Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-07-19 19:37:33    
Wang Ruiguang na majaribio matatu katika maisha yake

cri

Bw. Wang Ruiguang mwenye umri wa miaka 35 ni mwenyeji wa Beijing. Ingawa yeye anaonekena mkimya kama walivyo wakazi wa kusini mwa China, lakini anapoongea huonesha uchangamfu.

Bw. Wang Ruiguang alihitimu masomo ya lugha ya kiitalia mwaka 1995 kwenye chuo kikuu cha lugha za kigeni cha Beijing, na alianza kufanya kazi kwenye idara ya mambo ya Ulaya katika wizara ya mambo ya nje ya China. Baada ya mwaka mmoja alitumwa kufanya kazi kwenye ubalozi wa China nchini Italia.

Kazi ya uanadiplomasia aliyoifanya kwa miaka miwili ilimpa maarifa mengi. Lakini pia nataka kupata uzoefu mpya katika maisha yake. Baada ya kutafakari kwa makini, Bw. Wang Ruiguang aliamua kujiuzulu na kuanza kufanya biashara. Watu wengine hawakuelewa uamuzi wake wa kuacha kazi nzuri ya mwanadiplomasia, lakini Wang Ruiguang aliamini kuwa chaguo lake ni sahihi. Alisema:

"Maarifa niliyopata kutokana na kufanya kazi kwenye wizara ya mambo ya nje ni makubwa na yatanisaidia katika kazi za baadaye. Naona chaguo langu ni sahihi na sijutii."

Baada ya kujiuzulu, Wang Ruiguang alitaka kupumzika kwa muda mfupi nyumbani, lakini wakati huo huo opera ya Turandot iliyoandaliwa chini ya uongozi wa Bw. Zhang Yimou ilikuwa inaoneshwa kwenye ukumbi wa kasri ya kifalme hapa Beijing, hivyo Bw. Wang Ruiguang alitakiwa kuwa mtafsiri. Katika muda huo, kiwango chake cha utafsiri kilisifiwa na wafanyakazi wa kikundi cha opera hiyo na pia kilimvutia mtendaji wa kampuni moja ya utamaduni. Hivyo Bw. Wang Ruiguang alijiunga na kampuni hiyo baada ya kuondoka kutoka wizara ya mambo ya nje. Alisema:

"mwanzoni nilijihusisha na mawasiliano ya utamaduni wa filamu na televisheni kuhusu haki ya kunakili ya vipindi vya televisheni, kwa kuwa niliwahi kufanya kazi nchini Italia, hivyo nilishughulikia kujenga uhusiano kati yetu na kituo cha televisheni na radio ya taifa ya Italia na kuingiza vipindi vya Italia, mpaka sasa katuni zilizoingizwa kutoka Italia zinaoneshwa kwenye kituo cha televisheni cha CCTV.

Bw. Wang Ruiguang alifanya kazi kwenye kampuni hiyo kwa miaka mitatu, alisaidia kampuni hiyo kusaini mikataba ya miradi mingi kutokana na uwezo wake mkubwa na alikuwa tegemeo la kampuni hiyo. Bw. Tian Xing ambaye aliwahi kusoma na kufanyakazi naye alimsifu Bw. Wang Ruiguang, akisema:

"yeye ni mchekeshaji. Kwanza niliona kuwa anapenda sana michezo ya sanaa na pia ana mawazo yake mazuri na anathubutu kufanya ujasiri na kila kazi anaifanya kwa makini."

Baada ya miaka mitatu, Bw. Wang Ruiguang alianzisha kampuni yake na kuendelea kujihusisha na mawasiliano ya utamaduni kati ya China na Italia. Mwezi Januari mwaka 2006, mwaka wa utamaduni wa China na Italia ulifunguliwa hapa Beijing, kampuni ya Bw. Wang Ruiguang ilishiriki kwenye shughuli za maonesho ya kikundi cha ngoma cha Italia nchini China na mkutano wa baraza la ujenzi la China na Italia. Maonesho zaidi ya 20 ya utamaduni na maonesho karibu na 100 ya michezo ya sanaa yaliyoandaliwa na serikali ya Italia yalifanyika kwa mafanikio nchini China. Ushirikiano kati ya China na Italia umepata mafaniko mengi kutokana na michango ya wafanyabiashara wanaojihusisha na mambo ya kiutamaduni Kama Wang Ruiguang.

