Idara husika imedokeza kuwa Mkutano wa viongozi wa ujumbe utakaohudhuria duru la 6 la mazungumzo ya pande 6 unaotazamiwa kumalizika tarehe 19 umerefushwa, wakati huo huo hatua ya Korea ya kaskazini ya kufunga majengo ya nyuklia pia imekaribishwa na pande mbalimbali.
Tangu mazungumzo ya pande 6 kuhusu suala la nyuklia ya peninsula ya Korea yaanze mwezi Agosti mwaka 2003, mazungumzo hayo yanafanyika kwa kutimiza lengo la kuifanya peninsula ya Korea iwe sehemu isiyo na silaha za nyuklia. Ingawa mchakato wa mazungumzo unakabiliwa na vipengele vingi na taabu kubwa pamoja na migongano mbalimbali, lakini pande zinazohusika zote hazijaacha juhudi zao. Naibu mkurugenzi wa idara ya utafiti wa mambo ya Japan katika Taasisi ya sayansi ya jamii ya China Bwana Jin Xide alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alisema:
"Mkutano wa viongozi wa ujumbe unaohudhuria duru la 6 la mazungumzo ya pande 6 unaofanyika sasa umerefushwa, naona hii ni ishara nzuri. Kiongozi wa ujumbe wa Marekani Bwana Christopher Hill aliwahi kusema, ni bora Mkutano huo upitishe taarifa ya mwenyekiti ya kutangaza maoni ya pamoja yaliyofikiwa kwenye Mkutano huo, ili jumuiya ya kimataifa iweze kufanya usimamizi, naona kurefushwa kwa Mkutano ni kwa ajili ya hiyo, ili kujadili kwa makini na kufikia maoni ya pamoja".
Kiongozi wa ujumbe wa Korea ya kusini unaohudhuria mazungumzo ya pande 6 Bwana Chun Yung Woo alisema, msimamo wa Korea ya kaskazini wa kufuata hali halisi kwenye Mkutano utasaidia kutunga mpango halisi wa utekelezaji wa siku zijazo na kutekeleza hatua ya mwanzo. Mwandishi wetu wa habari aliyeko Korea ya kusini amesema:
" Shirika la habari la Korea ya kusini tarehe 19 lilimkariri ofisa wa ujumbe wa Korea ya kusini akisema, hali ya mazungumzo hayo ni nzuri zaidi kuliko mazungumzo yote yaliyopita. Na hivi sasa Korea ya kaskazini inafanya mawasiliano na pande nyingine zote kwa kufuata kanuni zenye ufanisi halisi, msimamo huo unasaidia pande 6 za mazungumzo zitunge mpango wa utekelezaji wa kipindi cha pili wa waraka wa pamoja. Kutokana na maendeleo ya mazungumzo ya pande 6, uhusiano kati ya Korea ya kusini na Korea ya kaskazini, pia utaingia katika kipindi kipya cha maendeleo".
Vyombo vya habari vya nchi mbalimbali pia vinafuatilia sana mazungumzo hayo. Mwandishi wetu wa habari aliyeko nchini Marekani alisema:
"Gazeti la USA today la leo limesema, kwa kuwa Korea ya kaskazini ilifunga majengo makuu ya nyuklia jumamosi iliyopita, hivyo mazungumzo ya jumatano wiki hii yalifanyika katika hali inayosaidia pande husika zifanye juhudi. Gazeti la New York Times limesema, mazungumzo hayo yalifanyika kwa makini zaidi kuliko mazungumzo mengine yote yaliyopita".
Kiongozi wa ujumbe wa Russia Bwana Vladimir Rakhmanin tarehe 19 alisema, "kwa kuwa pande zote zinazohusika zimepata maendeleo kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea, hivyo Mkutano wa viongozi wa ujumbe unafanyika katika hali ya kirafiki". Alisema washiriki wa Mkutano huo wamejadili hali ya utekelezaji wa hatua ya mwanzo na kazi za kipindi kijacho.
Profesa Jin Dexi alisema mazungumzo hayo huenda yatatangaza waraka wa pamoja. Alisema kama Mkutano utarefushwa kwa siku moja, na kutangaza maoni ya pamoja, ambayo yatakuwa majumuisho ya utekelezaji wa hatua ya mwanzo ya waraka wa pamoja wa tarehe 13 Februari, halafu mpango wa utekelezaji wa kipindi cha pili wa hatua ya kutokomeza uwezo wa majengo ya nyuklia utatolewa, ambao utatoa mwelekeo mpya kwa mazungumzo ya pande 6 na mchakato wa kutokomeza uwezo wa majengo ya nyuklia.
|