Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-07-18 18:56:24    
Mapishi ya samaki na bilinganya

cri

Mahitaji

Samaki mmoja, bilinganya moja, chumvi vijiko viwili, chembechembe za kukoleza ladha kijiko kimoja, mchuzi wa sosi vijiko viwili, pilipili manga kijiko kimoja, vipande vya vitunguu maji, pilipili hoho, tangawizi , sosi ya pilipili hoho vijiko viwili.

Njia

1. ondoa vitu vilivyo ndani ya tumbo la samaki, halafu osha samaki na kumkata awe vipande.

2. kata bilinganya liwe vipande. Washa moto weak sufuria motoni, tia vipande vya bilinganya vikaange halafu vipakue.

3. tia vipande vya tangawizi na sosi ya pilipili hoho korogakoroga, halafu tia vipande vya samaki korogakoroga, mimina maji baada ya kuchemka, tia chumvi, chembechembe za kukoleza ladha, korogakoroga, tia vipande vya bilingaya, na pilipili hoho korogakoroga halafu punguza moto kidogo, baada ya dakika 15, tia mchuzi wa sosi na maji ya wanga korogakoroga, ipakue. Tia vipande vya vitunguu maji na pilipili hoho. Mpaka hapa kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.