Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-07-25 16:56:43    
Mapishi ya kukaanga uyoga

cri

Mahitaji

Uyoga gramu 150, unga gramu 80, chembechembe za kukoleza ladha gramu 2, chumvi iliyokorogwa pamoja na pilipili manga gramu 2, ute wa mayai mawili

Njia

1. kata uyoga uwe vipande vipande, koroga pamoja na chembechembe za kukoleza ladha, chumvi na unga. Koroga ute wa mayai na unga.

2. washa moto mimina mafuta kwenye sufuria, mpaka yawe nyuzi ya joto la 50, weka vipande vya uyoga kwenye ute wa mayai na unga halafu weka kwenye sufuria vikaange mpaka viwe rangi ya hudhurungi, vipakue. Mimina chumvi iliyokorogwa pamoja na pilipili manga kwenye uyoga, mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.