadilishana maoni kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa.
Mkutano huo umetoa ripoti ya mwaka kuhusu hali ya "makubaliano ya dunia kwa makampuni". Ripoti inasema, kati ya makampuni, mashirikisho ya wafanyabiashara na vyama vya wafanyakazi zaidi ya 4,000, makampuni makubwa kiasi na madogo yanachukua zaidi ya 90% na makampuni 500 yanayoongoza duniani yanachukua 3% tu. Bw. Neville Isdell ambaye ni katibu mkuu mtendaji wa kampuni ya Coca Cola ambayo imejiunga na "makubaliano ya dunia kwa makampuni" siku moja kabla ya mkutano huo alieleza,
"Hivi sasa mambo ya dunia yanatatanisha na yanategemeana sana. Makampuni yakitaka kujiendeleza, ni lazima yawe na uwezo wa kukabiliana na hali mpya, maendeleo ya makampuni yanahitaji hali nzuri ya kijamii, mambo ambayo hapo zamani yalikuwa hayahusiki na makampuni kama vile afya na heshima, sasa yanahusika moja kwa moja na maendeleo ya makampuni. Kampuni ya Coca Cola ikitaka kupata maendeleo ni lazima ijiunge na "makubaliano ya dunia kwa makampuni" na kuwajibika sawa na makampuni mengine."
Kwenye "makubaliano ya dunia kwa makampuni" kuna mada nyingine muhimu, nayo ni kupiga marufuku kwa ufisadi katika shughuli za makampuni. Kwa mujibu wa takwimu za benki ya dunia, kila mwaka dola za Kimarekani kiasi cha milioni 250 zinatumika katika rushwa au wizi. Kwenye mkutano mwenyekiti wa Shirika la Uwazi la Kimataifa Bi. Huguette Labelle alisema.
"Shughuli za biashara zina fursa nyingi za ufisadi, kwa hiyo si rahisi kutekeleza kanuni za kupambana na ufisadi. Mkutano huu umetupatia fursa ya kubadilishana uzoefu."
Idhaa ya kiswahili 2007-07-06
|