Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-07-12 16:39:22    
Kama wanandoa wote ni watoto pekee kutoka familia zao nchini China,wanaruhusiwa kuzaa watoto wawili

cri

Msemaji wa kamati ya idadi ya watu na uzazi wa mpango ya China Bwana Yu Xuejun tarehe 10 Julai alipotembelea tovuti ya serikali ya China alisema, katika miji na mikoa mingi ya China kama wanandoa wote ni watoto pekee kutoka familia zao basi wanaruhusiwa kuzaa watoto wawili.

Bw. Yu Xuejun alisema China ina eneo kubwa, maendeleo ya jamii na idadi ya watu hayana uwiano, hivyo suala la idadi ya watu lina tofauti kubwa kati ya sehemu mbalimbali nchini China katika vipindi tofauti. Kwa hivyo serikali za sehemu mbalimbali zinachukua hatua halisi zenyewe kuhusu utekelezaji wa sera ya uzazi wa mpango. Kwa mfano mjini Beijing familia za aina 9 zinaruhusiwa kuzaa mtoto wa pili, kama vile mtoto wao pekee amethibitishwa kuwa na ulemavu usio wa kurithi; wanandoa wote ni watoto pekee kutoka familia zao; wanandoa walimwasili mtoto kutokana na kushindwa kuzaa baada ya kufunga ndoa kwa miaka mitano, lakini baadaye wanapata mimba wao wenyewe; Wafanyakazi wa makabila madogo madogo waliohamia mjini Beijing kufanya kazi; na mwanakijiji wa kiume anayeishi pamoja na familia ya mke wake isiyo na mtoto wa kiume na anapenda kuwatunza wazee. Hivyo wanandoa wakitaka kuzaa mtoto wa pili, wanaweza kuangalia sera husika ya sehemu wanakoishi.

Imefahamika kuwa hivi sasa licha ya mkoa wa Henan, miji na mikoa mingine nchini China imeweka vifungu kuwa, kama wanandoa wote ni watoto pekee kutoka familia zao wanaruhusiwa kuzaa watoto wawili. Lakini hii haimaanishi kuwa sera ya uzazi wa mpango imebadilika. Bw. Yu Xuejun alisema, kutekeleza sera ya uzazi wa mpango kunawahimiza wananchi wazae watoto kwa mpango, lakini siyo kuhimiza familia zinazoruhusiwa kuzaa watoto wawili kuzaa mtoto mmoja tu, wala siyo kuwahimiza wanandoa kutozaa mtoto. Watu wana haki ya kuamua kama watazaa watoto au la.

Bw. Yu Xuejun alidhihirisha kuwa, nchini China kuna tofauti katika sera ya uzazi wa mpango kati ya sehemu mbalimbali, kati ya miji na vijiji, na kati ya makabila mbalimbali. Asilimia 35.9 ya familia zinaruhusiwa kuzaa mtoto mmoja, asilimia 52.9 ya familia zinaruhusiwa kuzaa mtoto mmoja na nusu, na asilimia 11 ya familia zinaruhusiwa kuzaa watoto wawili hata zaidi.

Bw. Yu Xuejun pia alidhihirisha kuwa, China ilipoanza kutekeleza sera ya uzazi wa mpango ilikuwa inachukua hatua kali zaidi kwa wakazi wa mijini kuliko wakazi wa vijijini, kwa wakazi wa sehemu ya mashariki na kati kuliko watu wanaoishi katika sehemu ya magharibi, na kwa watu wa kabila la wahan kuliko watu wa makabila madogo madogo.

Kutokana na tofauti ya utoaji huduma za jamii kati ya miji na vijiji, wakulima wengi wanapaswa kutegemea familia zao kuwatunza wanapozeeka, hivyo sera ya uzazi wa mpango ni lazima itoe kipaumbele kwa familia za vijijini ambazo zinaruhusiwa kuzaa watoto wengi zaidi kuliko familia za mjini. Bw. Yu Xuejun alisisitiza kuwa, ni kweli kwamba baadhi ya familia hasa za vijijini zimeathirika na sera ya uzazi wa mpango. Lakini katika miaka zaidi ya 30 iliyopita tangu sera ya uzazi wa mpango ianze kutekelezwa, China imepata maendeleo makubwa ya kiuchumi na kijamii. Hivyo kutupia macho mbali, sera hiyo italinufaisha taifa zima la China na wakazi wake wote. Kwa hivyo serikali ya China imetoa pendekezo la kuzinufaisha zaidi familia zilizofuata sera ya uzazi wa mpango kwa matokeo ya maendeleo ya jamii na uchumi. Kwa mfano katika miaka ya karibuni familia za vijijini zilizofuata sera ya uzazi wa mpango zimepewa sera nafuu katika juhudi za kupunguza umaskini.

Idhaa ya kiswahili 2007-07-12