Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-07-11 15:59:09    
Mapishi ya nyama ya kuku na tangawizi

cri

Mahitaji

Nyama ya kuku, tangawizi gramu 10, vitunguu maji gramu 5, siki kijiko kimoja, mchuzi wa sosi kijiko kimoja, mvinyo wa kupikia kijiko kimoja, maji ya wanga vijiko viwili.

Njia

1. kata nyama ya kuku iwe vipande vipande, washa moto, mimina mafuta kwenye sufuria, mpaka yawe joto la nyuzi 60, tia vipande vya nyama ya kuku na tangawizi korogakoroga, halafu tia chumvi, vitunguu maji, korogakoroga, tia mchuzi wa soya na maji.

2. baada ya dakika 5, tia vitunguu maji na mimina maji ya wanga, korogakoroga, mimina siki korogakoroga, baada ya maji ikukauka, ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari.