Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-07-27 18:21:15    
Russia yawa na msimamo imara siku hadi siku kuhusu suala la "Mkataba wa nguvu za majeshi ya kawaida ya Ulaya"

cri

Rais Vladimir Putin wa Russia tarehe 25 alisema, mwaka ule wakati "Mkataba wa nguvu za majeshi ya kawaida ya Ulaya" ulipokuwa unasainiwa kulikuwa na makundi makubwa mawili ya kijeshi yaani Jumuiya ya NATO na Jumuiya ya Mkataba wa Warsaw, hivi sasa karibu nchi zote za Ulaya ya mashariki zimejiunga na Jumuiya ya NATO, hali ya mambo imepata mabadiliko ya kimsingi, hivyo mkataba huo umekuwa haulingani na wakati huu, ndiyo maana Russia haina la kufanya ila tu kusimamisha utekelezaji wa mkataba huo na makubaliano mengine ya kimataifa yanayohusiana na mkataba huo.

Russia imekuwa na msimamo imara zaidi siku hadi siku kuhusu "Mkataba wa nguvu za majeshi ya kawaida ya Ulaya", mbali na sababu kuhusu mkataba huo haulingani na wakati, na dosari nyingi za mkataba huo, Marekani kutaka kuweka mfumo wa ulinzi dhidi ya makombora kwenye sehemu ya Ulaya ya mashariki pia ni sababu kubwa. Tokea mwanzoni mwa mwaka huu, Marekani imeshikilia msimamo wa kuweka mfumo wake wa ulinzi dhidi ya makombora katika nchi za Ulaya mashariki bila kujali upinzani mkali wa Russia, lengo lake hasa ni kupunguza nguvu ya tishio la silaha za nyuklia za Russia dhidi ya Marekani. Hakika Russia haiwezi kukaa kimya kutokana na kitendo hicho cha Marekani kinachohusiana na usalama wa nchi na maslahi makuu ya Russia.

Sababu nyingine inayoihimiza Russia iwe na msimamo imara kuhusu "Mkataba wa nguvu za majeshi ya kawaida ya Ulaya" ni kwamba Marekani haijaweza kujibu moja kwa moja pendekezo la rais Putin kuhusu suala la mfumo wa ulinzi dhidi ya makombora. Kutokana na pendekezo la Putin, mazungumzo kati ya Russia na Marekani kuhusu mfumo wa ulinzi dhidi ya makombora yanaweza kupanuliwa na kuhusisha nchi nyingine za Ulaya ambazo zina hamu na suala hilo, lakini sharti ni kwamba Marekani haitaweka mfumo wa ulinzi dhidi ya makombora nchini Jamhuri ya Czech na Poland. Rais Putin pia aliishauri Marekani itumie rada ya Russia nchini Azerbaijan katika kujenga mfumo wake wa ulinzi dhidi ya makombora, pia alisema Russia inapenda kufanya ushirikiano na Marekani. Rais Putin alisisitiza kuwa, kama Marekani itakubali pendekezo lake, kiwango cha uhusiano kati ya Russia na Marekani kitainuliwa kihalisi, yaani uhusiano huo utakuwa wa kimkakati; kama Marekani haitakubali pendekezo lake, basi uhusiano kati ya nchi hizo mbili utakuwa mbaya. Ingawa Rais George Bush wa Marekani hajakataa moja kwa moja pendekezo la Rais Putin, lakini alisisitiza kuwa nchi za Jamhuri ya Czech na Poland zinapaswa sehemu isiyotengeka kwenye mfumo wa ulinzi dhidi ya makombora, na alisema kujenga mfumo wa ulinzi dhidi ya makombora nje ya Ulaya kutachukuliwa kuwa ni nyongeza tu. Katika hali hiyo, hakika Russia inaweza kutoa jibu lake la kuonesha msimamo wake imara, ili kuzuia hali ya mikakati ya Russia na Marekani isipoteze zaidi uwiano.

Wachambuzi wanaona kuwa msimamo imara wa Russia inaouonesha siku hadi siku kuhusu "Mkataba wa nguvu za majeshi ya kawaida ya Ulaya" ni kutokana na sababu mbalimbali za kina. Kwanza Jumuiya ya NATO inayoongozwa na Marekani inaendelea kufanya upanuzi wake kwenda Ulaya mashariki, ambapo nafasi za mkakati wa Russia zinabanwa siku hadi siku, na hali ya mazingira ya usalama inazidi kuwa mbaya, hivyo Russia inataka kutoa ishara ya onyo, kama jumuiya ya NATO itaendelea kufanya hivyo, Russia itakuwa na msimamo wa kufanya kama inavyopenda na kutoshirikiana nayo. Kama ishara hiyo haitoshi kuifanya Marekani na Jumuiya ya NATO itilie maanani, basi kusimamisha utekelezaji wa "Mkataba wa nguvu za majeshi ya kawaida ya Ulaya" kwa Russia huenda kutabadilika kuwa "kujitoa" kutoka kwenye mkataba huo; pili, Russia inataka kujiandaa kwa ajili ya kujitoa kutoka kwenye mkataba huo. Kwa kuwa nchi za Jumuiya ya NATO hazijaidhinisha "Makubaliano ya marekebisho ya Mkataba wa nguvu za majeshi ya kawaida ya Ulaya", tena zinatoa matakwa mengi kwa Russia kwa kisingizio cha kuidhinisha makubaliano hayo, hivyo Russia inaona kuwa mkataba huo umekuwa mkataba usio na usawa ambao unakwamisha Russia na nchi huru za Jamhuri. Kutokana na hali hiyo, hakika Russia itajitoa kutoka kwenye mkataba huo. Zaidi ya hayo hivi sasa hali ya kisiasa na kiuchumi nchini Russia inaendelea kuwa nzuri, ambapo imani ya wananchi wa Russia kwa rais Putin inaongezeka sana, ndiyo maana Russia inathubutu kuwa na msimamo imara dhidi ya Marekani na jumuiya ya NATO.