Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-07-25 14:55:38    
China yaimarisha shughuli za kutoa mafunzo kwa madaktari wa ngazi ya shina ili kukinga na ugonjwa wa kisukari

cri

Kisukari ni mmoja wa magonjwa sugu ya kawaida, ugonjwa huo unatokana na upungufu wa kitu cha insulini au insulini kutofanya kazi vizuri mwilini. Hivi sasa China ina wagonjwa milioni 5 wa kisukari, na idadi hiyo inachukua asilimia 20 ya wagonjwa wote duniani. Katika miaka ya hivi karibuni, idadi hiyo bado inaongezeka kwa kasi.

Ili kupunguza idadi ya wagonjwa wa kisukari na kufanya vizuri kazi ya upimaji na matibabu ya ugonjwa huo, katika muda wa miaka mitatu iliyopita, wizara ya afya ya China na shirikisho la udaktari la China zilitoa mafunzo ya upimaji na matibabu kwa madaktari wa ngazi ya shina kutoka mikoa na sehemu 23, na kueneza ufahamu kuhusu ugonjwa wa kisukari kwa wakazi wa sehemu hizo.

Kisukari ni ugonjwa unaodumu kwa maisha yote, hivi sasa bado hautibiki kikamilifu. Lakini matibabu ya kisayansi yanaweza kudhibiti vizuri maendeleo ya ugonjwa huo. Kwa hivyo, kutambuliwa mapema na matibabu ya kisayansi ni muhimu sana kwa wagonjwa wa kisukari. Naibu mkuu wa shirikisho la udaktari la China Bw. Wu Mingjiang alisema,

"kisukari ni ugonjwa unaoweza kuthibitishwa na kutibiwa, kama kiwango cha matibabu cha madaktari kinainuliwa zaidi, ugonjwa huo unaweza kugunduliwa mapema na kutibiwa mwafaka, na kuzuia kutokea kwa magonjwa nyemelezi. Hali hii ni muhimu sana kwa kupunguza idadi ya wagonjwa wanaolemazwa na kufa kutokana na ugonjwa huo na magonjwa nyemelezi yake."

Kutokana na kuboreshwa kwa maisha ya watu wa China na kubadilika kwa utaratibu wa maisha yao, idadi ya wagonjwa wa kisukari inaongezeka kwa kasi. Mwaka 1979, wagonjwa wa kisukuri walichukua asilimia 0.67 ya idadi ya watu wa China, lakini hivi sasa idadi hiyo imezidi asilimia 5. kutokana na hali hiyo, serikali ya China imeendelea kuongeza uwekezaji kwa hospitali na idara za utafit wa dawa ili kuinua uwezo wa kinga na tiba ya ugonjwa huo. Lakini kiasi kikubwa cha raslimali za kinga na tiba ya kisukari zinakusanyika katika miji mikubwa, miji ya wastani na midogo na sehemu za vijijini, ambapo madaktari wana fursa chache tu kusikiliza mihadhara ya wataalamu wa eneo hilo, na pia ni vigumu kwo kupata ujuzi na teknolojia mpya za upimaji na matibabu ya kisukari.

Kuanzia mwaka 2004, wizara ya afya ya China na shirikisho la udaktari la China ziliandaa kwa pamoja shughuli za kuenza ufahamu kuhusu ugonjwa wa kisukari zinazoitwa "safari ndefu ya afya". Shughuli hizo zimetekelezwa kwenye mikoa na sehemu 23 nchii China na kwa jumla zimewatuma mamia ya wataalamu kutoa mafunzo na uelekezaji kwenye hospitali za sehemu mbalimbali, ili kueneza teknolojia mpya za matibabu ya kisukari na kuinua uwezo wa madaktari wa sehemu hizo katika kuthibitisha na kutoa matibabu ya ugonjwa huo. Profesa Chen Hong wa hospitali ya mto Zhujiang mkoani Guangdong ni mmoja wa wataalamu walioshiriki kwenye shughuli hizo. Bw. Chen Hong alisema:

"naona kuwa watumishi wa matibabu wa ngazi ya shina wanakosa sana ujuzi kuhusu ugonjwa wa kisukari, hali hiyo imeathiri moja kwa moja ufanisi wa kazi ya kinga na tiba ya ugonjwa huo."

Madaktari waliopewa mafunzo katika shughuli hizo wanaonesha hamu kubwa na kuona kuwa mafunzo kama hayo ni muhimu na ya lazima kwenye miji ya wastani na midogo na sehemu za vijijini. Kwa kuwa yanasaidia kuinua kiwango cha madaktari wa sehemu hizo. Mdaktari wa hospitali ya umma ya wilaya ya Linxia mkoani Gansu Bw. Hu Zhengqiang alisema:

"kwenye sehemu za mbali za makabila madogomadogo, kutokana na kuwa nyumba kiuchumi na kimaendeleo, teknolojia za kimatibabu za madakari kwenye sehemu hizo bado zinabaki nyuma, licha ya kutumia teknolojia mpya za matibabu ya ugonjwa huo."

Bw. Hu Zhengqiang alisema, katika miaka ya hivi karibuni, wagonjwa wa kisukari katika wilaya ya Linxia wameongezeka kwa kiasi kikubwa, na wengi wao hawakupata matibabu ya kisayansi huko. Wagonjwa wengi wanalazimishwa kwenda Lanzhou, mji mkuu wa mkoa huo kupata matibabu. Shuguli za safari ndefu ya afya kweli zimesaidia kuondoa matatizo hayo kwa wagonjwa. Bw. Hu Zhengqiang alisema:

"madaktari walioshiriki kwenye mafunzo hayo wote wanaona kuwa mafunzo hayo yamewasaidia kuinua kwa kiasi kikubwa ufahamu kuhusu ugonjwa wa kisukari, na wamejifunza ujuzi na mbinu mpya za matibabu ya ugonjwa huo."

Kwa mujibu wa takwimu husika, mpaka shughuli hizo kumalizika mwezi Juni mwaka huu, idara zaidi ya 1200 za matibabu katika ngazi ya shina zimeshiriki kwenye shughuli hizo, na madaktari zaidi ya elfu 32 wamepewa mafunzo, madatari zaidi ya elfu 18 wanatoka wilaya mbalimbali na wengine elfu 14 anatoka tarafu mbalimbali.

Mtaalamu mkuu wa kundi la wataalamu la shughuli hizo Bw. Xu Zhangrong alisema:

"shughuli za safari ndefu ya afya ni kubwa sana, watu walioshiriki shughuli hizo wamesafiri zaidi ya kilomita laki moja, na kutoa mafunzo kwa madaktari zaidi ya elfu 30 katika ngazi ya shina. "

Naibu mkuu wa idara ya kinga na udhibiti wa magonjwa katika wizara ya afya ya China Bi. Kong Lingzhi alisema, shughuli hizo zimepata mafanikio makubwa, idara husika za afya zinapaswa kujumuisha uzoefu na kuimarisha zaidi mafanikio yaliyopatikana, ili kuendelea kutoa mafunzo kwa madaktari wa sehemu za vijijini.