Kutokana na shughuli za mwaka wa utamaduni wa China na Italia, wachina wameanza kuongeza hamu juu ya Italia siku hadi siku, wanafunzi wengi wa China waliomba kwenda kusoma kwenye vyuo vikuu vya Italia. Wakati huo huo serikali ya Italia ilirahisisha utaratibu kwa wanafunzi wa China kwenda kusoma nchini Italia, Bw. Wang Ruiguang alipoona hali hiyo, ndoto nyingi aliyokuwa nayo moyoni mwake ilianaza kumsukuma. Alisema:

"Nikiwa na umri wa miaka zaidi 40 nitakuwa mwalimu, hii ni ndoto yangu kutokana na athari ya familia yangu."

Kwenye ukoo wa Bw. Wang Ruiguang kuna watu zaidi ya 20 wanaojishughulisha na elimu. Ingawa aliendsha vizuri kampuni yake, lakini biashara ilikuwa sio jambo analofuatilia sana katika maisha yake. Alipoongea na rafiki yake wa wizara ya mambo ya nje ya China alipata habari kuhusu wizara ya elimu za Italia na China zimesaini makubaliano ya kuimarisha ushirikiano kati ya vyuo vikuu vya nchi hizo mbili, chuo kikuu cha Tonji cha Shanghai kilikuwa kimoja kati ya vyuo vikuu vilivyotangulia kufanya ushirikiano huo. Hivyo Bw. Wang Ruiguang alikwenda kwenye chuo cha Chonyi katika chuo kikuu cha Tongji mjini Shanghai na kufahamishwa chuo hicho kilihitaji walimu wa lugha ya kiitalia. Baada ya kubadilishana maoni na wakuu wa chuo, Bw. Wang Ruiguang aliamua kubadilisha tena kazi yake, alisema: "

"kuendesha kampuni na kuwa mwalimu ni mambo tofauti sana, lakini mambo hayo yanahusiana, maarifa niliyopata kwenye kazi zinazohusu utamaduni na miradi yalinisaidia baada ya kuanza kazi kwenye chuo kikuu cha Tongji. Nimewahi kufundisha, nina uvumilivu na pia nina maoni yangu katika ufundishaji wangu, nilichanganya maarifa ya watu wengine na kufundisha kutokana na uwezo tofauti wa kila mwanafunzi wangu."

Baada ya kuanza kufanya kazi katika chuo kikuu cha Tongji, licha ya kushughulikia majadiliano kuhusu ushirikiano kati ya chuo hicho na vyuo vikuu husika vya Italia, Bw. Wang Ruiguang pia anatoa ufundishaji wa kuongea kwa lugha ya kiitalia kwa wanafunzi wa China zaidi 30. mwanafunzi wake Li Xiaolin alisema: "

"ufundishaji wa mwalimu Wang unanivutia sana, kwa sababu yeye ana maarifa mengi, ufundishaji wake unavuia."

Hivi sasa Wang Ruiguang anaishi maisha ya kawaida kama waalimu wengine wa chuo kikuu, kila siku kutoka bweni hadi bwalo halafu kwenda darasani, ingawa ametengana na jamaa na rafiki zake, lakini anafurahia maisha yake, na anafanya kazi kwa bidii. Alisema: "

"mwaka 2007 ilikuwa ni maadhimisho ya miaka 100 ya chuo kikuu cha Tongji, wakati wa sherehe hiyo kulikuwa na shughuli kadhaa za ushirikiano kati ya vyuo vikuu, mashirika na serikali za nchi hizo mbili, nilishiriki kwenye shughuli za ushirikiano ya China na wizara ya mazingira, ardhi na bahari ya Italia. Aidha kwenye ushirikiano kati ya China na Italia, kuna mradi wa usimamizi wa mawasiliano ya umma kwenye maonesho ya bidhaa duniani yatakayofanyika huko Shanghai mwaka 2010, nitashiriki kwenye shughuli za kutoa ufundishaji na elimu katika miradi hiyo ya ushirikiano huo."