Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-07-13 16:25:50    
Wataalamu wa mafuta wa China wafundisha ujuzi nchini Sudan

cri

Tarehe 21 mwezi Juni kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara ya nishati na madini ya Sudan, wataalamu kadhaa wa mafuta wa China walitoa hotuba wakielezea wenzao wa Sudan uzoefu wa uchimbaji wa mafuta. Hotuba hizo zilizotolewa na wataalamu wa China ziliwavuta wasudan wengi, na kukaribishwa sana nao.

Mtaalamu wa mafuta wa China Bw. Wang Qimin ambaye alipewa tuzo ya kitaifa mara nyingi alisema, tangu mwaka 1960 amefanya kazi katika machimbo ya mafuta ya Daqing, na alipita vipindi vya mwanzo na maendeleo ya machimbo ya mafuta ya Daqing. Bw Wang alisema anafurahi sana kuwa na fursa ya kufanya mawasiliano na wenzao wa Sudan. Alisema ingawa shughuli za mafuta ya Sudan zimeendelezwa kwa miaka kumi tu, lakini zimepata maendeleo makubwa. Uzalishaji mafuta wenye ufanisi na njia ya usimamizi wa kimataifa wa machimbo ya mafuta nchini Sudan uliwavutia wataalamu wa China.

Bw. Wang alisema machimbo ya mafuta ya Daqing yalianza kuendelezwa tangu mwishoni mwa miaka ya 50 na mwanzoni mwa miaka ya 60 ya karne iliyopita. Kutokana na kukosa misaada kutoka nchi za nje na uzoefu, wafanyakazi waliokuwepo kwenye machimbo hayo walifanya juhudi kuchimba mafuta, na kukusanya uzoefu.

Bw. Wang Qimin na wataalamu wengine wa China walijulisha maendeleo ya machimbo ya Daqing, hasa uzoefu wa kudumisha utoaji mkubwa wa mafuta kwa hatua madhati katika miongo kadhaa iliyopita, pia walijibu maswali mengi ya kiufundi yaliyotolewa na wenzao wa Sudan. Hotuba hizo ziliwatia moyo wenzao wa Sudan kuhusu mustakabali wa maendeleo ya sekta ya mafuta ya nchi hiyo.

Baada ya mkutano huo wa hotuba, mhandisi mmoja wa kampuni ya mafuta ya Sudan aliwaambia waandishi wa habari kuwa, hotuba zilizotolewa na wataalamu wa China zilimnufaisha sana. Alisema shughuli za uchimbaji wa mafuta nchini Sudan haziwezi kupata maendeleo makubwa bila kupata msaada kutoka kwa China, hali kadhalika kwa maendeleo makubwa ya uchumi wa Sudan katika miaka kadhaa iliyopita. Alisema China inatoa misaada ya uzoefu na ufundi kwa Sudan siku zote bila kutafuta maslahi, mkutano huo pia umethibitisha hali hiyo.

*************

Ubalozi wa China nchini Cote D'ivoire tarehe 20 mwezi June ulikabidhi zana za uvuvi zenye thamani ya RMB Yuan laki 2.5 kwa Cote D'ivoire, ili kuiunga mkono Cote D'ivoire kuendeleza ufugaji wa samaki. Balozi wa China nchini Cote D'ivoire Bw. Ma Zhixue alisema, China ina matumaini kuwa zana hizo za uvuvi zinaweza kutoa msaada katika kuboresha mazingira ya kazi na maisha ya wafugaji wa samaki wa Cote D'ivoire. Vilevile alisema serikali ya China na wananchi wake wataendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wananchi wa Cote D'ivoire kwa ajili ya kurudisha amani na kufanya ukarabati wa uchumi.

Waziri wa miundo mbinu ya uchumi wa Cote d'ivoire pia alishiriki kwenye sherehe ya kukabidhi zana hizo, aliishukuru serikali ya China kwa misaada inayotoa siku zote kwa ufugaji wa samaki na shughuli nyingine nchini Cote d'ivoire. Alisema zana hizo zinakidhi mahitaji ya upande wa Cote D'ivoire, China ina uzoefu mkubwa katika ufugaji wa samaki, na Cote d'ivoire ina matumaini kuwa China itawafundisha watu wa Cote d'ivoire ujuzi wa kufuga samaki.

*************

Vyombo vya habari vya Kenya hivi karibuni vilisema, wafanyabiashara kadhaa wa China watashirikiana na wafanyabiashara wa Kenya kuanzisha kiwanda cha kusindika samaki wa aina mbalimbali mkoani Niansa nchini Kenya, na uwekezaji wa mwanzo ulikadiriwa kufikia dola za kimarekani milioni 1.5.

Kiwanda hicho kinafanya maandalizi ya kununua ardhi, na kitaanzisha vituo vitano vya samaki barafu. Kituo cha kwanza kitajengwa miaka mitano ijayo, ambapo wavuvi na wafanyabiashara wa samaki wataweza kufanya biashara vizuri, na pia nafasi za ajira za huko zitaongezeka.

*********************

Balozi wa China nchini Cote d'ivoire Bw. Ma Zhixue ambaye ataondoka madarakani hivi karibuni, mwezi June alipewa tuzo ya heshima ya taifa na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo akiwa kwa niaba ya rais Laurent Gbagbo wa Cote d'ivoire.

Waziri wa mambo ya nje wa Cote d'ivoire alimsifu sana Bw. Ma Zhixue kwa juhudi zake za kuendeleza uhusiano kati ya China na Cote d'ivoire na kuimarisha urafiki kati ya wananchi wa nchi hizo mbili. Waziri huyo alieleza matumaini yake kuwa baada ya kuondoka kazini kutoka Cote d'ivoire, Bw. Ma Zhixue anaendelea kushughulikia na kuhimiza maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Bw. Ma Zhixue alimshukuru rais Gbagbo na serikali ya Cote d'ivoire na wananchi wake kwa kumpa tuzo hilo. Alisema hii ilionesha kuwa serikali ya Cote d'ivoire inatilia maanani kuendeleza uhusiano kati yake na China. Bw. Ma Zhixue pia alisema, baada ya kuondoka madarakani ataendelea kutoa mchango wake katika kuhimiza maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili kama alivyofanya siku zote zilizopita.

*******************

Mwenyekiti wa tume ya maonesho ya biashara ya Madagascar Bw. Bazafi Rica hivi karibuni alitangaza kuwa, Madagascar imepanga kufanya maonesho ya biashara ya Madagascar kuanzia tarehe 11 hadi tarehe 12 mjini Guangzhou nchini China.

Bw. Rica alisema nia ya kufanya maonesho hayo ni kuonesha na kuuza bidhaa za Madagascar kwa wafanyabiashara wa China, kutangaza fursa za ushirikiano na wafanyabiashara wa China. Maonesho hayo yatafanywa pamoja na wizara ya uchumi, mpango na kampuni binafsi ya Madagascar, shirikisho la viwanda na biashara la Madagascar, na shirikisho la biashara kati ya Madagascar na China. Imefahamika kuwa kampuni zaidi ya 60 zimejiandikisha kushiriki kwenye maonesho hayo.

Katika miaka kadhaa iliyopita, ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Madagascar umeendelezwa haraka. Thamani ya biashara kati ya nchi hizo mbili mwaka 2006 ilifikia dola za kimarekani milioni 250, na katika miezi minne ya kwanza ya mwaka huu thamani hiyo ilifikia dola za kimarekani milioni 150, na kuongezeka kwa asilimia 22 kuliko mwaka jana wakati kama huo.

Idhaa ya kiswahili 2007-07-13