Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-07-26 15:20:52    
Wanajeshi wa China wako mstari wa mbele katika kukabiliana na hatari

cri

Katika nchi nyingi duniani, majeshi yanabeba majukumu ya ulinzi na kufanya uokoaji wakati wa maafa, hali kadhalika kwa jeshi la China. China ni moja ya nchi zinazokumbwa na maafa mengi ya kimaumbile duniani, jeshi la China linawajibika na uokoaji wakati wa maafa.

Senior Colonel Tian Yixiang ni mkurugenzi wa ofisi ya kukabiliana na matukio ya dharura kwenye makao makuu ya general staff ya jeshi la ukombozi la umma la China. Alieleza kuwa tangu China mpya kuasisiwa mwaka 1949, karibu shughuli zote za kukabiliana na maafa zilishirikisha jeshi la China. Alisema  "Hususan kwenye mafuriko makubwa ya mwaka 1963 yaliyoikumba sehemu ya Huabei, tetemeko la ardhi la Xingtai mwaka 1966 na tetemeko kubwa la ardhi lililotokea miaka 10 iliyofuata huko Tangshan, moto kubwa uliowashwa milimani Daxinganling mwaka 1987 na mafuriko makubwa yaliyozikumba sehemu nyingi za China mwishoni mwa miaka ya 1990. Kila mara yalipotokea maafa makubwa ya kimaumbile, kwa uhakika jeshi la China lilishiriki kwenye shughuli za kukabiliana na maafa. Hili ni jukumu la jeshi."

Senior Colonel Tian Yixiang alieleza kuwa, wanajeshi wa China wanaweza kuwasili kwa haraka kwenye sehemu zilizoathirika na maafa, kuanza kazi mara moja na kupunguza kabisa hasara za wananchi. Ndiyo maana kila mara wanajeshi wa China wanabeba majukumu yenye shida na hatari kubwa kabisa. Alisema  "Katika kukabiliana na mafuriko makubwa mwaka 1998, wanajeshi walipelekwa kwa wakati muhimu na katika mahali muhimu. Kwa mfano mjini Jiujiang, sehemu ya ufuko ilibomolewa na mafuriko, ili kukabiliana na mafuriko makubwa, wanajeshi walipelekwa huko, tuliamini kuwa kwa uhakika waliweza kudhibiti hali isiwe mbaya zaidi."

Hivi karibuni tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 6.4 kwenye kipimo cha Richta liliikumba sehemu ya Puer mkoani Yunnan, kusini magharibi mwa China. Muda mfupi tu baada ya kutokea kwa tetemeko hilo la ardhi, wanajeshi walipelekwa huko. Waliingia shule, vijiji na viwanda, kuondoa majengo yaliyoharibika, kukarabati nyumba, kutoa matibabu na kuwaelimisha watu elimu kuhusu kujilinda kwenye tetemeko la ardhi.

Mkuu wa kampuni moja Bw. Chen Hongji alishiriki kwenye shughuli hizo, alisema "Tulifanya kila tuwezalo kuwasaidia watu walioathirika na tetemeko la ardhi. Tulipoondoa vifusi vya nyumba zao, tulihifadhi mali zao zisizoharibika kama vile madirisha, kabati n.k, ili kupunguza hasara zao."

Kuwasili kwa wanajeshi kuliwatuliza sana watu waliokumbwa na maafa hayo. Mwenyeji Bw. Zhang Yong alisema "Tulitulizwa sana baada ya kuwaona wanajeshi kufika. Ingawa matetemeko madogo ya ardhi yalikuwa bado yanaendelea, hawajali usalama wao wenyewe, walitusaidia kuondoa hali ya hatari na kuokoa mali zetu. Wao ni kama wajumbe wa serikali na chama. Kwa hakika tutaimarika zaidi, kuondoa athari za tetemeko la ardhi na kukarabati maskani yetu."

Kutokana na maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini China na kuimarika kwa nguvu ya China, wanajeshi wa China wanaanza kubeba majukumu ya uokoaji katika nchi za nje. Mwaka 2001 China iliunda kikosi cha uokoaji cha kimataifa, kikosi hicho kinaundwa na askari wahandisi, madaktari wa kijeshi na wataalamu kutoka idara ya matetemeko ya ardhi ya China. Katika miaka 6 iliyopita tangu kikosi hicho kiundwe, kilishiriki kwenye shughuli za uokoaji nchini Algeria, Iran, Pakistan zilizokumbwa na matetemeko ya ardhi na nchini Indonesia ilipoathirika na tsunami.

Kijana Zhang Jianqiang mwenye umri wa miaka 29 ni askari mhandisi kwenye kikosi hicho. Akikumbusha shughuli hizo za uokoaji, alisema alipata furaha za kuwasaidia wengine pamoja na urafiki wa watu wa nchi za nje. Alisema "Nikiwa mwanajeshi na mwokozi, nilitoa msaada kwa niaba ya taifa na watu wa China, hili ni jambo lenye fahari kubwa. Kila tulipofika sehemu iliyokumbwa na maafa, wahanga walitukaribisha sana, wakituuliza nchi tuliyotoka, tulijibu tunatoka China, wakaonesha kidole gumba wakisifu uzuri wa China."

Katiba ya kwanza ya China iliyopitishwa miaka ya 1950 inasema, jeshi la China linawajibika kulinda wananchi na amani, kushiriki kwenye ujenzi wa taifa na kuwahudumia wananchi. Mwaka 2000 China ilianza kutekeleza sheria ya ulinzi wa taifa, ikiweka bayana kwamba, jeshi la China linabeba majukumu ya kukabiliana na hali ya hatari na maafa. Hadi kufikia mwaka 2005 China ilitoa utaratibu wa jeshi kushiriki kwenye shughuli za kukabiliana na hali ya hatari na maafa, utaratibu huo unaamua kanuni, majukumu, uongozi na uhakikisho wa jeshi la China kwenye shughuli hizo.

Hivi sasa kukabiliana na matukio ya dharura yakiwemo maafa mbalimbali ni sehemu ya mkakati wa ulinzi wa taifa wa China. Kwa hiyo jeshi la China litatoa mchango mkubwa zaidi katika suala hilo, na kutekeleza jukumu la kulinda maisha ya wananchi na mali zao.

Idhaa ya kiswahili 2007-07-26   < Jeshi la China >